90 Bible Verses About Wisdom

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Wisdom
  1. 18 Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Kwa maana imeandikwa:

    “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima,

    na kubatilisha akili ya wenye akili.”

    20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? 21 Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. 22 Wayahudi wanadai ishara za miujiza na Wayunani wanatafuta hekima. 23 Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi. 24 Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, Wayahudi na pia Wayunani, Kristo ndiye nguvu ya Mungu na pia hekima ya Mungu. 25 Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.

    26 Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. 27 Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu.

  2. 2 Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 3 kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4 Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote. 5 Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa. 6 Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku. 7 Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana. 8 Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.

  3. 13 Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima. 14 Lakini ikiwa mna wivu na ni wenye chuki na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu kwa ajili ya hayo wala msiikatae kweli. 15 Hekima ya namna hiyo haishuki kutoka mbinguni, bali ni ya kidunia, isiyo ya kiroho, na ya kishetani. 16 Kwa maana panapokuwa na wivu na ubinafsi, ndipo penye machafuko na uovu wa kila namna.

    17 Lakini hekima itokayo mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki. 18 Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

  4. 1 Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu

    na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,

    2 kutega sikio lako kwenye hekima

    na kuweka moyo wako katika ufahamu,

    3 na kama ukiita busara

    na kuita kwa sauti ufahamu,

    4 na kama utaitafuta kama fedha

    na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,

    5 ndipo utakapoelewa kumcha Bwana

    na kupata maarifa ya Mungu.

    6 Kwa maana Bwana hutoa hekima,

    na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

    7 Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,

    yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

    8 kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki

    na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.

    9 Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki

    na sawa: yaani kila njia nzuri.

    10 Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako,

    nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.

  5. 7 “Sasa, Ee Bwana Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme badala ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu, wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu. 8 Mtumishi wako yuko hapa miongoni mwa watu uliowachagua: taifa kubwa, watu wengi wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao. 9 Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu ili kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana, ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi hivi?”

    10 Bwana akapendezwa kwamba Solomoni ameliomba jambo hili. 11 Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki, 12 nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako. 13 Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima, ili kwamba maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme. 14 Nawe kama ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.”

  6. 2 Kwa kupata hekima na nidhamu;

    kwa kufahamu maneno ya busara;

    3 kwa kujipatia nidhamu na busara,

    kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;

    4 huwapa busara wajinga,

    maarifa na akili kwa vijana;

    5 wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,

    wenye kupambanua na wapate mwongozo;

    6 kwa kufahamu mithali na mifano,

    misemo na vitendawili vya wenye hekima.

    7 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,

    lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

  7. 1 Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu. 2 Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote wakati nikiwa nanyi isipokuwa Yesu Kristo aliyesulubiwa. 3 Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana. 4 Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho 5 ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.

    6 Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. 7 Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. 8 Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu. 9 Lakini ni kama ilivyoandikwa:

    “Hakuna jicho limepata kuona,

    wala sikio limepata kusikia,

    wala hayakuingia moyoni wowote,

    yale Mungu amewaandalia

    wale wampendao”:

    10 Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa Roho wake.

    Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu. 11 Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 12 Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure. 13 Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa maneno ya kiroho. 14 Mtu ambaye hana Roho hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni. 15 Mtu wa kiroho hubainisha mambo yote, lakini yeye mwenyewe habainishwi na mtu yeyote.

  8. 10 Chagua mafundisho yangu badala ya fedha,

    maarifa badala ya dhahabu safi,

    11 kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani

    na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.

    12 “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;

    ninamiliki maarifa na busara.

    13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;

    ninachukia kiburi na majivuno,

    tabia mbaya na mazungumzo potovu.

    14 Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu;

    nina ufahamu na nina nguvu.

    15 Kwa msaada wangu wafalme hutawala

    na watawala hutunga sheria zilizo za haki,

    16 kwa msaada wangu wakuu hutawala,

    na wenye vyeo wote watawalao dunia.

    17 Nawapenda wale wanipendao,

    na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

    18 Utajiri na heshima viko kwangu,

    utajiri udumuo na mafanikio.

    19 Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi;

    kile nitoacho hupita fedha iliyo bora.

