34 Bible Verses About Gossip

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Gossip
  1. 20 Bila kuni moto huzimika;

    pasipo uchongezi ugomvi humalizika.

    21 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto,

    ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.

    22 Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;

    huingia sehemu za ndani sana za mtu.

  2. 28 Nao kwa kuwa hawakuona umuhimu wa kudumisha ufahamu wa Mungu, yeye akawaachilia wafuate akili za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa. 29 Wakiwa wamejawa na udhalimu wa kila namna, uasherati, uovu, tamaa mbaya na hila. Wamejawa na husuda, uuaji, ugomvi, udanganyifu, hadaa na nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 30 wasingiziaji, wanaomchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno, wenye hila, wasiotii wazazi wao, 31 wajinga, wasioamini, wasio na huruma na wakatili. 32 Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda.

  3. 11 Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,

    bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.

    12 Mtu asiye na akili humdharau jirani yake,

    bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.

    13 Masengenyo husaliti tumaini,

    bali mtu mwaminifu hutunza siri.

  4. 11 Lakini kwa habari za wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena. 12 Nao kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kukiuka ahadi yao ya kwanza. 13 Zaidi ya hayo, wajane kama hao huwa na tabia ya uvivu wakizurura nyumba kwa nyumba, wala hawawi wavivu tu, bali pia huwa wasengenyaji, wajiingizao katika mambo yasiyowahusu na kusema mambo yasiyowapasa kusema. 14 Hivyo nawashauri wajane vijana waolewe, wazae watoto na wasimamie nyumba zao, wasije wakampa adui nafasi ya kutushutumu.

  5. 28 Mtu mpotovu huchochea ugomvi,

    nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.

  6. 6 Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi

    na kinywa chake hualika kipigo.

    7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake

    na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

    8 Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;

    huingia sehemu za ndani sana za mtu.

  7. 19 Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,

    kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.

  8. 16 “ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako.

    “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Bwana.

  9. 20 Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.

  10. 18 Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo,

    na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu.

  11. 9 Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,

    bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.

  12. 33 “Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake. 34 Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake. 35 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake. 36 Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena. 37 Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”

  13. 1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

  14. 5 Adui zangu wanasema kwa hila,

    “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”

    6 Kila anapokuja mtu kunitazama,

    huzungumza uongo,

    huku moyo wake hukusanya masingizio;

    kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.

    7 Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu,

    hao huniwazia mabaya sana, wakisema,

    8 “Ugonjwa mbaya sana umempata,

    kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”

  15. 3 Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,

    weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

  16. 19 Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani,

    lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.

  17. 23 Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake

    hujilinda na maafa.

  18. 5 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,

    huyo nitamnyamazisha;

    mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi

    huyo sitamvumilia.

  19. 29 Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao.

  20. 9 Kama ukifanya shauri na jirani yako,

    usisaliti siri ya mtu mwingine,

    10 ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha

    na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka.

  21. 10 Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri. 11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?”

    12 Kulikuwa na minongʼono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.”

    Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.” 13 Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.

  22. 5 Basi, mara ya tano, Sanbalati akamtuma msaidizi wake kwangu akiwa na ujumbe wa aina ile ile, naye alikuwa amechukua mkononi mwake barua isiyofungwa, 6 iliyokuwa imeandikwa:

    “Habari imeenezwa miongoni mwa mataifa, naye Geshemu anasema kwamba ni kweli, kuwa wewe na Wayahudi mnafanya hila ya kuasi, ndiyo sababu mnajenga ukuta. Zaidi ya hayo, kufuatana na taarifa hizi, karibuni utakuwa mfalme wao, 7 na hata umewateua manabii wafanye tangazo hili kukuhusu wewe huko Yerusalemu: ‘Yuko mfalme katika Yuda!’ Sasa taarifa hii itarudishwa kwa mfalme. Basi njoo, tufanye shauri pamoja.”

    8 Nilimpelekea jibu hili: “Hakuna jambo kama hilo unalosema linalofanyika. Unalitunga tu kwenye kichwa chako.”

  23. 23 Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua,

    ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira.

  24. 11 Mpumbavu huonyesha hasira yake yote,

    bali mwenye hekima hujizuia.

  25. 2 Usiwe mwepesi kuzungumza,

    usiwe na haraka katika moyo wako

    kuzungumza lolote mbele za Mungu.

    Mungu yuko mbinguni

    nawe uko duniani,

    kwa hiyo maneno yako

    na yawe machache.

    3 Kama vile ndoto huja

    wakati kuna shughuli nyingi,

    ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu

    wakati kuna maneno mengi.

  26. 11 Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.

  27. 1 Inakupasa kufundisha itikadi sahihi. 2 Wafundishe wazee kuwa na kiasi, wastahivu, wenye busara na wanyofu katika imani, upendo na saburi.

    3 Vivyo hivyo, wafundishe wanawake wazee kuwa na mwenendo wa utakatifu, wala wasiwe wasingiziaji au walevi, bali wafundishe yale yaliyo mema, 4 ili waweze kuwafundisha wanawake vijana kuwa na kiasi, wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao, 5 wawe waaminifu, watakatifu, wakitunza vyema nyumba zao, wema, watiifu kwa waume zao, ili mtu yeyote asije akalikufuru neno la Mungu.

    6 Vivyo hivyo, himiza vijana wawe na kiasi. 7 Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu, 8 na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema juu yetu.

    9 Wafundishe watumwa kuwatii mabwana zao katika kila jambo, wakijitahidi kuwapendeza wala wasijibizane nao, 10 wala wasiwaibie, bali waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa, ili kwa kila namna wayafanye mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yawe ya kuvutia.

    11 Kwa maana neema ya Mungu ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa. 12 Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa, 13 huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu, aliye Mwokozi wetu Yesu Kristo. 14 Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani, wale walio na juhudi katika kutenda mema.

    15 Basi wewe fundisha mambo haya. Onya na kukaripia kwa mamlaka yote. Mtu yeyote asikudharau.

  28. 1 Wakumbushe watu kuwanyenyekea watawala na kuwatii wenye mamlaka, wawe tayari kutenda kila lililo jema. 2 Wasimnenee mtu yeyote mabaya, wasiwe wagomvi, bali wawe wapole, wakionyesha unyenyekevu kwa watu wote.

  29. 13 basi auzuie ulimi wake na mabaya,

    na midomo yake kutokana na kusema uongo.

  30. 9 Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu

    humwangamiza jirani yake,

    bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.

  31. 21 Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,

    nao waupendao watakula matunda yake.

  32. 15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. 16 Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu. 17 Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa. Naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru.

  33. 31 Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.

  34. 26 Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu.