38 Bible Verses About Keeping Your Word

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Keeping Your Word
  1. 33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36 Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 ‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.

  2. 1 Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndilo Bwana analoagiza: 2 Mwanaume awekapo nadhiri kwa Bwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.

    3 “Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwa Bwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi, 4 na baba yake akasikia kuhusu nadhiri au ahadi yake lakini asimwambie lolote, ndipo nadhiri zake zote na kila ahadi aliyoiweka na kujifunga kwayo itathibitika. 5 Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake yoyote aliyojifunga kwayo itakayosimama; Bwana atamweka huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.

    6 “Ikiwa ataolewa baada ya kuweka nadhiri au baada ya midomo yake kutamka ahadi fulani bila kufikiri akawa amejifunga hivyo, 7 na mume wake akasikia habari hiyo asimwambie neno lolote, ndipo nadhiri zake ama ahadi zake ambazo alikuwa amejifunga nazo zitathibitika. 8 Lakini ikiwa mume wake atamkataza atakaposikia kuhusu hilo, atakuwa ametangua nadhiri ambazo zilikuwa zimemfunga mkewe, ama ahadi aliyotamka pasipo kufikiri ambayo amejifunga kwayo, naye Bwana atamweka huru yule mwanamke.

  3. 4 Wakati unapomwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza. Yeye hafurahii wapumbavu; timiza nadhiri yako. 5 Ni afadhali usiweke nadhiri kuliko kuiweka na usiitimize. 6 Usiruhusu kinywa chako kukuingiza dhambini. Tena usijitetee mbele ya huyo mjumbe wa hekaluni, ukisema, “Niliweka nadhiri kwa makosa.” Kwa nini Mungu akasirike kwa ajili ya yale unayosema na kuiharibu kazi ya mikono yako? 7 Kuota ndoto kwingi na maneno mengi ni ubatili. Kwa hiyo simama katika kicho cha Mungu.

  4. 21 Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. 22 Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. 23 Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

  5. Zaburi ya Daudi.

    1 Bwana, ni nani awezaye kukaa

    katika Hekalu lako?

    Nani awezaye kuishi

    katika mlima wako mtakatifu?

    2 Ni yule aendaye pasipo mawaa,

    atendaye yaliyo haki,

    asemaye kweli toka moyoni mwake,

    3 na hana masingizio ulimini mwake,

    asiyemtenda jirani yake vibaya,

    na asiyemsingizia mwenzake,

    4 ambaye humdharau mtu mbaya,

    lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana,

    yule atunzaye kiapo chake

    hata kama anaumia.

    5 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,

    na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.

    Mtu afanyaye haya

    kamwe hatatikisika.

  6. 11 “ ‘Usiibe.

    “ ‘Usiseme uongo.

    “ ‘Msidanganyane.

  7. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.

  8. 12 Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, iwe kwa mbingu au kwa dunia, au kwa kitu kingine chochote. “Ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, la sivyo mtahukumiwa.

  9. 28 Yakobo akaishi Misri miaka kumi na saba, nayo miaka ya maisha yake ilikuwa 147. 29 Wakati ulipokaribia wa Israeli kufa, akamwita mwanawe Yosefu na kumwambia, “Kama nimepata kibali machoni pake, weka mkono wako chini ya paja langu na uniahidi kuwa utanifanyia fadhili na uaminifu. Usinizike Misri, 30 lakini nitakapopumzika na baba zangu, unichukue kutoka Misri, ukanizike walipozikwa.”

    Yosefu akamwambia, “Nitafanya kama unavyosema.”

    31 Akamwambia, “Niapie.” Ndipo Yosefu akamwapia, naye Israeli akaabudu, akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake.

  10. 4 Wewe si Mungu unayefurahia uovu,

    kwako mtu mwovu hataishi.

    5 Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,

    unawachukia wote watendao mabaya.

    6 Unawaangamiza wasemao uongo.

    Bwana huwachukia

    wamwagao damu na wadanganyifu.

  11. 22 Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,

    bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.

  12. 25 Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka

    na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.

  13. 19 Mungu si mtu, hata aseme uongo,

    wala yeye si mwanadamu, hata ajute.

    Je, anasema, kisha asitende?

    Je, anaahidi, asitimize?

  14. 7 Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

  15. 14 “Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njema Bwana Mungu wenu alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia.

