79 Bible Verses About Birthdays

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Birthdays
  1. 1 Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. 2 (Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Shamu). 3 Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.

    4 Hivyo Yosefu akapanda kutoka mji wa Nazareti ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 5 Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Maria, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. 6 Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Maria wa kujifungua ukawa umetimia, 7 naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ngʼombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

    8 Katika eneo lile walikuwako wachungaji waliokuwa wakikaa mashambani, wakilinda makundi yao ya kondoo usiku. 9 Ghafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawangʼaria kotekote, wakaingiwa na hofu. 10 Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 11 Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. 12 Hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ngʼombe.”

    13 Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema,

    14 “Atukuzwe Mungu juu mbinguni,

    na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

    15 Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Bwana ametuambia habari zake.”

    16 Hivyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga akiwa amelala katika hori la kulia ngʼombe. 17 Walipomwona yule mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa kuhusu huyo mtoto. 18 Nao wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wale wachungaji wa kondoo. 19 Lakini Maria akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. 20 Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.

  2. 20 Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake: 21 Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mikononi mwa Farao tena, 22 lakini akamwangika yule mwokaji mkuu, sawasawa na jinsi Yosefu alivyowaambia katika tafsiri yake.

    23 Pamoja na hayo, mnyweshaji mkuu hakumkumbuka Yosefu, bali alimsahau.

  3. 11 Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako,

    wakulinde katika njia zako zote.

    12 Mikononi mwao watakuinua,

    ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.

    13 Utawakanyaga simba na nyoka wakali,

    simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

    14 Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa;

    nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.

    15 Ataniita, nami nitamjibu;

    nitakuwa pamoja naye katika taabu,

    nitamwokoa na kumheshimu.

    16 Kwa siku nyingi nitamshibisha

    na kumwonyesha wokovu wangu.”

  4. 18 Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.

    20 Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

    22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 23 “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”

    24 Yosefu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Maria kuwa mke wake. 25 Lakini hawakukutana kimwili mpaka Maria alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Yesu.

  5. 6 Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode, 7 kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba. 8 Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” 9 Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. 10 Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. 11 Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

  6. 17 Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka. 18 Kwa mapenzi yake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mazao ya kwanza katika viumbe vyake vyote.

  7. 13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

    uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

    14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

    kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

    kazi zako ni za ajabu,

    ninajua hayo kikamilifu.

    15 Umbile langu halikufichika kwako,

    nilipoumbwa mahali pa siri.

    Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

    16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

    Siku zangu zote ulizonipangia

    ziliandikwa katika kitabu chako

    kabla haijakuwepo hata moja.

  8. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, 9 si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu. 10 Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.

  9. 3 Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili.”

    4 Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!”

    5 Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho. 6 Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ 8 Upepo huvuma popote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”

  10. 11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. 12 Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza.

  11. 4 Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao. 5 Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu.

  12. 12 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

    ili tujipatie moyo wa hekima.

  13. 21 Hata hivyo najikumbusha neno hili

    na kwa hiyo ninalo tumaini.

    22 Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,

    kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

    23 Ni mpya kila asubuhi,

    uaminifu wako ni mkuu.

  14. 10 Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia,

    nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.

    11 Ninakuongoza katika njia ya hekima

    na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka.

    12 Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa;

    ukimbiapo, hutajikwaa.

    13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;

    mshike, maana yeye ni uzima wako.

  15. 6 Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

    tumepewa mtoto mwanaume,

    nao utawala utakuwa mabegani mwake.

    Naye ataitwa

    Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,

    Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

    7 Kuongezeka kwa utawala wake na amani

    hakutakuwa na mwisho.

    Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi

    na juu ya ufalme wake,

    akiuthibitisha na kuutegemeza

    kwa haki na kwa adili,

    tangu wakati huo na hata milele.

    Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote

    utatimiza haya.

  16. 6 Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe,

    ulinitoa tumboni mwa mama yangu.

    Nitakusifu wewe daima.

    7 Nimekuwa kama kioja kwa wengi,

    lakini wewe ni kimbilio langu imara.

    8 Kinywa changu kimejazwa sifa zako,

    nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.

  17. 11 Kwa maana kwa msaada wangu

    siku zako zitakuwa nyingi,

    na miaka itaongezwa katika maisha yako.

  18. 15 Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

  19. 4 Na akujalie haja ya moyo wako,

    na aifanikishe mipango yako yote.

  20. 4 Jifurahishe katika Bwana

    naye atakupa haja za moyo wako.

    5 Mkabidhi Bwana njia yako,

    mtumaini yeye, naye atatenda hili:

    6 Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko,

    na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.

  21. 24 Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,

    tushangilie na kufurahi ndani yake.

    25 Ee Bwana, tuokoe,

    Ee Bwana, utujalie mafanikio.

  22. 5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

    kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

    nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

  23. 11 Umenijulisha njia ya uzima;

    utanijaza na furaha mbele zako,

    pamoja na furaha za milele

    katika mkono wako wa kuume.

  24. 8 Hata kama mtu ataishi miaka mingi kiasi gani,

    na aifurahie yote.

