48 Bible Verses About Greed

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Greed
  1. 6 Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa. 7 Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu chochote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu. 8 Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo. 9 Lakini wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa haraka huanguka kwenye majaribu, na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi. 10 Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.

  2. 15 Ndipo Yesu akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.”

  3. 3 Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. 4 Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu. 5 Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Msherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu.

  4. 27 Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu,

    bali yeye achukiaye rushwa ataishi.

  5. 1 Basi sikilizeni, ninyi matajiri, lieni na kuomboleza kwa ajili ya hali mbaya sana inayowajia. 2 Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho. 4 Angalieni! Ule ujira wa vibarua waliolima mashamba yenu mliouzuia kwa hila unapiga kelele dhidi yenu na vilio vya wavunaji vimefika masikioni mwa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 5 Mmeishi duniani kwa anasa na kwa starehe, mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. 6 Mmewahukumu na kuwaua watu wenye haki, waliokuwa hawapingani nanyi.

  6. 10 Yeyote apendaye fedha kamwe

    hatosheki na fedha;

    yeyote apendaye utajiri kamwe

    hatosheki na kipato chake.

    Hili nalo pia ni ubatili.

    11 Mali ikiongezeka, ndivyo walaji

    wanavyoongezeka.

    Hii nayo inamfaidia nini mwenye mali

    isipokuwa ni kushibisha macho yake?

    12 Usingizi wa kibarua ni mtamu,

    awe amekula kidogo au kingi,

    lakini wingi wa mali

    humnyima tajiri usingizi.

  7. 9 Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, 10 wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu. 11 Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.

  8. 25 Mtu mwenye tamaa huchochea fitina,

    bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.

    26 Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu,

    bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama.

    27 Yeye ampaye maskini

    hatapungukiwa na kitu chochote,

    bali yeye awafumbiaye maskini macho

    hupata laana nyingi.

    28 Wakati waovu watawalapo,

    watu huenda mafichoni,

    bali waovu wanapoangamia,

    wenye haki hufanikiwa.

  9. 24 “Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.

  10. 5 Kwa hiyo, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambayo ndiyo ibada ya sanamu.

  11. 19 Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;

    huuondoa uhai wa wale wenye mali.

  12. 3 Usitamani vyakula vyake vitamu

    kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

    4 Usijitaabishe ili kuupata utajiri,

    uwe na hekima kuonyesha kujizuia.

    5 Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka,

    huwa kama umepata mabawa ghafula,

    ukaruka na kutoweka angani kama tai.

  13. 5 Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,

    “Kamwe sitakuacha,

    wala sitakupungukia.”

  14. 15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. 16 Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 17 Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

  15. 20 Mtu mwaminifu atabarikiwa sana,

    bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka

    hataacha kuadhibiwa.

    21 Kuonyesha upendeleo si vizuri,

    hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate.

    22 Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri,

    naye hana habari kuwa umaskini unamngojea.

  16. 3 Nao katika tamaa zao mbaya, walimu hawa watajipatia faida kwenu kwa hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, wala uangamivu wao haujalala usingizi.

  17. 3 Hujivunia tamaa za moyo wake;

    humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

  18. 19 “Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba.

  19. 11 Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.

  20. 16 yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen.

    17 Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie. 18 Waagize watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio tayari kushiriki mali zao na wengine. 19 Kwa njia hii watajiwekea hazina kama msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima ambao ni wa kweli.

  21. 1 Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa: 2 lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika. 3 Msijifanye mabwana juu ya wale walio chini ya uangalizi wenu, bali kuweni vielelezo kwa hilo kundi.

  22. 5 hakika mvinyo humsaliti;

    ni mwenye kiburi na hana amani.

    Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu

    na kama kifo kamwe hatosheki;

    anajikusanyia mataifa yote

    na kuchukua watu wote mateka.

    6 “Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema,

    “ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa

    na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu!

    Ataendelea hivi kwa muda gani?’

  23. 5 Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu.

  24. 2 Basi, imempasa mwangalizi awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha, 3 asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha.

  25. 10 Usitumainie vya udhalimu

    wala usijivune kwa vitu vya wizi;

    ingawa utajiri wako utaongezeka,

    usiviwekee moyo wako.

  26. 13 “Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

    wote wana tamaa ya kupata faida zaidi;

    manabii na makuhani wanafanana,

    wote wanafanya udanganyifu.

  27. 20 Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21 Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, 22 tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”

  28. 28 Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,

    bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.

  29. 25 Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake,

    kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.

    26 Mchana kutwa hutamani zaidi,

    lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.

  30. 10 Walinzi wa Israeli ni vipofu,

    wote wamepungukiwa na maarifa;

    wote ni mbwa walio bubu,

    hawawezi kubweka;

    hulala na kuota ndoto,

    hupenda kulala.

    11 Ni mbwa wenye tamaa kubwa,

    kamwe hawatosheki.

    Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu;

    wote wamegeukia njia yao wenyewe,

    kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.

  31. 10 Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,

    na mashamba yao kwa wamiliki wengine.

    Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

    wote wana tamaa ya kupata zaidi;

    manabii na makuhani wanafanana,

    wote wanafanya udanganyifu.

  32. 36 Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake?

  33. 11 Fedha isiyo ya halali hupungua,

    bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.

    12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,

    bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.

  34. 21 Urithi upatikanao haraka mwanzoni,

    hautabarikiwa mwishoni.

  35. 1 Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi,

    kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.

  36. 25 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na kutokuwa na kiasi.

  37. 39 Ndipo Bwana akamwambia, “Sasa, enyi Mafarisayo, mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na uovu.

  38. 8 Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali.

  39. 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.”

  40. 35 Niongoze kwenye njia ya amri zako,

    kwa kuwa huko napata furaha.

    36 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako,

    na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.

    37 Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa,

    uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

  41. 8 Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno

    hukusanya kwa ajili ya mwingine,

    ambaye atawahurumia maskini.

  42. 4 Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti,

    bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.

  43. 31 Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali.

  44. 1 Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu, walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao. 2 Hakuna jambo lolote lililositirika ambalo halitafunuliwa, au lililofichwa ambalo halitajulikana. 3 Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonongʼona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.

  45. 4 Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema, 5 “Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300 na fedha hizo wakapewa maskini?” 6 Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

  46. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

  47. 11 Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote. 12 Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa. 13 Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

  48. 7 Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali.