31 Bible Verses About Thanksgiving

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Thanksgiving
  1. 16 Furahini siku zote; 17 ombeni bila kukoma; 18 shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

  2. 18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

    21 Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.

  3. 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

    na katika nyua zake kwa kusifu,

    mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

    5 Kwa maana Bwana ni mwema

    na upendo wake wadumu milele;

    uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

  4. 10 Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. 11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

    12 Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu. 13 Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote. 14 Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu. 15 Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

  5. 34 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

    upendo wake wadumu milele.

  6. 6 Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

  7. 15 Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. 17 Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.

  8. 2 Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru.

  9. 15 Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.

  10. 15 Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.

  11. 18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, 19 kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameyadhihirisha kwao. 20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

    21 Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza.

  12. 7 Ndani yake tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake

  13. 6 Hivyo basi, kama vile mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kukaa ndani yake, 7 mkiwa na mizizi, na mmejengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.

  14. 9 Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 10 Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema:

    “Wokovu una Mungu wetu,

    yeye aketiye kwenye kiti cha enzi,

    na Mwana-Kondoo!”

    11 Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, 12 wakisema:

    “Amen!

    Sifa na utukufu

    na hekima na shukrani na heshima

    na uweza na nguvu

    viwe kwa Mungu wetu milele na milele.

    Amen!”

  15. 2 Tuje mbele zake kwa shukrani,

    tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

  16. KITABU CHA TANO

    1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema,

    upendo wake wadumu milele.

  17. 1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

    upendo wake wadumu milele.

  18. 4 Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu. 5 Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote, 6 kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Kristo ulithibitishwa ndani yenu. 7 Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 8 Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

  19. 3 Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. 4 Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, 5 kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo.

  20. 3 Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka. 4 Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.

  21. 11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,

    ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

    12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.

    Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

  22. 18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,

    nitakusifu katikati ya watu wengi.

  23. 6 Nitakutolea dhabihu za hiari;

    Ee Bwana, nitalisifu jina lako

    kwa kuwa ni vyema.

    7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote,

    na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.

  24. 30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,

    nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.

  25. Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.

    1 Ni vyema kumshukuru Bwana

    na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

    2 kuutangaza upendo wako asubuhi,

    na uaminifu wako wakati wa usiku,

    3 kwa zeze yenye nyuzi kumi

    na kwa sauti ya kinubi.

    4 Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,

    nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

  26. 21 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

    na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

    22 Na watoe dhabihu za kushukuru,

    na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.

  27. 17 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru

    na kuliita jina la Bwana.

  28. 9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

    nitakutolea dhabihu.

    Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

    Wokovu watoka kwa Bwana.”

  29. 25 Wakati huo Yesu alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo.

  30. 57 Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

  31. 3 Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi, 4 kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote: 5 imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili 6 iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote. 7 Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu, 8 ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.