    20 Natembea katika njia ya unyofu

    katika mapito ya haki,

    21 nawapa utajiri wale wanipendao

    na kuzijaza hazina zao.

    22 “Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,

    kabla ya matendo yake ya zamani;

    23 niliteuliwa tangu milele,

    tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.

  9. 8 Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia;

    mkemee mwenye hekima naye atakupenda.

    9 Mfundishe mtu mwenye hekima

    naye atakuwa na hekima zaidi;

    mfundishe mtu mwadilifu

    naye atazidi kufundishika.

    10 “Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

    na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.

    11 Kwa maana kwa msaada wangu

    siku zako zitakuwa nyingi,

    na miaka itaongezwa katika maisha yako.

    12 Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo;

    kama wewe ni mtu wa mzaha,

    wewe mwenyewe ndiwe utateseka.”

  10. 13 Heri mtu yule aonaye hekima,

    mtu yule apataye ufahamu,

    14 kwa maana hekima ana faida kuliko fedha

    na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.

    15 Hekima ana thamani kuliko marijani;

    hakuna chochote unachokitamani

    kinachoweza kulinganishwa naye.

    16 Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;

    katika mkono wake wa kushoto

    kuna utajiri na heshima.

    17 Njia zake zinapendeza,

    mapito yake yote ni amani.

    18 Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;

    wale wamshikao watabarikiwa.

    19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia,

    kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake;

    20 kwa maarifa yake vilindi viligawanywa,

    nayo mawingu yanadondosha umande.

    21 Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara,

    usiache vitoke machoni pako;

    22 ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako

    na pambo la neema shingoni mwako.

    23 Kisha utaenda katika njia yako salama,

    wala mguu wako hautajikwaa;

  11. 29 Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari. 30 Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri. 31 Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka. 32 Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005. 33 Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki. 34 Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.

  12. 9 Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu. 10 Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu,

  13. 20 Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,

    hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;

    21 kwenye makutano ya barabara za mji

    zenye makelele mengi hupaza sauti,

    kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:

    22 “Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?

    Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha,

    na wapumbavu kuchukia maarifa?

    23 Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,

    ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu

    na kuwafahamisha maneno yangu.

    24 Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita

    na hakuna yeyote aliyekubali

    niliponyoosha mkono wangu,

    25 kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote

    na hamkukubali karipio langu,

    26 mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,

    nitawadhihaki wakati janga litawapata:

  14. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

    wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

    6 katika njia zako zote mkiri yeye,

    naye atayanyoosha mapito yako.

    7 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;

    mche Bwana ukajiepushe na uovu.

    8 Hii itakuletea afya mwilini mwako,

    na mafuta kwenye mifupa yako.

  15. 19 Wakati wa usiku lile fumbo lilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Ndipo Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni, 20 na akasema:

    “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;

    hekima na uweza ni vyake.

    21 Yeye hubadili nyakati na majira;

    huwaweka wafalme na kuwaondoa.

    Huwapa hekima wenye hekima,

    na maarifa wenye ufahamu.

    22 Hufunua siri na mambo yaliyofichika;

    anajua yale yaliyo gizani,

    nayo nuru hukaa kwake.

    23 Ninakushukuru na kukuhimidi,

    Ee Mungu wa baba zangu:

    Umenipa hekima na uwezo,

    umenijulisha kile tulichokuomba,

    umetujulisha ndoto ya mfalme.”

  16. 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. 31 Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”

  17. 16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. 17 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. 18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu 19 na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno

  18. 1 Ndipo Bwana akamwambia Mose, 2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 4 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 5 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi.

  19. 1 Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese,

    kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.

    2 Roho wa Bwana atakaa juu yake,

    Roho wa hekima na wa ufahamu,

    Roho wa shauri na wa uweza,

    Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana

    3 naye atafurahia kumcha Bwana.

    Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,

    wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

  20. 10 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

    wote wanaozifuata amri zake wana busara.

    Sifa zake zadumu milele.

  21. 28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

    ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

    nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

  22. 1 Hekima amejenga nyumba yake;

    amechonga nguzo zake saba.

    2 Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake;

    pia ameandaa meza yake.

    3 Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita

    kutoka mahali pa juu sana pa mji.

