69 Bible Verses About Harvest

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Harvest
  1. 35 Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi. 36 Alipoona makutano, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. 37 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. 38 Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.”

  2. 34 Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake. 35 Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! 36 Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja. 37 Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”

  3. 7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. 8 Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9 Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. 10 Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.

  4. 18 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri.

    19 “Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ngʼombe au wa kondoo au mbuzi. 20 Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume.

    “Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.

    21 “Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike.

    22 “Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka.

  5. 9 Bwana akamwambia Mose, 10 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa nafaka ya kwanza mtakayovuna.

  6. 13 Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wafu wafao katika Bwana tangu sasa.”

    “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”

    14 Nikatazama, hapo mbele yangu palikuwa na wingu jeupe, na aliyekuwa ameketi juu ya hilo wingu alikuwa “kama Mwana wa Adamu” mwenye taji ya dhahabu kichwani mwake na mundu mkali mkononi mwake. 15 Kisha malaika mwingine akaja kutoka hekaluni naye akamwita kwa sauti kubwa yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akasema, “Chukua mundu wako ukavune kwa kuwa wakati wa mavuno umewadia, kwa maana mavuno ya dunia yamekomaa.” 16 Hivyo yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akauzungusha mundu wake duniani, nayo dunia ikavunwa.

    17 Malaika mwingine akatoka katika hekalu lililoko mbinguni, naye pia alikuwa na mundu mkali. 18 Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.” 19 Hivyo yule malaika akauzungusha mundu wake duniani na kukusanya zabibu za dunia na kuzitupa kwenye shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu. 20 Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasi, kwa umbali wa maili 200.

  7. 22 “Kwa muda dunia idumupo,

    wakati wa kupanda na wa kuvuna,

    wakati wa baridi na wa joto,

    wakati wa kiangazi na wa masika,

    usiku na mchana

    kamwe havitakoma.”

  8. 5 Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi

    ni mwana mwenye hekima,

    lakini yeye alalaye wakati wa mavuno

    ni mwana mwenye kuaibisha.

  9. 3 Umelikuza taifa,

    na kuzidisha furaha yao,

    wanafurahia mbele zako,

    kama watu wanavyofurahia wakati wa mavuno,

    kama watu wafurahivyo

    wagawanyapo nyara.

  10. 24 Wao hawaambiani wenyewe,

    ‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu,

    anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,

    anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’

  11. 36 Kisha Yesu akaagana na makutano, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”

    37 Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu. 38 Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. 39 Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika.

    40 “Kama vile magugu yangʼolewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia.

  12. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno. 3 Haya! nendeni. Ninawatuma kama wana-kondoo katikati ya mbwa mwitu. 4 Msichukue mkoba, wala mfuko, wala viatu, na msimsalimu mtu yeyote njiani.

  13. 9 “ ‘Wakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako. 10 Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

  14. 17 Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba Bwana ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya Bwana mlipoomba mfalme.”

    18 Kisha Samweli akamwomba Bwana, na siku ile ile Bwana akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana Bwana na Samweli.

  15. 12 “Mataifa na yaamshwe;

    na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati,

    kwa kuwa nitaketi mahali pale

    kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.

    13 Tia mundu,

    kwa kuwa mavuno yamekomaa.

    Njooni, mkanyage zabibu,

    kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa

    na mapipa yanafurika:

    kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”

  16. 30 Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”

  17. 10 Mmemsahau Mungu Mwokozi wenu,

    hamkumkumbuka Mwamba aliye ngome yenu.

    Kwa hiyo, hata ingawa mlipandikiza mimea iliyo mizuri sana

    na kuotesha mizabibu ya kigeni,

    11 hata kama siku ile unapoipandikiza, unaifanya iote

    na asubuhi ile ile unayoipanda, unaifanya ichipue,

    hata hivyo mavuno yatakuwa kama si kitu

    katika siku ile ya ugonjwa na maumivu yasiyoponyeka.

  18. 7 “Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu

    kabla ya kufikia mavuno.

    Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja,

    lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine.

