104 Bible Verses About Fear of the Lord

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Fear of the Lord
  1. 4 Nilimtafuta Bwana naye akanijibu,

    akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

    5 Wale wamtazamao hutiwa nuru,

    nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

    6 Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia,

    akamwokoa katika taabu zake zote.

    7 Malaika wa Bwana hufanya kituo

    akiwazunguka wale wamchao,

    naye huwaokoa.

    8 Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,

    heri mtu yule anayemkimbilia.

    9 Mcheni Bwana enyi watakatifu wake,

    kwa maana wale wamchao

    hawapungukiwi na chochote.

    10 Wana simba wenye nguvu

    hutindikiwa na kuona njaa,

    bali wale wamtafutao Bwana

    hawatakosa kitu chochote kilicho chema.

    11 Njooni, watoto wangu, mnisikilize,

    nitawafundisha kumcha Bwana.

    12 Yeyote kati yenu anayependa uzima

    na kutamani kuziona siku nyingi njema,

    13 basi auzuie ulimi wake na mabaya,

    na midomo yake kutokana na kusema uongo.

    14 Aache uovu, atende mema,

    aitafute amani na kuifuatilia.

    15 Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,

    na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.

  2. 7 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,

    lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

  3. 26 Yeye amchaye Bwana ana ngome salama,

    na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.

    27 Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima,

    ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

  4. 26 “Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. 27 Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinongʼonwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba. 28 Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu. 29 Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. 31 Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

  5. 9 Mfundishe mtu mwenye hekima

    naye atakuwa na hekima zaidi;

    mfundishe mtu mwadilifu

    naye atazidi kufundishika.

    10 “Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

    na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.

    11 Kwa maana kwa msaada wangu

    siku zako zitakuwa nyingi,

    na miaka itaongezwa katika maisha yako.

  6. 12 Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana?

    Atamfundisha katika njia

    atakayoichagua kwa ajili yake.

    13 Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake,

    nao wazao wake watairithi nchi.

    14 Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao,

    yeye huwajulisha agano lake.

    15 Macho yangu humwelekea Bwana daima,

    kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa

    miguu yangu kutoka mtego.

  7. 10 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

    wote wanaozifuata amri zake wana busara.

    Sifa zake zadumu milele.

  8. 12 “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;

    ninamiliki maarifa na busara.

    13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;

    ninachukia kiburi na majivuno,

    tabia mbaya na mazungumzo potovu.

    14 Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu;

    nina ufahamu na nina nguvu.

    15 Kwa msaada wangu wafalme hutawala

    na watawala hutunga sheria zilizo za haki,

    16 kwa msaada wangu wakuu hutawala,

    na wenye vyeo wote watawalao dunia.

    17 Nawapenda wale wanipendao,

    na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

    18 Utajiri na heshima viko kwangu,

    utajiri udumuo na mafanikio.

  9. 16 Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.

    Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Kwa njia hii, pendo hukamilishwa miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu. 18 Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.

    19 Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

  10. 7 Sheria ya Bwana ni kamilifu,

    ikihuisha nafsi.

    Shuhuda za Bwana ni za kuaminika,

    zikimpa mjinga hekima.

    8 Maagizo ya Bwana ni kamili,

    nayo hufurahisha moyo.

    Amri za Bwana huangaza,

    zatia nuru machoni.

    9 Kumcha Bwana ni utakatifu,

    nako kwadumu milele.

    Amri za Bwana ni za hakika,

    nazo zina haki.

    10 Ni za thamani kuliko dhahabu,

    kuliko dhahabu iliyo safi sana,

    ni tamu kuliko asali,

    kuliko asali kutoka kwenye sega.

    11 Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,

    katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

  11. 13 Hii ndiyo jumla ya maneno;

    yote yamekwisha sikiwa:

    Mche Mungu, nawe uzishike amri zake,

    maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

    14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi,

    pamoja na kila neno la siri,

    likiwa jema au baya.

  12. 23 Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima,

    kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,

    bila kuguswa na shida.

  13. 28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

    ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

    nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

  14. 11 Mtumikieni Bwana kwa hofu

    na mshangilie kwa kutetemeka.

