58 Bible Verses About Understanding

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Understanding
  1. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

    wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

    6 katika njia zako zote mkiri yeye,

    naye atayanyoosha mapito yako.

    7 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;

    mche Bwana ukajiepushe na uovu.

  2. 9 Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu. 10 Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu, 11 mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha 12 mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru.

  3. 7 Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo hayo yote.

  4. 28 Wao ni taifa lisilo na akili,

    hakuna busara ndani yao.

    29 Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili,

    na kutambua mwisho wao utakuwa aje!

  5. 13 Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano:

    “Ingawa wanatazama, hawaoni;

    wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi.

    14 Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema:

    “ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

    na pia mtatazama lakini hamtaona.

    15 Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

    hawasikii kwa masikio yao,

    na wamefumba macho yao.

    Wasije wakaona kwa macho yao,

    na wakasikiliza kwa masikio yao,

    wakaelewa kwa mioyo yao,

    na kugeuka nami nikawaponya.’

  6. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana.

  7. 5 Tazama, nimewafundisha amri na sheria kama Bwana Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki. 6 Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.”

  8. 29 Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari.

  9. 12 Bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya Bwana Mungu wako.

  10. 104 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako,

    kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

  11. 11 Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano, 12 ili,

    “ ‘daima waone lakini wasitambue,

    daima wasikie lakini wasielewe;

    wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ”

  12. 25 Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho Mtakatifu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:

    26 “ ‘Nenda kwa watu hawa na useme,

    “Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

    na pia mtatazama, lakini hamtaona.”

    27 Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

    hawasikii kwa masikio yao,

    na wamefumba macho yao.

    Wasije wakaona kwa macho yao,

    na wakasikiliza kwa masikio yao,

    wakaelewa kwa mioyo yao,

    na kugeuka nami nikawaponya.’

  13. 17 Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

    20 Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo. 21 Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 22 Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, 23 ili mfanywe upya roho na nia zenu, 24 mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

  14. 20 Nasi pia twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi ufahamu ili tupate kumjua yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani yake yeye aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele.

  15. 8 “Ukaulize vizazi vilivyotangulia

    na uone baba zao walijifunza nini,

    9 kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote,

    nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.

    10 Je, hawatakufundisha na kukueleza?

    Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

  16. 28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

    ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

    nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

  17. 9 Usiwe kama farasi au nyumbu

    wasio na akili,

    ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu

    la sivyo hawatakukaribia.

  18. 6 Kwa maana Bwana hutoa hekima,

    na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

  19. 14 Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu;

    nina ufahamu na nina nguvu.

  20. 10 “Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

    na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.

  21. 12 Mtu asiye na akili humdharau jirani yake,

    bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.

  22. 11 Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,

    bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

  23. 15 Ufahamu mzuri hupata upendeleo,

    bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.

  24. 27 Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia,

    naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.

  25. 1 Mtu ajitengaye na wengine

    hufuata matakwa yake mwenyewe;

    hupiga vita kila shauri jema.

    2 Mpumbavu hafurahii ufahamu,

    bali hufurahia kutangaza

    maoni yake mwenyewe.

  26. 30 Nilipita karibu na shamba la mvivu,

    karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,

    31 miiba ilikuwa imeota kila mahali,

    ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na

    ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.

  27. 22 “Watu wangu ni wapumbavu,

    hawanijui mimi.

    Ni watoto wasio na akili,

    hawana ufahamu.

    Ni hodari kutenda mabaya,

    hawajui kutenda yaliyo mema.”

  28. 10 Naye akasema, “Ninyi mmepewa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili,

    “ ‘ingawa wanatazama, wasione;

    ingawa wanasikiliza, wasielewe.’

  29. 45 Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko.

  30. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.

  31. 4 Umezifunga akili zao zisipate ufahamu,

    kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.

  32. 8 Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu,

    pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.

  33. 10 “Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu.

    Kamwe Mungu hatendi uovu,

    Mwenyezi hafanyi kosa.

    11 Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda;

    huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili.

  34. 36 Ni nani aliyeujalia moyo hekima

    au kuzipa akili ufahamu?

  35. 34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako

    na kuitii kwa moyo wangu wote.

  36. 130 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,

    kunampa mjinga ufahamu.

  37. 5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,

    ufahamu wake hauna kikomo.

  38. 1 Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu;

    sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu.

  39. 2 Roho wa Bwana atakaa juu yake,

    Roho wa hekima na wa ufahamu,

    Roho wa shauri na wa uweza,

    Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana

  40. 28 Je wewe, hufahamu?

    Je wewe, hujasikia?

    Bwana ni Mungu wa milele,

    Muumba wa miisho ya dunia.

    Hatachoka wala kulegea,

    wala hakuna hata mmoja

    awezaye kuupima ufahamu wake.

  41. 10 “Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,

    “na mtumishi wangu niliyemchagua,

    ili mpate kunijua na kuniamini,

    na kutambua kwamba Mimi ndiye.

    Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa,

    wala hatakuwepo mwingine baada yangu.

  42. 24 lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:

    kwamba ananifahamu na kunijua mimi,

    kwamba mimi ndimi Bwana, nitendaye wema,

    hukumu na haki duniani,

    kwa kuwa napendezwa na haya,”

    asema Bwana.

  43. 21 Yeye hubadili nyakati na majira;

    huwaweka wafalme na kuwaondoa.

    Huwapa hekima wenye hekima,

    na maarifa wenye ufahamu.

  44. 23 Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.”

  45. 18 Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi? 19 Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Yesu alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni “safi.”)

    20 Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21 Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, 22 tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”

  46. 30 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.’ 31 Ya pili ndiyo hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”

    32 Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu zote.”

    34 Yesu alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumuuliza maswali tena.

  47. 32 Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”

    33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?”

  48. 43 Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. 45 Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini!

  49. 40 “Amewafanya vipofu,

    na kuifanya mioyo yao kuwa migumu,

    ili wasiweze kuona kwa macho yao,

    wala kuelewa kwa mioyo yao,

    wasije wakageuka nami nikawaponya.”

  50. 30 Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, “Je, unaelewa hayo usomayo?”

    31 Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.

  51. 18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, 19 kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameyadhihirisha kwao. 20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

    21 Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza.

  52. 21 Lakini kama ilivyoandikwa:

    “Wale ambao hawajahubiriwa habari zake wataona,

    nao wale ambao hawajazisikia watafahamu.”

  53. 16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. 17 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. 18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu 19 na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 20 aliyoitumia katika Kristo alipomfufua kutoka kwa wafu, na akamketisha mkono wake wa kuume huko mbinguni, 21 juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia. 22 Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23 ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote.

  54. 14 Kwa sababu hii nampigia Baba magoti, 15 ambaye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unatokana naye. 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, 17 ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo, 18 mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo, 19 na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.

  55. 9 Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, 10 ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo,

  56. 7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

  57. 3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana havikuumbwa kutoka kwa vitu vinavyoonekana.

  58. 13 Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.