109 Bible Verses About Lies

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Lies
  1. 43 Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. 45 Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini! 46 Je, kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? 47 Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”

  2. 17 Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,

    bali shahidi wa uongo husema uongo.

    18 Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga,

    bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

    19 Midomo isemayo kweli hudumu milele,

    bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.

    20 Upo udanganyifu katika mioyo

    ya wale ambao hupanga mabaya,

    bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.

    21 Hakuna dhara linalompata mwenye haki,

    bali waovu wana taabu nyingi.

    22 Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,

    bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.

  3. 8 Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. 9 Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, 10 nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake.

  4. 17 Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

    20 Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo. 21 Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 22 Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, 23 ili mfanywe upya roho na nia zenu, 24 mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

    25 Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.

  5. 7 Yeye ashindaye atayarithi haya yote, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8 Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

  6. 16 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,

    naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

    17 macho ya kiburi,

    ulimi udanganyao,

    mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

    18 moyo uwazao mipango miovu,

    miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

    19 shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,

    na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

    20 Mwanangu, zishike amri za baba yako,

    wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

  7. 16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

  8. 1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. 2 Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.

    3 Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? 4 Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.”

    5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia.

  9. 11 “ ‘Usiibe.

    “ ‘Usiseme uongo.

    “ ‘Msidanganyane.

    12 “ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu, na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

  10. 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.

    14 “Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake. 15 Huko nje wako mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu, na kila mtu apendaye udanganyifu na kuufanya.

  11. 23 Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo

    ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.

    24 Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake,

    lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.

    25 Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini,

    kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.

    26 Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu,

    lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.

    27 Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake,

    kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.

    28 Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza,

    nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

  12. 6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,

    ili waweze kuishi pamoja nami;

    yeye ambaye moyo wake hauna lawama

    atanitumikia.

    7 Mdanganyifu hatakaa

    nyumbani mwangu,

    yeye asemaye kwa uongo

    hatasimama mbele yangu.

    8 Kila asubuhi nitawanyamazisha

    waovu wote katika nchi;

    nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya

    kutoka mji wa Bwana.

  13. 1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

    2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”

    4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. 5 Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

    6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala. 7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

  14. 4 Wewe si Mungu unayefurahia uovu,

    kwako mtu mwovu hataishi.

    5 Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,

    unawachukia wote watendao mabaya.

    6 Unawaangamiza wasemao uongo.

    Bwana huwachukia

    wamwagao damu na wadanganyifu.

  15. 9 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

    naye amwagaye uongo ataangamia.

  16. 8 Tunajua kwamba sheria ni njema ikiwa inatumika kwa halali kama ilivyokusudiwa. 9 Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru; kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji, 10 kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli, 11 ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa, ambayo mimi nimewekewa amana.

  17. 1 Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. 2 Mafundisho kama hayo huja kupitia kwa waongo ambao ni wanafiki, hali dhamiri zao zikiungua kwa kuchomwa moto.

  18. 27 Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu yeyote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

  19. 5 Mwenye haki huchukia uongo,

    bali waovu huleta aibu na fedheha.

  20. 19 Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Bwana: Nilimwona Bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto. 20 Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’

    “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. 21 Mwishoni, pepo mchafu akajitokeza, akasimama mbele za Bwana na kusema, ‘Nitamshawishi.’

    22 “Bwana akauliza, ‘Kwa njia gani?’

    “Akasema, ‘Nitakwenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’

    “Bwana akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’

    23 “Kwa hiyo sasa Bwana ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. Bwana ameamuru maafa kwa ajili yako.”

  21. 1 Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji

    na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!

    Ningelia usiku na mchana

    kwa kuuawa kwa watu wangu.

    2 Laiti ningekuwa na nyumba

    ya kukaa wasafiri jangwani,

    ningewaacha watu wangu

    na kwenda mbali nao,

    kwa kuwa wote ni wazinzi,

    kundi la watu wadanganyifu.

    3 “Huweka tayari ndimi zao kama upinde,

    ili kurusha uongo;

    wamekuwa na nguvu katika nchi

    lakini si katika ukweli.

    Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,

    hawanitambui mimi,”

    asema Bwana.

    4 “Jihadhari na rafiki zako;

    usiwaamini ndugu zako.

    Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,

    na kila rafiki ni msingiziaji.

    5 Rafiki humdanganya rafiki,

    hakuna yeyote asemaye kweli.

    Wamefundisha ndimi zao kudanganya,

    wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.

    6 Unakaa katikati ya udanganyifu;

    katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”

    asema Bwana.

  22. 5 Shahidi mwaminifu hadanganyi,

    bali shahidi wa uongo humimina uongo.