  15. 31 Ndipo kanisa katika Uyahudi wote, Galilaya na Samaria likafurahia wakati wa amani. Likatiwa nguvu, na kwa faraja ya Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka, na likaendelea kudumu katika kumcha Bwana.

  16. 18 Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali 19 na wakamwambia Mose, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.”

    20 Mose akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.”

    21 Watu wakabaki mbali, wakati Mose alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa.

  17. 8 Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;

    si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

    9 Yeye hatalaumu siku zote,

    wala haweki hasira yake milele,

    10 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu

    wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.

    11 Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,

    ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;

    12 kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

    ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.

    13 Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,

    ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;

  18. 16 Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana,

    kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

  19. 6 Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa;

    kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.

  20. 28 Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji, 29 kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”

  21. 12 Kwa hiyo, wapenzi wangu, kama vile ambavyo mmekuwa mkitii siku zote, si tu wakati nikiwa pamoja nanyi, bali sasa zaidi sana nisipokuwepo, utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka, 13 kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi lake jema.

  22. 27 Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha,

    lakini miaka ya mwovu inafupishwa.

    28 Tarajio la mwenye haki ni furaha,

    bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.

    29 Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki,

    lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.

  23. 13 Kwa ajili ya Bwana, tiini kila mamlaka iliyowekwa na wanadamu: Kwa mfalme kwani ndiye aliye na mamlaka ya juu zaidi, 14 au kwa maafisa aliowaweka, kwa kuwa mfalme amewatuma ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale watendao mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema mnyamazishe maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16 Ishini kama watu huru, lakini msitumie uhuru wenu kama kisingizio cha kutenda uovu, bali ishini kama watumishi wa Mungu. 17 Mheshimuni kila mtu ipasavyo: Wapendeni jamaa ya ndugu waumini, mcheni Mungu, mpeni heshima mfalme.

  24. 12 Na sasa, ee Israeli, Bwana Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha Bwana Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, 13 na kuyashika maagizo ya Bwana na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

    14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako.

  25. 1 Msifuni Bwana.

    Heri mtu yule amchaye Bwana,

    mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

    2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,

    kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

    3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,

    haki yake hudumu milele.

  26. 11 Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana,

    yeye ni msaada na ngao yao.

    12 Bwana anatukumbuka na atatubariki:

    ataibariki nyumba ya Israeli,

    ataibariki nyumba ya Aroni,

    13 atawabariki wale wanaomcha Bwana,

    wadogo kwa wakubwa.

    14 Bwana na awawezeshe kuongezeka,

    ninyi na watoto wenu.

    15 Mbarikiwe na Bwana

    Muumba wa mbingu na dunia.

  27. 1 Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.

  28. 6 Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,

    jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.

    7 Ameyakusanya maji ya bahari

    kama kwenye chungu;

    vilindi vya bahari

    ameviweka katika ghala.

    8 Dunia yote na imwogope Bwana,

    watu wote wa dunia wamche.

    9 Kwa maana Mungu alisema, na ikawa,

    aliamuru na ikasimama imara.

  29. Wimbo wa kwenda juu.

    1 Heri ni wale wote wamchao Bwana,

    waendao katika njia zake.

    2 Utakula matunda ya kazi yako;

    baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

    3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao

    ndani ya nyumba yako;

    wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni

    kuizunguka meza yako.

    4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa

    mtu amchaye Bwana.

  30. 4 “Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. 5 Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!

  31. 5 Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma. 6 Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili ya Bwana ambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu. 7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Bwana Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa.”

  32. 11 Ee Bwana, nifundishe njia yako,

    nami nitakwenda katika kweli yako;

    nipe moyo usiositasita,

    ili niweze kulicha jina lako.

    12 Ee Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote;

    nitaliadhimisha jina lako milele.

  33. 12 “Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina,

    usiogope kile wanachokiogopa,

    wala usikihofu.

    13 Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake

    ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu,

    ndiye peke yake utakayemwogopa,

    ndiye peke yake utakayemhofu,

    14 naye atakuwa mahali patakatifu;

    lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa

    jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa

    na mwamba wa kuwaangusha.

    Kwa watu wa Yerusalemu,

    atakuwa mtego na tanzi.