    Lakini na akumbuke siku za giza,

    kwa maana zitakuwa nyingi.

    Kila kitu kitakachokuja ni ubatili.

    9 Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana,

    moyo wako na ukupe furaha

    katika siku za ujana wako.

    Fuata njia za moyo wako

    na chochote macho yako yaonayo,

    lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote

    Mungu atakuleta hukumuni.

    10 Kwa hiyo basi, ondoa wasiwasi moyoni mwako

    na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako,

    kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.

  25. 11 Umeuvika mwaka taji ya baraka,

    magari yako yanafurika kwa wingi.

  26. 1 Baada ya Yesu kuzaliwa katika mji wa Bethlehemu huko Uyahudi, wakati wa utawala wa Mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu 2 wakiuliza, “Yuko wapi huyo aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tumekuja kumwabudu.”

  27. 21 Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni.

  28. 4 “Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu

    na hesabu ya siku zangu;

    nijalie kujua jinsi maisha yangu

    yanavyopita upesi.

    5 Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;

    muda wangu wa kuishi ni kama

    hauna thamani kwako.

    Maisha ya kila mwanadamu

    ni kama pumzi.

  29. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

    wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

    6 katika njia zako zote mkiri yeye,

    naye atayanyoosha mapito yako.

  30. 1 Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi,

    nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa.

  31. 12 Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao.

  32. 4 Jambo moja ninamwomba Bwana,

    hili ndilo ninalolitafuta:

    niweze kukaa nyumbani mwa Bwana

    siku zote za maisha yangu,

    niutazame uzuri wa Bwana

    na kumtafuta hekaluni mwake.

    5 Kwa kuwa siku ya shida,

    atanihifadhi salama katika maskani yake,

    atanificha uvulini mwa hema yake

    na kuniweka juu kwenye mwamba.

    6 Kisha kichwa changu kitainuliwa

    juu ya adui zangu wanaonizunguka.

    Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;

    nitamwimbia Bwana na kumsifu.

    7 Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana,

    unihurumie na unijibu.

  33. 31 bali wale wamtumainio Bwana

    atafanya upya nguvu zao.

    Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

    watapiga mbio wala hawatachoka,

    watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

  34. 12 Kwa maana ni nani anayejua lililo jema kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, katika siku chache na za ubatili anazopita kama kivuli? Ni nani awezaye kumwambia yatakayotokea chini ya jua baada ya yeye kuondoka?

  35. 5 Mtu mmoja anaitukuza siku fulani kuwa ni bora kuliko nyingine, na mwingine anaona kuwa siku zote ni sawa. Basi kila mmoja awe na hakika na yale anayoamini. 6 Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye alaye nyama hula kwa Bwana, kwa maana humshukuru Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Bwana na humshukuru Mungu.

  36. 15 Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, 16 “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” 17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. 18 Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

    19 Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

    20 Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi.

  37. 9 Hata hivyo ulinitoa tumboni,

    ukanifanya nikutegemee,

    hata nilipokuwa ninanyonya

    matiti ya mama yangu.

    10 Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,

    toka tumboni mwa mama yangu

    umekuwa Mungu wangu.

  38. 9 Baada ya kumsikia mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama mahali pale alipokuwa mtoto. 10 Walipoiona ile nyota wakajawa na furaha kubwa mno. 11 Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Maria mama yake, wakamsujudu na kumwabudu yule mtoto Yesu. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane.

  39. 13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

  40. Sehemu Ya Pili: Mazungumzo Ya Ayubu Na Rafiki Zake Watatu

    Hotuba Ya Kwanza Ya Ayubu

    1 Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

    2 Kisha akasema:

    3 “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali,

    nao usiku ule iliposemekana,

    ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’

    4 Siku ile na iwe giza;

    Mungu juu na asiiangalie;

    nayo nuru isiiangazie.

  41. 9 Mfanyakazi anapata faida gani kutokana na taabu yake? 10 Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu. 11 Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho. 12 Ninajua kwamba hakuna kitu bora kwa wanadamu kuliko kuwa na furaha na kutenda mema wakati wanapoishi. 13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote. 14 Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.

  42. 7 “Kabla hajasikia utungu, alizaa;

    kabla hajapata maumivu,

    alizaa mtoto mwanaume.

    8 Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?

    Ni nani amepata kuona mambo kama haya?

    Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja,

    au taifa laweza kutokea mara?

    Mara Sayuni alipoona utungu,

    alizaa watoto wake.

    9 Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa

    na nisizalishe?” asema Bwana.

    “Je, nifunge tumbo la uzazi

    wakati mimi ndiye nizalishaye?”

    asema Mungu wako.

    10 “Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,

    ninyi nyote mnaompenda,

    shangilieni kwa nguvu pamoja naye,

    ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.

    11 Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka

    katika faraja ya matiti yake;

    mtakunywa sana,

    na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

    12 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

    “Nitamwongezea amani kama mto,

    nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;

    utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake

    na kubembelezwa magotini pake.

  43. 14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

    Nayo isibarikiwe ile siku

    mama yangu aliyonizaa!