    4 Anawaambia wale wasio na akili,

    “Wote ambao ni wajinga na waje hapa!

    5 Njooni, mle chakula changu

    na mnywe divai niliyoichanganya.

    6 Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi;

    tembeeni katika njia ya ufahamu.

  23. 6 Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,

    bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.

    7 Kaa mbali na mtu mpumbavu,

    kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.

    8 Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,

    bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.

  24. 18 Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima. 19 Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za Mungu. Kama ilivyoandikwa: “Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao,” 20 tena, “Bwana anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni ubatili.”

  25. 12 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

    ili tujipatie moyo wa hekima.

  26. 97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

    Ninaitafakari mchana kutwa.

    98 Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,

    kwa kuwa nimezishika daima.

    99 Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,

    kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

    100 Nina ufahamu zaidi kuliko wazee,

    kwa kuwa ninayatii mausia yako.

  27. 5 Pata hekima, pata ufahamu;

    usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.

    6 Usimwache hekima naye atakuweka salama;

    mpende, naye atakulinda.

    7 Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.

    Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.

  28. 33 Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri

    wa hekima na maarifa ya Mungu!

    Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki,

    na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!

    34 “Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana?

    Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?”

    35 “Au ni nani aliyempa chochote

    ili arudishiwe?”

    36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake.

    Utukufu ni wake milele! Amen.

  29. 12 Je, hekima haipatikani katikati ya wazee?

    Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?

    13 “Hekima na nguvu ni vya Mungu;

    shauri na ufahamu ni vyake yeye.

  30. 16 Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu,

    kuchagua ufahamu kuliko fedha!

  31. 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.

  32. 1 Je, hekima haitani?

    Je, ufahamu hapazi sauti?

    2 Juu ya miinuko karibu na njia,

    penye njia panda, ndipo asimamapo;

    3 kando ya malango yaelekeayo mjini,

    kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:

    4 “Ni ninyi wanaume, ninaowaita;

    ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.

    5 Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili;

    ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.

    6 Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema;

    ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa.

  33. 1 Usiwaonee wivu watu waovu,

    usitamani ushirika nao;

    2 kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri,

    nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara.

    3 Kwa hekima nyumba hujengwa,

    nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa

    4 kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa

    vitu vya thamani na vya kupendeza.

    5 Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa,

    naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu,

    6 kwa kufanya vita unahitaji uongozi

    na kwa ushindi washauri wengi.

    7 Hekima i juu mno kwa mpumbavu,

    katika kusanyiko langoni

    hana lolote la kusema.

  34. 12 “Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?

    Ufahamu unakaa wapi?

    13 Mwanadamu hatambui thamani yake;

    haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

    14 Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’;

    bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’

    15 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote,

    wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.

    16 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri,

    kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.

    17 Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo,

    wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.

  35. 2 Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,

    bali unyenyekevu huja na hekima.

  36. 24 “Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba. 26 Naye kila anayesikia haya maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

  37. 30 Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima,

    nao ulimi wake huzungumza lililo haki.

  38. 24 Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi!

    Kwa hekima ulizifanya zote,

    dunia imejaa viumbe vyako.

  39. 20 Yeyote anayekubali mafundisho hustawi,

    tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana.

    21 Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu,

    na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho.

    22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao,

    bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu.

    23 Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake,

    na midomo yake huchochea mafundisho.

    24 Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali,

    ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

  40. 12 Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima,

    wazimu na upumbavu.

    Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme

    anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa?

    13 Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,

    kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

    14 Mtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,

    lakini mpumbavu anatembea gizani;

    lakini nikaja kuona kwamba

    wote wawili hatima yao inafanana.

    15 Kisha nikafikiri moyoni mwangu,

    “Hatima ya mpumbavu itanipata mimi pia.

    Nitafaidi nini basi kwa kuwa na hekima?”

    Nikasema moyoni mwangu,

    “Hili nalo ni ubatili.”

    16 Kwa maana kwa mtu mwenye hekima,

    kama ilivyo kwa mpumbavu,

    hatakumbukwa kwa muda mrefu,

    katika siku zijazo wote watasahaulika.

    Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,

    mtu mwenye hekima pia lazima atakufa!