  34. 14 “Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele za Bwana Mwenye Nguvu Zote? 15 Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda mabaya wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ”

    16 Ndipo wale waliomcha Bwana wakasemezana wao kwa wao, naye Bwana akasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha Bwana na kuliheshimu jina lake.

    17 “Nao watakuwa watu wangu,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, “katika siku ile nitakapowafanya watu kuwa hazina yangu. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia. 18 Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.

  35. 26 Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. 27 Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu. 28 Yeyote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu. 29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema? 30 Kwa kuwa tunamjua yeye aliyesema, “Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.” Tena asema, “Bwana atawahukumu watu wake.” 31 Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.

  36. 6 Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. 7 Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”

  37. 17 Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi,

    bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.

    18 Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako,

    nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.

  38. 3 Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,

    Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?

    4 Lakini kwako kuna msamaha,

    kwa hiyo wewe unaogopwa.

  39. 1 Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu

    na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,

    2 kutega sikio lako kwenye hekima

    na kuweka moyo wako katika ufahamu,

    3 na kama ukiita busara

    na kuita kwa sauti ufahamu,

    4 na kama utaitafuta kama fedha

    na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,

    5 ndipo utakapoelewa kumcha Bwana

    na kupata maarifa ya Mungu.

    6 Kwa maana Bwana hutoa hekima,

    na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

  40. 18 Bwana yu karibu na wote wamwitao,

    karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

    19 Huwatimizia wamchao matakwa yao,

    husikia kilio chao na kuwaokoa.

  41. 38 Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. 39 Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao. 40 Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kamwe wasigeukie mbali nami.

  42. 9 Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana. 10 Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.

    11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Bwana, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. 12 Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. 13 Kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu; kama tuna akili timamu, ni kwa ajili yenu. 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. 15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao.

  43. 10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi,

    wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.

    11 Bwana hupendezwa na wale wamchao,

    wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.

  44. 20 Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,

    hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;

    21 kwenye makutano ya barabara za mji

    zenye makelele mengi hupaza sauti,

    kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:

    22 “Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?

    Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha,

    na wapumbavu kuchukia maarifa?

    23 Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,

    ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu

    na kuwafahamisha maneno yangu.

    24 Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita

    na hakuna yeyote aliyekubali

    niliponyoosha mkono wangu,

    25 kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote

    na hamkukubali karipio langu,

    26 mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,

    nitawadhihaki wakati janga litawapata:

    27 wakati janga litawapata kama tufani,

    wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,

    wakati dhiki na taabu zitawalemea.

    28 “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;

    watanitafuta lakini hawatanipata.

    29 Kwa kuwa walichukia maarifa,

    wala hawakuchagua kumcha Bwana,

    30 kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,

    na kukataa maonyo yangu,

    31 watakula matunda ya njia zao,

    na watashibishwa matunda ya hila zao.

  45. 50 Rehema zake huwaendea wale wamchao,

    kutoka kizazi hadi kizazi.

  46. 9 Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 10 Kama ilivyoandikwa:

    “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

    11 Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,

    hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

    12 Wote wamepotoka,

    wote wameoza pamoja;

    hakuna atendaye mema,

    naam, hakuna hata mmoja.”

    13 “Makoo yao ni makaburi wazi;

    kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”

    “Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”

    14 “Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”

    15 “Miguu yao ina haraka kumwaga damu;

    16 maangamizi na taabu viko katika njia zao,

    17 wala njia ya amani hawaijui.”

    18 “Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.”

  47. 23 Kwa maana Bwana Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Bwana Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka. 24 Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Bwana ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha Bwana Mungu wenu.”

  48. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

    wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

    6 katika njia zako zote mkiri yeye,

    naye atayanyoosha mapito yako.

    7 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;

    mche Bwana ukajiepushe na uovu.

  49. 33 Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima,

    nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

  50. 4 Unyenyekevu na kumcha Bwana

    huleta utajiri, heshima na uzima.

  51. 5 Bwana ametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka,

    ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu.

    6 Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu,

    ghala za wokovu tele, hekima na maarifa;

    kumcha Bwana ni ufunguo wa hazina hii.

  52. 6 Siku moja wana wa Mungu walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani naye akaja pamoja nao. 7 Bwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”

    Shetani akamjibu Bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

    8 Ndipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”

    9 Shetani akamjibu Bwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? 10 Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima.

