46 Bible Verses About Honesty

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Honesty
  1. 17 Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,

    bali shahidi wa uongo husema uongo.

    18 Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga,

    bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

    19 Midomo isemayo kweli hudumu milele,

    bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.

    20 Upo udanganyifu katika mioyo

    ya wale ambao hupanga mabaya,

    bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.

    21 Hakuna dhara linalompata mwenye haki,

    bali waovu wana taabu nyingi.

    22 Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,

    bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.

  2. 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. 9 Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

  3. 10 Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu,

    wala kinywa chake hakipotoshi haki.

    11 Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana;

    mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.

    12 Wafalme huchukia sana kutenda maovu,

    kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki.

    13 Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu;

    humthamini mtu asemaye kweli.

  4. 19 Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makanisa ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana mwenyewe, na ili kuonyesha hisani yetu kuwasaidia. 20 Tunataka kuepuka lawama yoyote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu. 21 Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki si machoni mwa Bwana peke yake, bali pia machoni mwa watu wengine.

  5. 9 Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, 10 nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake. 11 Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote, na ndani ya wote.

  6. 16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

  7. 22 Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, 23 ili mfanywe upya roho na nia zenu, 24 mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

    25 Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.

  8. 10 Kwa maana,

    “Yeyote apendaye uzima

    na kuona siku njema,

    basi auzuie ulimi wake usinene mabaya,

    na midomo yake isiseme hila.

    11 Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema;

    lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

    12 Kwa maana macho ya Bwana

    huwaelekea wenye haki,

    na masikio yake yako makini

    kusikiliza maombi yao.

    Bali uso wa Bwana uko kinyume

    na watendao maovu.”

  9. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.

  10. 17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote.

  11. 35 “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. 36 Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

  12. 13 Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. 14 Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. 15 Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 16 Kwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu.

  13. Zaburi ya Daudi.

    1 Bwana, ni nani awezaye kukaa

    katika Hekalu lako?

    Nani awezaye kuishi

    katika mlima wako mtakatifu?

    2 Ni yule aendaye pasipo mawaa,

    atendaye yaliyo haki,

    asemaye kweli toka moyoni mwake,

    3 na hana masingizio ulimini mwake,

    asiyemtenda jirani yake vibaya,

    na asiyemsingizia mwenzake,

  14. 1 Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,

    bali vipimo sahihi ni furaha yake.

  15. 3 Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,

    bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.

  16. 2 Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu.

  17. 7 Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,

    wamebarikiwa watoto wake baada yake.

  18. 6 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.

  19. 3 Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika

    zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.

  20. 18 Kama vile rungu au upanga au mshale mkali

    ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake.

  21. 14 Hivyo uadilifu umerudishwa nyuma,

    nayo haki inasimama mbali,

    kweli imejikwaa njiani,

    uaminifu hauwezi kuingia.

    15 Kweli haipatikani popote,

    na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.

    Bwana alitazama naye akachukizwa

    kwamba hapakuwepo haki.

  22. 16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, 17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asema Bwana.

  23. 33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36 Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 ‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.

  24. 5 Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote. 6 Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. 7 Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

    8 Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 9 Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.

  25. 4 “Kukuhusu wewe, kama ukienenda kwa unyofu wa moyo na uadilifu, kama baba yako Daudi alivyofanya na kutenda yote ninayoyaagiza kwa kutunza maagizo yangu na sheria, 5 nitakiimarisha kiti chako cha enzi juu ya Israeli milele kama nilivyomwahidi Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe kuwa na mtu kwenye kiti cha enzi cha Israeli.’

  26. 15 Wao hawakudai kupewa hesabu ya fedha kutoka kwa wale waliowapa ili kuwalipa wafanyakazi, kwa sababu walifanya kwa uaminifu wote.

  27. 16 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,

    naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

    17 macho ya kiburi,

    ulimi udanganyao,

    mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

    18 moyo uwazao mipango miovu,

    miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

    19 shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,

    na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

    20 Mwanangu, zishike amri za baba yako,

    wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

  28. 16 Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo.

  29. 26 Jawabu la uaminifu

    ni kama busu la midomoni.

  30. 10 “Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu hata katika mambo makubwa, naye mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya kidunia, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli? 12 Nanyi kama hamkuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?

  31. 9 Mtu mwadilifu hutembea salama,

    lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

  32. 1 Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,

    kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.

  33. 7 Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu, 8 na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema juu yetu.

  34. 24 Epusha kinywa chako na ukaidi;

    weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako.

    25 Macho yako na yatazame mbele,

    kaza macho yako moja kwa moja mbele yako.

    26 Sawazisha mapito ya miguu yako

    na njia zako zote ziwe zimethibitika.

    27 Usigeuke kulia wala kushoto;

    epusha mguu wako na ubaya.

  35. 3 Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana?

    Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

    4 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,

    yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake

    au kuapa kwa kitu cha uongo.

    5 Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana,

    na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

  36. 13 Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi,

    bali mwenye haki huepuka taabu.

    14 Kutokana na tunda la midomo yake

    mtu hujazwa na mambo mema,

    hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.

  37. 17 Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,

    bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.

  38. 6 Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo

    ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.

  39. 10 Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa na bathi.

  40. 37 Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”

    38 Pilato akamuuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lolote alilotenda mtu huyu.

  41. 4 La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa:

    “Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena,

    na ukashinde utoapo hukumu.”

  42. 7 Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa.

  43. 3 Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu.

  44. 7 Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali. 8 Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake. 9 Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwaonya wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.

  45. 22 “Yeye hakutenda dhambi,

    wala hila haikuonekana kinywani mwake.”

  46. 17 Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? 18 Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.