  23. 6 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.

  24. 10 Kwa maana,

    “Yeyote apendaye uzima

    na kuona siku njema,

    basi auzuie ulimi wake usinene mabaya,

    na midomo yake isiseme hila.

    11 Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema;

    lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

    12 Kwa maana macho ya Bwana

    huwaelekea wenye haki,

    na masikio yake yako makini

    kusikiliza maombi yao.

    Bali uso wa Bwana uko kinyume

    na watendao maovu.”

  25. 3 Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao,

    toka tumboni mwa mama zao

    ni wakaidi na husema uongo.

  26. 4 Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya;

    mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.

  27. 1 Hakika mkono wa Bwana si mfupi hata usiweze kuokoa,

    wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia.

    2 Lakini maovu yenu yamewatenga

    ninyi na Mungu wenu,

    dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake,

    ili asisikie.

    3 Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu

    na vidole vyenu kwa hatia.

    Midomo yenu imenena uongo,

    nazo ndimi zenu zimenongʼona mambo maovu.

    4 Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki;

    hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki.

    Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo,

    huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.

  28. 4 Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 5 Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. 6 Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.

  29. 31 Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. 32 Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”

  30. 12 Yeyote kati yenu anayependa uzima

    na kutamani kuziona siku nyingi njema,

    13 basi auzuie ulimi wake na mabaya,

    na midomo yake kutokana na kusema uongo.

  31. 163 Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo,

    lakini napenda sheria yako.

  32. 18 Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo,

    na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu.

    19 Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani,

    lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.

  33. 5 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

    naye amwagaye uongo hataachwa huru.

  34. 8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. 9 Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo, 10 na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 11 Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo, 12 na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.

  35. 7 Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu:

    je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!

  36. 6 Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo

    ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.

  37. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi.

    1 Nijibu nikuitapo,

    Ee Mungu wangu mwenye haki!

    Nipumzishe katika shida zangu;

    nirehemu, usikie ombi langu.

    2 Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu

    kuwa aibu mpaka lini?

    Mtapenda udanganyifu

    na kufuata miungu ya uongo mpaka lini?

    3 Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga

    wale wamchao kwa ajili yake;

    Bwana atanisikia nimwitapo.

    4 Katika hasira yako, usitende dhambi.

    Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya

    mkiichunguza mioyo yenu.

  38. 2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.

    Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.

    3 Unapenda mabaya kuliko mema,

    uongo kuliko kusema kweli.

    4 Unapenda kila neno lenye kudhuru,

    ewe ulimi wenye hila!

    5 Hakika Mungu atakushusha chini

    kwa maangamizi ya milele:

    atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu

    kutoka hema yako,

    atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.

  39. 1 Sikieni neno la Bwana, enyi Waisraeli,

    kwa sababu Bwana analo shtaka

    dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi:

    “Hakuna uaminifu, hakuna upendo,

    hakuna kumjua Mungu katika nchi.

    2 Kuna kulaani tu, uongo na uuaji,

    wizi na uzinzi,

    bila kuwa na mipaka,

    nao umwagaji damu mmoja

    baada ya mwingine.

  40. 16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, 17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asema Bwana.

  41. 17 Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo. 18 Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti.

  42. 9 Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.

  43. 16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. 18 Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20 Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini yule aishiye kwa ukweli huja kwenye nuru, ili ionekane wazi kwamba matendo yake yametendeka katika Mungu.”

  44. 3 Mtamshambulia mtu hata lini?

    Je, ninyi nyote mtamtupa chini,

    ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika?

    4 Walikusudia kikamilifu kumwangusha

    toka mahali pake pa fahari;

    wanafurahia uongo.

    Kwa vinywa vyao hubariki,

    lakini ndani ya mioyo yao hulaani.

  45. 29 Niepushe na njia za udanganyifu,

    kwa neema unifundishe sheria zako.

    30 Nimechagua njia ya kweli,

    nimekaza moyo wangu katika sheria zako.

  46. 8 Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo;

    usinipe umaskini wala utajiri,

    bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.

    9 Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana

    na kusema, ‘Bwana ni nani?’

    Au nisije nikawa maskini nikaiba,

    nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.

  47. 13 Mabaki ya Israeli hayatafanya kosa;

    hawatasema uongo,

    wala udanganyifu hautakuwa

    katika vinywa vyao.

    Watakula na kulala

    wala hakuna yeyote

    atakayewaogopesha.”

  48. 20 Usimshuhudie jirani yako uongo.

  49. 22 Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha na mivao miwili ya mavazi.’ ”

    23 Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mivao miwili ya mavazi. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi. 24 Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka. 25 Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Elisha bwana wake.