  53. 23 Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni!

    Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye!

    Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!

  54. 18 Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao,

    kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,

    19 ili awaokoe na mauti,

    na kuwahifadhi wakati wa njaa.

  55. 10 Ndipo pia, nikaona waovu wakizikwa, wale ambao walizoea kuingia na kutoka mahali patakatifu na kupewa sifa katika mji ambapo walikuwa wamefanya haya. Hili nalo ni ubatili.

    11 Wakati hukumu juu ya tendo ovu haitekelezwi upesi, mioyo ya watu hujaa mipango ya kutenda maovu. 12 Ingawa mtu mwovu hufanya maovu mia moja na akaendelea kuishi maisha marefu, najua kwamba itakuwa bora zaidi kwa watu wanaomwogopa Mungu, wamchao Mungu. 13 Lakini kwa sababu waovu hawamwogopi Mungu, hawatafanikiwa, maisha yao hayatarefuka kama kivuli.

  56. 1 Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese,

    kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.

    2 Roho wa Bwana atakaa juu yake,

    Roho wa hekima na wa ufahamu,

    Roho wa shauri na wa uweza,

    Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana

    3 naye atafurahia kumcha Bwana.

    Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,

    wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

    4 bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,

    kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.

    Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,

    kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.

    5 Haki itakuwa mkanda wake

    na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.

  57. 7 Kisha mabaharia wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tupige kura tumtafute anayehusika na maafa haya.” Wakapiga kura, kura ikamwangukia Yona.

    8 Kwa hiyo walimuuliza, “Tuambie, ni nani anayehusika kwa kutuletea tatizo hili lote? Unafanya kazi gani? Umetoka wapi? Nchi yako ni ipi? Wewe ni kutoka taifa lipi?”

    9 Akajibu, “Mimi ni Mwebrania, nami namwabudu Bwana, Mungu wa Mbinguni, aliyeumba bahari na nchi kavu.”

    10 Hili liliwaogopesha nao wakamuuliza,

    “Umefanya nini?” (Walijua alikuwa anamkimbia Bwana, kwa sababu alishawaambia hivyo.)

    11 Bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Kwa hiyo walimuuliza, “Tukutendee nini ili kufanya bahari itulie kwa ajili yetu?”

    12 Akawajibu, “Niinueni mnitupe baharini, nayo itakuwa shwari. Ninajua mawimbi haya makubwa yamewatokea kwa ajili ya kosa langu.”

    13 Badala yake, wale watu walijitahidi kupiga makasia wawezavyo ili wapate kurudi pwani. Lakini hawakuweza, kwa kuwa bahari ilizidi kuchafuka kuliko mwanzo. 14 Ndipo wakamlilia Bwana, “Ee Bwana, tafadhali usituue kwa kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umefanya kama ilivyokupendeza.” 15 Kisha walimchukua Yona, wakamtupa baharini nayo bahari iliyokuwa imechafuka ikatulia. 16 Katika jambo hili watu wakamwogopa Bwana sana, wakamtolea Bwana dhabihu na kumwekea nadhiri.

  58. 13 Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake. 14 Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; 15 kwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi.

  59. 24 Lakini hakikisheni mnamcha Bwana na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote; tafakarini mambo makubwa aliyoyatenda kwa ajili yenu. 25 Hata hivyo mkiendelea kufanya uovu, ninyi na mfalme wenu mtafutiliwa mbali!”

  60. 3 Mungu wa Israeli alinena,

    mwamba wa Israeli akaniambia:

    ‘Mtu anatawala watu kwa haki,

    wakati anapotawala

    akiwa na hofu ya Mungu,

    4 yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo

    asubuhi isiyo na mawingu,

    kama mwanga baada ya mvua

    uchipuzao majani kutoka ardhini.’

  61. 14 Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana,

    bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu

    huangukia kwenye taabu.

  62. 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu. 15 Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, “Abba, yaani, Baba,”

  63. 6 Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu. 7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

  64. 8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”

    10 Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.”

    11 Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”

    12 Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.”

    13 Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”

  65. 9 Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 10 Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 11 Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”

    Akajibu, “Mimi hapa.”