  41. 26 Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

  42. 1 Ni nani aliye kama mtu mwenye hekima?

    Ni nani ajuaye maelezo ya mambo?

    Hekima hungʼarisha uso wa mtu na kubadili ugumu wa uso wake.

  43. 13 Pia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana: 14 Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake. 15 Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini. 16 Kwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake.

    17 Maneno ya utulivu ya mwenye hekima

    husikiwa kuliko makelele ya mtawala wa wapumbavu.

    18 Hekima ni bora kuliko silaha za vita,

    lakini mwenye dhambi mmoja

    huharibu mema mengi.

  44. 18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, 19 kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameyadhihirisha kwao. 20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.

    21 Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. 22 Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga 23 na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, na mfano wa ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo.

  45. 15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16 mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana.

  46. 33 Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima,

    nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

  47. 8 Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,

    yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.

  48. 26 Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu,

    bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama.

  49. 16 Nilipotafakari akilini mwangu ili nijue hekima na kuangalia kazi ya mwanadamu duniani, jinsi ambavyo macho yake hayapati usingizi mchana wala usiku, 17 ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna yeyote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.

  50. 4 Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6 Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

    7 Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja. 10 Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha. 11 Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.

  51. 12 Huipinga mipango ya wenye hila,

    ili mikono yao isifikie ufanisi.

    13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao,

    nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali.

  52. 8 Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo,

    lakini mpumbavu apayukaye huangamia.

    9 Mtu mwadilifu hutembea salama,

    lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

  53. 13 Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri;

    asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja.

    14 Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako,

    kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,

    nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.

  54. 10 Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?”

    Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo.

    11 Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema

    na huwafaidia wale walionalo jua.

    12 Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi,

    lakini faida ya maarifa ni hii:

    kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.

    13 Tafakari kile Mungu alichokitenda:

    Nani awezaye kunyoosha

    kile ambacho yeye amekipinda?

    14 Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi,

    lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari:

    Mungu amefanya hiyo moja,

    naam, sanjari na hiyo nyingine.

    Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua

    kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.

  55. 21 Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe,

    na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe.

  56. 13 Bwana anasema:

    “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao

    na kuniheshimu kwa midomo yao,

    lakini mioyo yao iko mbali nami.

    Ibada yao kwangu inatokana na maagizo

    waliyofundishwa na wanadamu.

    14 Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa,

    kwa ajabu juu ya ajabu.

    Hekima ya wenye hekima itapotea,

    nayo akili ya wenye akili itatoweka.”

  57. 23 Hili ndilo asemalo Bwana:

    “Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,

    au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,

    wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,

    24 lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:

    kwamba ananifahamu na kunijua mimi,

    kwamba mimi ndimi Bwana, nitendaye wema,

    hukumu na haki duniani,

    kwa kuwa napendezwa na haya,”

    asema Bwana.

  58. 9 Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya.

    Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa.

    Njia za Bwana ni adili;

    wenye haki huenda katika njia hizo,

    lakini waasi watajikwaa ndani yake.

  59. 54 Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?”

  60. 14 Lakini kusudieni mioyoni mwenu msisumbuke awali kuhusu mtakalosema mbele ya mashtaka. 15 Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo hakuna hata adui yenu mmoja atakayeweza kushindana nayo wala kuipinga.

  61. 4 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, 5 chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika hekalu la Bwana, alipatwa na mshangao.

    6 Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. 7 Lakini sikuamini mambo haya hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana ile taarifa niliyoisikia. 8 Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako!

  62. 36 Ni nani aliyeujalia moyo hekima

    au kuzipa akili ufahamu?

    37 Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu?

    Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni

  63. 33 Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako,

    nami nitayashika mpaka mwisho.

    34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako

    na kuitii kwa moyo wangu wote.

    35 Niongoze kwenye njia ya amri zako,

    kwa kuwa huko napata furaha.

  64. 1 Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu,

    sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,

    2 ili uweze kutunza busara

    na midomo yako ihifadhi maarifa.

  65. 10 Kiburi huzalisha magomvi tu,

    bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

  66. 20 Katika nyumba ya mwenye hekima

    kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta,

    lakini mtu mpumbavu

    hutafuna vyote alivyo navyo.