    Elisha akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?”

    Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda popote.”

    26 Lakini Elisha akamwambia, “Je, roho yangu haikuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka kwenye gari lake ili kukulaki? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea nguo, mashamba ya mizeituni, mashamba ya mizabibu, makundi ya kondoo na mbuzi, makundi ya ngʼombe, au watumishi wa kiume na wa kike? 27 Ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Elisha, mwenye ukoma, mweupe kama theluji.

  50. Zaburi ya Daudi.

    1 Bwana, ni nani awezaye kukaa

    katika Hekalu lako?

    Nani awezaye kuishi

    katika mlima wako mtakatifu?

    2 Ni yule aendaye pasipo mawaa,

    atendaye yaliyo haki,

    asemaye kweli toka moyoni mwake,

    3 na hana masingizio ulimini mwake,

    asiyemtenda jirani yake vibaya,

    na asiyemsingizia mwenzake,

  51. 22 Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,

    afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.

    23 Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima,

    kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,

    bila kuguswa na shida.

  52. 22 Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. 23 Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba. Yeyote anayemkubali Mwana anaye na Baba pia.

  53. 11 Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. 12 Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai. 13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.”

    14 Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura. 15 Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akapelekwa kwa nyumba ya mfalme.

  54. 15 Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, 16 “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” 17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. 18 Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

    19 Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

    20 Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. 21 Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.

  55. 19 Mungu si mtu, hata aseme uongo,

    wala yeye si mwanadamu, hata ajute.

    Je, anasema, kisha asitende?

    Je, anaahidi, asitimize?

  56. 9 Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote,

    ni mwovu kupita kiasi.

    Ni nani awezaye kuujua?

    10 “Mimi Bwana huchunguza moyo

    na kuzijaribu nia,

    ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake,

    kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”

  57. 14 Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu

    nimeona jambo baya sana:

    Wanafanya uzinzi

    na kuenenda katika uongo.

    Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,

    kwa ajili hiyo hakuna yeyote

    anayeachana na uovu wake.

    Wote wako kama Sodoma kwangu;

    watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”

  58. 4 Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,

    asiyewategemea wenye kiburi,

    wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

  59. 2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo

    na ndimi za udanganyifu.

  60. 32 Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asema Bwana. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo,” asema Bwana.

  61. 18 Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. 19 Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. 20 Haya ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.”

  62. 14 Lakini ikiwa mna wivu na ni wenye chuki na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu kwa ajili ya hayo wala msiikatae kweli.

  63. 9 Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?”

    Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”

  64. 18 Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.”

    Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?”

    19 Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.”

  65. 25 Shahidi wa kweli huokoa maisha,

    bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.

  66. 1 Ole wa mji umwagao damu,

    uliojaa uongo,

    umejaa nyara,

    usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.

  67. 3 Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu? 4 La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa:

    “Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena,

    na ukashinde utoapo hukumu.”

  68. 12 Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?”

    13 Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ 14 Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.”

    15 Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.”

    Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”

  69. 6 Hivyo Isaki akaishi huko Gerari.

    7 Watu wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumuua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.”

    8 Wakati Isaki alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona jinsi Isaki alivyomkumbatia Rebeka mke wake. 9 Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’ ”

    Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.”

    10 Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu yeyote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.”

    11 Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.”

  70. 12 Kama mtawala akisikiliza uongo,

    maafisa wake wote huwa waovu.

  71. 33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36 Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 ‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.

  72. 17 Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli.

  73. 2 Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo.

  74. 1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

    2 “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu,

  75. 6 Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni,

    ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.

  76. 23 Lakini wewe, Ee Mungu,

    utawashusha waovu katika shimo la uharibifu.

    Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila,

    hawataishi nusu ya siku zao.

    Lakini mimi ninakutumaini wewe.

  77. 28 Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu,

    au kutumia midomo yako kudanganya.

  78. 6 Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli.

  79. 21 Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli.

  80. 31 Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. 32 Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.”

    33 Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.”

    34 Kisha Yakobo akararua nguo zake, akavaa nguo ya gunia na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi. 35 Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia.

  81. 2 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,

    Mwenyezi ambaye amenifanya

    nionje uchungu wa nafsi,

    3 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,

    nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,

    4 midomo yangu haitanena uovu,

    wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.

    5 Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;

    hadi nife, sitakana uadilifu wangu.

  82. 3 Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana?

    Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

    4 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,

    yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake

    au kuapa kwa kitu cha uongo.

    5 Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana,

    na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

  83. 11 Katika taabu yangu nilisema,

    “Wanadamu wote ni waongo.”