    12 Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

    13 Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”

  66. 17 Lakini kutoka milele hata milele

    upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,

    nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

    18 kwa wale walishikao agano lake

    na kukumbuka kuyatii mausia yake.

  67. 15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16 mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana. 18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

    21 Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.

  68. 7 Kwa imani, Noa alipoonywa na Mungu kuhusu mambo ambayo hayajaonekana bado, kwa kumcha Mungu alitengeneza safina ili kuokoa jamaa yake. Kwa imani yake aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

  69. 3 Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema:

    “Bwana Mungu Mwenyezi,

    matendo yako ni makuu na ya ajabu.

    Njia zako wewe ni za haki na za kweli,

    Mfalme wa nyakati zote!

    4 Ni nani ambaye hatakuogopa wewe Bwana

    na kulitukuza jina lako?

    Kwa kuwa wewe peke yako ndiwe mtakatifu.

    Mataifa yote yatakuja

    na kuabudu mbele zako,

    kwa kuwa matendo yako ya haki

    yamedhihirishwa.”

  70. 21 Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.

  71. 5 Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako,

    uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.

    6 Kwa kuwa ni nani katika mbingu

    anayeweza kulinganishwa na Bwana?

    Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni

    aliye kama Bwana?

    7 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana,

    anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

    8 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

    ni nani aliye kama wewe?

    Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu,

    na uaminifu wako unakuzunguka.

  72. 1 Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia. 2 Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima. 3 Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”

    4 Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?”

    Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. 5 Sasa tuma watu waende Yafa wakamwite mtu mmoja jina lake Simoni aitwaye Petro. 6 Yeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”

    7 Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia. 8 Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa.

  73. 34 Ndipo Petro akafungua kinywa chake akasema, “Mungu hana upendeleo, 35 Lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye.

  74. 5 Nanyi mmesahau yale maneno ya kuwaonya yanayowataja ninyi kuwa wana, yakisema:

    “Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana,

    wala usikate tamaa akikukemea,

    6 kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,

    na humwadhibu kila mmoja

    anayemkubali kuwa mwana.”

    7 Vumilieni taabu kwa ajili ya kufunzwa adabu. Mungu anawatendea ninyi kama watoto wake, kwa maana ni mtoto yupi asiyeadibishwa na mzazi wake? 8 Kama hakuna kuadibishwa (ambalo ni fungu la watoto wote), basi ninyi ni watoto wa haramu wala si watoto halali. 9 Tena, sisi sote tunao baba wa kimwili, waliotuadibisha nasi tukawaheshimu kwa ajili ya hilo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa Baba wa roho zetu ili tuishi? 10 Baba zetu walituadibisha kwa kitambo kidogo kama wao wenyewe walivyoona vyema, lakini Mungu hutuadibisha kwa faida yetu ili tupate kushiriki utakatifu wake. 11 Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.

  75. 17 Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni. 18 Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, 19 bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa. 20 Yeye alichaguliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 21 Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu.

  76. 1 Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki, 2 ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu.

  77. 1 Hili ndilo asemalo Bwana,

    “Mbingu ni kiti changu cha enzi,

    nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

    Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?

    Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

    2 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

    hivyo vikapata kuwepo?”

    asema Bwana.

    “Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

    yeye ambaye ni mnyenyekevu

    na mwenye roho yenye toba,

    atetemekaye asikiapo neno langu.

  78. 18 Siku ya tatu Yosefu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu:

  79. 4 Ni Bwana Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.

  80. Sehemu Ya Kwanza: Habari Za Awali

    1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.

  81. 19 Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,

    uliowawekea akiba wakuchao,

    ambao huwapa wale wakukimbiliao

    machoni pa watu.

    20 Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako

    kutokana na hila za wanadamu;

    katika makao yako huwaweka salama

    kutokana na ndimi za mashtaka.

  82. 25 Kuwaogopa watu huwa ni mtego,

    bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.

  83. 19 Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,

    na kwenye mahandaki ardhini

    kutokana na utisho wa Bwana

    na utukufu wa enzi yake,

    ainukapo kuitikisa dunia.

    20 Siku ile, watu watawatupia

    panya na popo

    sanamu zao za fedha na za dhahabu,

    walizozitengeneza ili waziabudu.

