32 Bible Verses About Winter

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Winter
  1. 5 Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu;

    yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.

    6 Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’

    nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’

    7 Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake,

    yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.

    8 Wanyama hujificha;

    hubakia kwenye mapango yao.

    9 Dhoruba hutoka katika chumba chake,

    baridi hutoka katika upepo uendao kasi.

    10 Pumzi ya Mungu hutoa barafu,

    eneo kubwa la maji huganda.

    11 Huyasheheneza mawingu kwa maji,

    naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.

    12 Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake,

    juu ya uso wa dunia yote,

    kufanya lolote ayaamuruyo.

    13 Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu,

    au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.

  2. 16 jiosheni na mkajitakase.

    Yaondoeni matendo yenu maovu

    mbele zangu!

    Acheni kutenda mabaya,

    17 jifunzeni kutenda mema!

    Tafuteni haki,

    watieni moyo walioonewa.

    Teteeni shauri la yatima,

    wateteeni wajane.

    18 “Njooni basi tuhojiane,”

    asema Bwana.

    “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu,

    zitakuwa nyeupe kama theluji;

    ingawa ni nyekundu sana kama damu,

    zitakuwa nyeupe kama sufu.

  3. 12 Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu,

    msifu Mungu wako, ee Sayuni,

    13 kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako

    na huwabariki watu wako walio ndani yako.

    14 Huwapa amani mipakani mwenu

    na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.

    15 Hutuma amri yake duniani,

    neno lake hukimbia kasi.

    16 Anatandaza theluji kama sufu

    na kutawanya umande kama majivu.

    17 Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe.

    Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?

    18 Hutuma neno lake na kuviyeyusha,

    huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.

    19 Amemfunulia Yakobo neno lake,

    sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

    20 Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote,

    hawazijui sheria zake.

    Msifuni Bwana.

  4. 10 Kama vile mvua na theluji

    ishukavyo kutoka mbinguni,

    nayo hairudi tena huko

    bila kunywesha dunia

    na kuichipusha na kuistawisha,

    hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi

    na mkate kwa mlaji,

    11 ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu:

    Halitanirudia tupu,

    bali litatimiliza lile nililokusudia

    na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.

    12 Mtatoka nje kwa furaha

    na kuongozwa kwa amani;

    milima na vilima

    vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu,

    nayo miti yote ya shambani

    itapiga makofi.

  5. 6 Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni,

    ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.

    7 Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi,

    unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

  6. 20 Kisha Noa akamjengea Bwana madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 21 Bwana akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya.

    22 “Kwa muda dunia idumupo,

    wakati wa kupanda na wa kuvuna,

    wakati wa baridi na wa joto,

    wakati wa kiangazi na wa masika,

    usiku na mchana

    kamwe havitakoma.”

  7. 20 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

  8. 9 “Nilipoendelea kutazama,

    “viti vya enzi vikawekwa,

    naye Mzee wa Siku akaketi.

    Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji;

    nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu.

    Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto,

    nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.

  9. 11 Neno lisemwalo kwa wakati ufaao

    ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu

    yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha.

    12 Kama vile kipuli cha dhahabu

    au pambo la dhahabu safi,

    ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima

    kwa sikio lisikilizalo.

    13 Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno

    ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao,

    huburudisha roho za bwana zake.

  10. 20 Huwanyooshea maskini mikono yake

    na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

    21 Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake,

    kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

  11. 22 “Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji,

    au kuona ghala za mvua ya mawe,

    23 ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu,

    na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?

    24 Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa,

    au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia?

    25 Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi

    na njia ya umeme wa radi,

    26 ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu,

    jangwa lisilo na yeyote ndani yake,

    27 ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa,

    na majani yaanze kumea ndani yake?

  12. 16 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,

    uliziweka jua na mwezi.

    17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,

    ulifanya kiangazi na masika.

  13. 11 Tazama! Wakati wa masika umepita,

    mvua imekwisha na ikapita.

    12 Maua yanatokea juu ya nchi;

    majira ya kuimba yamewadia,

    sauti za njiwa zinasikika

    katika nchi yetu.

  14. 22 Ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto.

  15. 16 Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kupitia kwangu lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen.

    19 Wasalimu Prisila na Akila, na wote wa nyumbani kwa Onesiforo. 20 Erasto alibaki Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko Mileto akiwa mgonjwa. 21 Jitahidi ufike huku kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu, vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.

    22 Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.

  16. 1 Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ya kwanza ya juma, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kulitazama kaburi.

    2 Ghafula, pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaenda penye kaburi, akalivingirisha lile jiwe na kulikalia. 3 Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4 Wale walinzi wa kaburi walimwogopa sana, wakatetemeka hata wakawa kama wafu.

    5 Yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope, kwa maana ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6 Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.

  17. 14 Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutoweka

    kwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote?

    Je, maji yake baridi yatokayo katika vyanzo vilivyo mbali

    yaliwahi kukoma kutiririka wakati wowote?

  18. 7 Mtukuzeni Bwana kutoka duniani,

    ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,

    8 umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu,

    pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,

  19. 15 Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,

    pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;

    nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu

    na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”

    asema Bwana.

  20. 12 Kwa kuwa ile bandari ilikuwa haifai kukaa wakati wa majira ya baridi, wengi wakashauri kwamba tuendelee na safari wakitarajia kufika Foinike na kukaa huko kwa majira ya baridi. Hii ilikuwa bandari iliyoko katika kisiwa cha Krete ikikabili upande wa kusini-magharibi na kaskazini-magharibi.

  21. 15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,

    ni kama vijito vya msimu,

    ni kama vijito ambavyo hufurika

    16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,

    ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,

  22. 20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato. 21 Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe.

  23. 2 Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. 3 Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. 4 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu.

  24. 22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

  25. 1 Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno,

    ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.

  26. 8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki, na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi wakati wa kiangazi na wakati wa masika.

  27. 4 Mvivu halimi kwa majira;

    kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama

    lakini hapati chochote.

  28. 6 Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani

    na wanyama pori,

    ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,

    nao wanyama pori wakati wote wa masika.

  29. 12 Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

  30. 18 Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi.

  31. 9 Jitahidi kuja kwangu upesi 10 kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia. 11 Ni Luka peke yake aliye hapa pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa sababu ananifaa sana katika huduma yangu. 12 Nimemtuma Tikiko huko Efeso. 13 Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi.

  32. 11 Miezi mitatu baadaye tukaanza safari kwa meli iliyokuwa imetia nanga kwenye kisiwa hicho kwa ajili ya majira ya baridi. Hii ilikuwa meli ya Iskanderia yenye alama ya miungu pacha waitwao Kasta na Poluksi.