    15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

    yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

    “Mtoto amezaliwa kwako,

    tena mtoto wa kiume!”

    16 Mtu huyo na awe kama miji ile

    ambayo Bwana Mungu

    aliiangamiza bila huruma.

    Yeye na asikie maombolezo asubuhi

    na kilio cha vita adhuhuri.

    17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

    hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

    nalo tumbo lake la uzazi

    lingebaki kuwa kubwa daima.

    18 Kwa nini basi nilitoka tumboni

    ili kuona taabu na huzuni,

    na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

  44. 1 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.

    3 Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa.

  45. 31 Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

  46. 4 Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe, ambaye alizaliwa na mwanamke, akazaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, ili tupate kupokea zile haki kamili za kufanywa watoto wa Mungu.

  47. 13 Basi sikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.” 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, “Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.”

  48. 15 Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo. 16 Ninakuamuru leo kwamba umpende Bwana Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.

    17 Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu, 18 nakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

    19 Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, 20 na ili upate kumpenda Bwana Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaki na Yakobo.

  49. 9 Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako.”

  50. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

  51. 9 Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.

  52. 2 “Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Bwana,

    hakuna mwingine zaidi yako;

    hakuna Mwamba kama Mungu wetu.

    3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo

    wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi,

    kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye,

    na kwa yeye matendo hupimwa.

    4 “Pinde za mashujaa zimevunjika,

    lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.

    5 Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe

    ili kupata chakula,

    lakini wale waliokuwa na njaa

    hawana njaa tena.

    Mwanamke yule aliyekuwa tasa

    amezaa watoto saba,

    lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi

    amedhoofika.

    6 “Bwana huua na huleta uhai,

    hushusha chini mpaka kaburini na hufufua.

    7 Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha,

    hushusha na hukweza.

  53. 1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke

    siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.

  54. 25 “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege?

  55. 1 Kwa sababu hii, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, basi na tuweke kando kila kitu kinachotuzuia na ile dhambi inayotuzinga kwa urahisi, nasi tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa kwa ajili yetu. 2 Basi na tumtazame sana Yesu mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

  56. KITABU CHA KWANZA

    1 Heri mtu yule ambaye

    haendi katika shauri la watu waovu,

    wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,

    au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

    2 Bali huifurahia sheria ya Bwana,

    naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

    3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa

    kando ya vijito vya maji,

    ambao huzaa matunda kwa majira yake

    na majani yake hayanyauki.

    Lolote afanyalo hufanikiwa.

  57. 14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

    17 “Kwa hiyo tokeni miongoni mwao,

    mkatengwe nao,

    asema Bwana.

    Msiguse kitu chochote kilicho najisi,

    nami nitawakaribisha.”

    18 “Mimi nitakuwa Baba kwenu,

    nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu,

    asema Bwana Mwenyezi.”

  58. 13 Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

  59. 16 Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, 17 ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.

  60. 3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema zake kuu ametuzaa sisi mara ya pili katika tumaini lenye uzima kupitia kwa kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu, 4 ili tuupate urithi usioharibika, usio na uchafu, ule usionyauka: uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,

  61. 7 Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

  62. 7 Basi Sauli alikuwa amekuwa na suria, jina lake Rispa binti wa Aiya. Naye Ish-Boshethi akamwambia Abneri, “Kwa nini umekutana kimwili na suria wa baba yangu?”

  63. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

    1 Ee Bwana, umenichunguza

    na kunijua.

    2 Unajua ninapoketi na ninapoinuka;

    unatambua mawazo yangu tokea mbali.

    3 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;

    unaelewa njia zangu zote.

    4 Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,

    wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.

    5 Umenizunguka nyuma na mbele;

    umeweka mkono wako juu yangu.

  64. 24 Hakuna kitu bora anachoweza kufanya mtu zaidi ya kula na kunywa na kuridhika katika kazi yake. Hili nalo pia, ninaona, latokana na mkono wa Mungu,

  65. 3 Naye akasema: “Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni.

  66. 3 Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. 4 Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, 5 kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. 6 Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Kristo Yesu.

  67. 7 Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

  68. 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. 2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

    3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.

  69. 8 “Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya.

    Je, sasa utageuka na kuniangamiza?

    9 Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi.

    Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?

    10 Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa,

    na kunigandisha kama jibini,

    11 ukanivika ngozi na nyama,

    na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?

    12 Umenipa uhai na kunitendea wema,

    katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.

  70. 5 Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi,

    mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.

  71. 5 Bwana ni mwenye neema na haki,

    Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

  72. 15 Kifo cha watakatifu kina thamani

    machoni pa Bwana.

  73. 10 Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

    usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

    Nitakutia nguvu na kukusaidia;

    nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

  74. 4 Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

    Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

    Nimewahuluku, nami nitawabeba,

    nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.

  75. 15 Ndipo Yesu akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.”

  76. 22 Kwa maana twajua ya kuwa hata sasa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa maumivu kama utungu wa mwanamke wakati wa kuzaa. 23 Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu.

  77. 3 Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe.

  78. 29 Kama mkijua kuwa yeye ni mwenye haki, mwajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.

  79. 3 Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani, kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito. 4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.