    Shamba moja lilipata mvua,

    na lingine halikupata, nalo likakauka.

  19. 19 Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili Bwana Mungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako. 20 Unapovuna zeituni kutoka miti yako, usirudie matawi mara ya pili. Acha kilichobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane. 21 Unapochuma zabibu katika shamba lako la mizabibu usirudie tena. Acha zinazobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane.

  20. 4 Hili ndilo Bwana aliloniambia:

    “Nitatulia kimya na kutazama

    kutoka maskani yangu,

    kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,

    kama wingu la umande

    katika joto la wakati wa mavuno.”

    5 Kwa maana, kabla ya mavuno,

    wakati wa kuchanua ukishapita

    na maua yakawa zabibu zinazoiva,

    atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi,

    naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.

  21. 26 Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27 Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. 28 Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. 29 Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.”

  22. 5 Wapandao kwa machozi

    watavuna kwa nyimbo za shangwe.

    6 Yeye azichukuaye mbegu zake

    kwenda kupanda, huku akilia,

    atarudi kwa nyimbo za shangwe,

    akichukua miganda ya mavuno yake.

  23. 1 Bwana akamwambia Mose katika Mlima Sinai, 2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili ya Bwana. 3 Kwa miaka sita mtapanda mazao katika mashamba yenu, nanyi kwa miaka sita mtaikata mizabibu yenu matawi na kuvuna mazao yake. 4 Lakini mwaka wa saba nchi lazima iwe na Sabato ya mapumziko, Sabato kwa Bwana. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi. 5 Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko. 6 Chochote nchi itoacho katika mwaka wa Sabato kitakuwa chakula chenu wenyewe, watumishi wenu wa kiume na wa kike, mfanyakazi aliyeajiriwa, na mkazi wa muda anayeishi miongoni mwenu, 7 vilevile malisho ya mifugo yenu na wanyama pori katika nchi yenu. Chochote nchi itakachozalisha kinaweza kuliwa.

  24. 1 Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno,

    ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.

  25. 33 Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:

    “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria

    wakati inapokanyagwa;

    wakati wa kumvuna utakuja upesi.”

  26. 22 “ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

  27. 9 Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo,

    kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.

    Ee Heshboni, ee Eleale,

    ninakulowesha kwa machozi!

    Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva

    na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.

  28. 11 “Pia kwa ajili yako, Yuda,

    mavuno yameamriwa.

    “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,

  29. 11 Uaminifu huchipua kutoka nchi,

    haki hutazama chini kutoka mbinguni.

    12 Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema,

    nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.

    13 Haki itatangulia mbele yake

    na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.

  30. 13 Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno

    ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao,

    huburudisha roho za bwana zake.

  31. 10 Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. 11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

    12 Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu. 13 Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote. 14 Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu. 15 Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

  32. 3 “ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu, 4 nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.

  33. 4 Mvivu halimi kwa majira;

    kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama

    lakini hapati chochote.

  34. 11 Kateni tamaa, enyi wakulima,

    lieni, enyi mlimao mizabibu;

    huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,

    kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.

  35. 7 Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. 8 Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.

  36. 10 “Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, 11 lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni.

  37. 11 Mwaka wa hamsini utakuwa yubile kwenu, msipande wala msivune kile kiotacho chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa. 12 Kwa kuwa ni yubile, nayo itakuwa takatifu kwenu; mtakula tu kile kilichotoka moja kwa moja mashambani.

  38. 5 Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka

    na kuvuna nafaka kwa mikono yake,

    kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke

    katika Bonde la Warefai.

  39. 18 Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

  40. 6 Kwa miaka miwili sasa imekuwepo njaa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwepo kulima wala kuvuna.

  41. 5 Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

    mataifa yote na wakusifu.

    6 Ndipo nchi itatoa mazao yake,

    naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

    7 Mungu atatubariki

    na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

  42. 16 Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli,

    pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna.

    Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu

    kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe,

    kila mmoja na akimbilie

    kwenye nchi yake mwenyewe.