    21 Yeye afuatiaye haki na upendo

    hupata uzima, mafanikio na heshima.

  67. 30 Hakuna hekima, wala akili, wala mpango

    unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.

  68. 16 Niliwaza mwenyewe, “Tazama, nimekua na kuongezeka katika hekima kuliko yeyote aliyewahi kutawala Yerusalemu kabla yangu. Nimekuwa na uzoefu mkubwa wa hekima na maarifa.” 17 Ndipo nilipojitahidi kufahamu kutofautisha hekima, wazimu na upumbavu, lakini nikatambua hata hili nalo ni kukimbiza upepo.

    18 Kwa kuwa hekima nyingi huleta huzuni kubwa;

    maarifa yanapoongezeka, masikitiko yanaongezeka.

  69. 5 Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika,

    moyo wa hekima utajua wakati muafaka

    na jinsi ya kutenda.

  70. 52 Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

  71. 2 Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. 3 Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa. 4 Ombeni ili nipate kuitangaza Injili kwa udhahiri kama ipasavyo kunena. 5 Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6 Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.

  72. 6 Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni,

    ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.

  73. 43 Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya,

    na atafakari upendo mkuu wa Bwana.

  74. 32 “Basi sasa wanangu, nisikilizeni;

    heri wale wanaozishika njia zangu.

    33 Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima;

    msiyapuuze.

    34 Heri mtu yule anisikilizaye mimi,

    akisubiri siku zote malangoni mwangu,

    akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu.

    35 Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima

    na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana.

    36 Lakini yeyote ashindwaye kunipata

    hujiumiza mwenyewe;

    na wote wanichukiao mimi hupenda mauti.”

  75. 30 Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima,

    naye mwenye hekima huvuta roho za watu.

  76. 33 Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu

    bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.

  77. 3 Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake,

    bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.

  78. 15 Fimbo ya maonyo hutia hekima,

    bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo

    humwaibisha mama yake.

  79. 11 Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja.

  80. 8 “Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,

    wala njia zenu si njia zangu,”

    asema Bwana.

    9 “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia,

    ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu

    na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

  81. 7 Hata korongo aliyeko angani

    anayajua majira yake yaliyoamriwa,

    nao njiwa, mbayuwayu na koikoi

    hufuata majira yao ya kurudi.

    Lakini watu wangu hawajui

    Bwana anachotaka kwao.

    8 “ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara

    kwa sababu tunayo sheria ya Bwana,”

    wakati ambapo kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi

    imeandika kwa udanganyifu?

    9 Wenye hekima wataaibika,

    watafadhaika na kunaswa.

    Kwa kuwa wamelikataa neno la Bwana,

    hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?

  82. 20 Katika kila jambo la hekima na ufahamu kuhusu kile mfalme alichowauliza, aliwaona bora mara kumi zaidi kuliko waganga na wasihiri wote katika ufalme wake wote.

  83. 11 Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi. 12 Mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza, alionekana kuwa na akili nyepesi, maarifa na ufahamu, pia uwezo wa kufasiri ndoto, kueleza mafumbo na kutatua matatizo magumu. Mwite Danieli, naye atakuambia maana ya haya maandishi.”

  84. 3 Wale wenye hekima watangʼaa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watangʼaa kama nyota milele na milele. 4 Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki mpaka wakati wa mwisho. Wengi watakwenda huku na huko, na maarifa yataongezeka.”

  85. 25 Wakati huo Yesu alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. 26 Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

    27 “Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.

  86. 21 Wakati huo Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu, akasema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

  87. 23 Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. 24 Dunia yote ikatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.

  88. 13 Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua,

    lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.

    14 Wenye hekima huhifadhi maarifa,

    bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.

  89. 17 Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima,

    elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo,

    18 kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako

    na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.

    19 Ili tumaini lako liwe katika Bwana,

    hata wewe, ninakufundisha leo.

    20 Je, sijakuandikia misemo thelathini,

    misemo ya mashauri na maarifa,

    21 kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika,

    ili uweze kutoa majibu sahihi

    kwake yeye aliyekutuma?

  90. 12 Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake,

    akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake,

    na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.