25 Bible Verses About Fall

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Fall
  1. 12 Watu hawa ni dosari katika karamu zenu za upendo, wakila pamoja nanyi bila hofu, wakijilisha pasipo hofu. Wao ni mawingu yasiyokuwa na maji, yakichukuliwa na upepo, miti isiyo na matunda wakati wa mapukutiko, ambayo hunyauka, iliyokufa mara mbili na kungʼolewa kabisa. 13 Wao ni mawimbi makali ya bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba waliowekewa milele.

  2. 24 Wao hawaambiani wenyewe,

    ‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu,

    anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,

    anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’

    25 Matendo yenu mabaya yamezuia haya yote,

    dhambi zenu zimewazuia msipate mema.

  3. 1 Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo,

    nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:

    2 wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,

    wakati wa kupanda na wakati wa kungʼoa yaliyopandwa,

  4. 5 Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,

    na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.

    6 Wanapopita katika Bonde la Baka,

    hulifanya mahali pa chemchemi,

    pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.

  5. 13 Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda Bwana Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, 14 ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta. 15 Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

  6. 22 “Kwa muda dunia idumupo,

    wakati wa kupanda na wa kuvuna,

    wakati wa baridi na wa joto,

    wakati wa kiangazi na wa masika,

    usiku na mchana

    kamwe havitakoma.”

  7. 1 “ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta.

  8. 19 Mwezi hugawanya majira,

    na jua hutambua wakati wake wa kutua.

  9. 4 Mvivu halimi kwa majira;

    kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama

    lakini hapati chochote.

  10. 27 “Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto.

  11. 34 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya Bwana ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba.

  12. 7 “ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi.

  13. 12 “ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwa Bwana kwa siku saba.

  14. 7 Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. 8 Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.

  15. 23 Furahini, enyi watu wa Sayuni,

    shangilieni katika Bwana Mungu wenu,

    kwa kuwa amewapa mvua za vuli

    kwa kipimo cha haki.

    Anawapelekea mvua nyingi,

    mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.

  16. 37 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. 38 Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.”

  17. 9 Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.

  18. 14 Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka,

  19. 26 Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka.

  20. 21 “Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike.

  21. 37 Msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa tano. 38 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Solomoni. Alilijenga kwa miaka saba.

  22. 9 Dhoruba hutoka katika chumba chake,

    baridi hutoka katika upepo uendao kasi.

  23. 17 Lakini hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake: Ameonyesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.”

  24. 6 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.

    Msifuni Bwana!

  25. 5 Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi

    ni mwana mwenye hekima,

    lakini yeye alalaye wakati wa mavuno

    ni mwana mwenye kuaibisha.