  43. 9 Kwa maana imeandikwa katika Sheria ya Mose: “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka.” Je, Mungu hapa anahusika na ngʼombe? 10 Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Hakika yameandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu mtu anapolima na mpuraji akapura nafaka, wote wanapaswa kufanya hivyo wakiwa na tumaini la kushiriki mavuno. 11 Je, ikiwa sisi tulipanda mbegu ya kiroho miongoni mwenu, itakuwa ni jambo kubwa iwapo tutavuna vitu vya mwili kutoka kwenu?

  44. 12 “Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa Bwana kama malimbuko katika mavuno yao. 13 Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamletea Bwana yatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani kwako ambaye ni safi kwa taratibu za Ibada anaweza kula.

  45. 1 Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia.

  46. 13 Wakati huu watu wa Beth-Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao huko bondeni, walipoinua macho yao na kuona lile Sanduku, wakafurahi kuliona.

  47. 17 Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,

    wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;

    wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe,

    wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.

    Kwa upanga wataangamiza

    miji yenye maboma mliyoitumainia.

  48. 13 Watapanda ngano lakini watavuna miiba;

    watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote.

    Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako

    kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”

  49. 11 Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.

  50. 4 Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,

    bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.

  51. 3 Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana,

    kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake;

    wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia,

    nayo maafa yaliwakumba,’ ”

    asema Bwana.

  52. 13 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimekusudia kuja kwenu (ingawa mpaka sasa nimezuiliwa), ili nipate kuvuna mavuno miongoni mwenu kama nilivyovuna miongoni mwa wengine ambao ni watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.

  53. 5 Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.

    6 Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. 7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.

  54. 4 Angalieni! Ule ujira wa vibarua waliolima mashamba yenu mliouzuia kwa hila unapiga kelele dhidi yenu na vilio vya wavunaji vimefika masikioni mwa Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  55. 5 Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 6 Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.”

    8 Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia.

  56. 14 Wakati wa chakula, Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya siki.”

    Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza.

  57. 6 Ewe mvivu, mwendee mchwa;

    zitafakari njia zake ukapate hekima!

    7 Kwa maana yeye hana msimamizi,

    wala mwangalizi, au mtawala,

    8 lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi

    na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

    9 Ewe mvivu, utalala hata lini?

    Utaamka lini kutoka usingizi wako?

    10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

    bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

    11 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

    na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

  58. 20 Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,

    atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.

  59. 13 Ndivyo itakavyokuwa duniani

    na miongoni mwa mataifa,

    kama vile wakati mzeituni upigwavyo,

    au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa.

  60. 4 Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

    uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,

    litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:

    mara mtu aionapo, huichuma na kuila.

  61. 10 Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,

    ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,

    mavuno ya zabibu yatakoma

    na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

  62. 13 “ ‘Nitayaondoa mavuno yao,

    asema Bwana.

    Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu.

    Hapatakuwepo na tini kwenye mtini,

    majani yake yatanyauka.

    Kile nilichowapa

    watanyangʼanywa.’ ”

  63. 4 Kilichosazwa na kundi la tunutu

    nzige wakubwa wamekula,

    kilichosazwa na nzige wakubwa

    parare wamekula,

    kilichosazwa na parare

    madumadu wamekula.

  64. 23 “ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa. 24 Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa Bwana. 25 Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezewa. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

  65. 9 Mheshimu Bwana kwa mali zako na

    kwa malimbuko ya mazao yako yote;

    10 ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika,

    viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.

  66. 4 Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu,

    kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.

  67. 19 Sikia kilio cha watu wangu

    kutoka nchi ya mbali:

    “Je, Bwana hayuko Sayuni?

    Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”

    “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,

    kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

    20 “Mavuno yamepita,

    kiangazi kimekwisha,

    nasi hatujaokolewa.”

  68. 15 Mtapanda lakini hamtavuna;

    mtakamua zeituni lakini

    hamtatumia mafuta yake.

    Mtakamua zabibu

    lakini hamtakunywa hiyo divai.

  69. 6 Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.”