  84. 5 “Kila neno la Mungu ni kamilifu;

    yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

    6 Usiongeze kwenye maneno yake,

    ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.

  85. 22 Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga 23 na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, na mfano wa ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo.

    24 Kwa hiyo, Mungu akawaacha wazifuate tamaa mbaya za mioyo yao katika uasherati, hata wakavunjiana heshima miili yao wao kwa wao. 25 Kwa sababu waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba, ahimidiwaye milele! Amen.

  86. 12 Nami nitaendelea kufanya lile ninalofanya sasa ili nisiwape nafasi wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia.

    13 Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Kristo. 14 Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. 15 Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.

  87. 18 Kama vile rungu au upanga au mshale mkali

    ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake.

  88. 28 Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo,’ wakati Bwana hajasema.

  89. 55 Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake.

  90. 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 12 Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 14 Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 16 Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

  91. 9 Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.

  92. 24 Akamuuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?”

    Akajibu, “Mimi ndiye.”

  93. 1 Bwana akamwambia Mose: 2 “Kama mtu yeyote akitenda dhambi, naye si mwaminifu kwa Bwana kwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa, au kimeachwa chini ya utunzaji wake, au kimeibwa, au kama akimdanganya, 3 au akiokota mali iliyopotea na akadanganya, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu waweza kuitenda; 4 wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata, 5 au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia.

  94. 1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja jina lake Rahabu na kukaa humo.

    2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” 3 Hivyo mfalme wa Yeriko akatuma huu ujumbe kwa Rahabu: “Watoe wale watu waliokujia na kuingia nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi yote.”

    4 Lakini huyo mwanamke alikuwa amewachukua hao watu wawili na kuwaficha. Akasema, “Naam, watu hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. 5 Kulipoingia giza, wakati wa kufunga lango la mji, watu hao waliondoka. Sijui njia waliyoiendea. Wafuatilieni haraka. Huenda mkawapata.” 6 (Lakini alikuwa amewapandisha darini akawafunika kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini.)

  95. 2 Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;

    midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

    3 Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila

    na kila ulimi uliojaa majivuno,

    4 ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;

    midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

    5 “Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge

    na kulia kwa uchungu kwa wahitaji,

    nitainuka sasa,” asema Bwana.

    “Nitawalinda kutokana na wale

    wenye nia mbaya juu yao.”

    6 Maneno ya Bwana ni safi,

    kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,

    iliyosafishwa mara saba.

  96. 18 Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,

    kwa maana kwa kiburi na dharau

    wao husema kwa majivuno

    dhidi ya wenye haki.

  97. 12 Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao,

    kwa ajili ya maneno ya midomo yao,

    waache wanaswe katika kiburi chao.

    Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,

  98. 14 Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia,

    tawi la mtende na tete katika siku moja.

    15 Wazee na watu mashuhuri ndio vichwa,

    nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia.

    16 Wale wanaowaongoza watu hawa wanawapotosha,

    nao wale wanaoongozwa wamepotoka.

  99. 6 Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Bwana amesema,” wakati Bwana hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa. 7 Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “Bwana asema,” lakini Mimi sijasema?

    8 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ya uongo wa maneno yenu na kwa madanganyo ya maono yenu, Mimi ni kinyume na ninyi, asema Bwana Mwenyezi. 9 Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.

  100. 69 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”

    70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.”

    71 Alipotoka nje kufika kwenye lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwepo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”

    72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Mimi simjui huyo!”

    73 Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”

    74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui mtu huyo!”

    Papo hapo jogoo akawika.

  101. 9 Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, 10 wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu. 11 Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.

  102. 26 Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu.

  103. 13 Naye akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi. 14 Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kuzifanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya wakaao duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 15 Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa.

  104. 1 Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,

    bali vipimo sahihi ni furaha yake.

  105. 7 Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,

    hufanya mipango miovu

    ili kumwangamiza maskini kwa uongo,

    hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

  106. 8 Alisema, “Hakika wao ni watu wangu,

    wana ambao hawatanidanganya”;

    hivyo akawa Mwokozi wao.

  107. 19 Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi.

  108. 10 Kama ilivyoandikwa:

    “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

    11 Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,

    hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

    12 Wote wamepotoka,

    wote wameoza pamoja;

    hakuna atendaye mema,

    naam, hakuna hata mmoja.”

    13 “Makoo yao ni makaburi wazi;

    kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”

    “Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”

    14 “Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”

  109. 17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. 20 Badala yake:

    “Kama adui yako ana njaa, mlishe;

    kama ana kiu, mpe kinywaji.

    Kwa kufanya hivyo,

    unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”

    21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.