    21 Watakimbilia kwenye mapango miambani

    na kwenye nyufa za miamba

    kutokana na utisho wa Bwana

    na utukufu wa enzi yake,

    ainukapo kuitikisa dunia.

  84. 17 Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka shina la mzeituni, 18 basi usijivune juu ya hayo matawi. Kama ukijivuna, kumbuka jambo hili: si wewe unayelishikilia shina, bali ni shina linalokushikilia wewe. 19 Basi utasema, “Matawi yale yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika hilo shina.” 20 Hii ni kweli. Matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwake, lakini wewe umesimama tu kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijivune, bali simama kwa kuogopa. 21 Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, wala hatakuhurumia wewe.

    22 Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali. 23 Wao nao wasipodumu katika kutokuamini kwao, watapandikizwa tena kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena kwenye hilo shina. 24 Ikiwa wewe ulikatwa kutoka kile ambacho kwa asili ni mzeituni mwitu na kupandikizwa kinyume cha asili kwenye mzeituni uliopandwa, si rahisi zaidi matawi haya ya asili kupandikizwa tena kwenye shina lake la mzeituni!

  85. 22 Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.

  86. 19 Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.

  87. 13 Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? 14 Lakini mmebarikiwa hata kama ikiwalazimu kuteseka kwa ajili ya haki. “Msiogope vitisho vyao, wala msiwe na wasiwasi.” 15 Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, 16 mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao.

    17 Kwa maana ni afadhali kupata mateso kwa ajili ya kutenda mema, kama kuteseka huko ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu.

  88. 14 “ ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

  89. 29 Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!

  90. 20 Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake. 21 Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.

  91. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana.

    1 Kuna neno moyoni mwangu

    kuhusu hali ya dhambi ya mwovu.

    Hakuna hofu ya Mungu

    mbele ya macho yake.

    2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno

    hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.

    3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,

    ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.

    4 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,

    hujitia katika njia ya dhambi

    na hakatai lililo baya.

  92. 30 Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi,

    bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.

  93. 14 Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.

  94. 10 Ingieni kwenye miamba,

    jificheni ardhini

    kutokana na utisho wa Bwana

    na utukufu wa enzi yake!

  95. 1 Katika mwaka ule Mfalme Uzia alikufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza Hekalu. 2 Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao, na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3 Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake:

    “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

    ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;

    dunia yote imejaa utukufu wake.”

    4 Kwa sauti zao, miimo ya milango na vizingiti vilitikisika, nalo Hekalu likajaa moshi.

    5 Ndipo nikalia, “Ole wangu! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

  96. 40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu iyo hiyo?

  97. 5 Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema:

    “Msifuni Mungu wetu,

    ninyi watumishi wake wote,

    ninyi nyote mnaomcha,

    wadogo kwa wakubwa!”

    6 Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema:

    “Haleluya!

    Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala.

    7 Tufurahi, tushangilie

    na kumpa utukufu!

    Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia

    na bibi arusi wake amejiweka tayari.

    8 Akapewa kitani safi, nyeupe

    inayongʼaa, ili avae.”

    (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)

    9 Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’ ” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.”

  98. 17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi.

  99. 18 Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi. 19 Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu Bwana Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, 20 naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

  100. 14 “Sasa basi mcheni Bwana na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ngʼambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieni Bwana. 15 Lakini msipoona vyema kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana.”

  101. 14 Kama mkimcha Bwana na kumtumikia na kumtii nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayetawala juu yenu mkimfuata Bwana, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu! 15 Lakini kama hamkumtii Bwana, nanyi kama mkiasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu.

  102. 9 Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao,

    ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.

  103. 19 Uovu wako utakuadhibu;

    kurudi nyuma kwako kutakukemea.

    Basi kumbuka, utambue

    jinsi lilivyo ovu na chungu kwako

    unapomwacha Bwana Mungu wako

    na kutokuwa na hofu yangu,”

    asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  104. 22 Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Bwana.

    “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu?

    Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari,

    kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita.

    Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita;

    yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.

    23 Lakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi,

    wamegeukia mbali na kwenda zao.

    24 Wao hawaambiani wenyewe,

    ‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu,

    anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,

    anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’