  16. 9 Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote,

    ni mwovu kupita kiasi.

    Ni nani awezaye kuujua?

    10 “Mimi Bwana huchunguza moyo

    na kuzijaribu nia,

    ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake,

    kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”

  17. 8 Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

  18. 22 Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. 23 Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.”

    24 Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”

  19. 20 Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, “Kama Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari niendayo, akinipa chakula nile na nguo nivae 21 na nirudi salama nyumbani kwa baba yangu, hapo ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu, 22 nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu na katika yote utakayonipa nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

  20. 13 Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake.

  21. 11 Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.”

  22. 7 Mnamo mwisho wa mwaka wa nne, Absalomu akamwambia mfalme, “Naomba unipe ruhusa niende Hebroni nikatimize nadhiri niliyomwekea Bwana. 8 Wakati mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii, ‘Ikiwa Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu Bwana huko Hebroni.’ ”

    9 Mfalme akamwambia, “Enenda kwa amani.” Hivyo akaenda Hebroni.

    10 Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ” 11 Watu mia mbili kutoka Yerusalemu walikuwa wamefuatana na Absalomu. Walikuwa wamealikwa kama wageni nao walikwenda kwa nia njema, pasipo kujua lolote. 12 Wakati Absalomu alipokuwa anatoa dhabihu, pia akatuma aitwe Ahithofeli, Mgiloni, mshauri wa Daudi, aje kutoka Gilo, ambao ndio mji wake wa nyumbani. Kwa hiyo mpango wa hila ukapata nguvu, na idadi ya waliofuatana na Absalomu ikaongezeka.

  23. 28 “Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu, na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Sheria ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu, 29 basi hawa wote wanajiunga na ndugu zao na wakuu wao, na kujifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Mose mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za Bwana, Bwana wetu.

  24. 16 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,

    naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

    17 macho ya kiburi,

    ulimi udanganyao,

    mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

    18 moyo uwazao mipango miovu,

    miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

    19 shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,

    na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

  25. 9 Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

    naye amwagaye uongo ataangamia.

  26. 4 “Jihadhari na rafiki zako;

    usiwaamini ndugu zako.

    Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,

    na kila rafiki ni msingiziaji.

    5 Rafiki humdanganya rafiki,

    hakuna yeyote asemaye kweli.

    Wamefundisha ndimi zao kudanganya,

    wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.

    6 Unakaa katikati ya udanganyifu;

    katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”

    asema Bwana.

    7 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

    “Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu,

    kwani ni nini kingine niwezacho kufanya

    kwa sababu ya dhambi ya watu wangu?

    8 Ndimi zao ni mshale wenye sumu,

    hunena kwa udanganyifu.

    Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,

    lakini moyoni mwake humtegea mtego.

    9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”

    asema Bwana.

    “Je, nisijilipizie kisasi

    kwa taifa kama hili?”

  27. 9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

    nitakutolea dhabihu.

    Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

    Wokovu watoka kwa Bwana.”

  28. 1 Ole wa mji umwagao damu,

    uliojaa uongo,

    umejaa nyara,

    usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.

  29. 71 Alipotoka nje kufika kwenye lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwepo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”

    72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Mimi simjui huyo!”

    73 Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.”

    74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui mtu huyo!”

    Papo hapo jogoo akawika. 75 Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amesema: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

  30. 1 Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama vile watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Bwana wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka. 2 Hata hivyo, wengi watafuata njia zao za ufisadi, na kwa ajili yao njia ya kweli itatukanwa. 3 Nao katika tamaa zao mbaya, walimu hawa watajipatia faida kwenu kwa hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, wala uangamivu wao haujalala usingizi.

  31. 34 Mimi sitavunja agano langu

    wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.

  32. 2 Usiwe mwepesi kuzungumza,

    usiwe na haraka katika moyo wako

    kuzungumza lolote mbele za Mungu.

    Mungu yuko mbinguni

    nawe uko duniani,

    kwa hiyo maneno yako

    na yawe machache.

  33. 11 Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

  34. 1 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,

    ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi

    kwa ajili ya mwingine,

    2 kama umetegwa na ulichosema,

    umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

    3 basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,

    kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:

    Nenda ukajinyenyekeshe kwake;

    msihi jirani yako!

  35. 25 Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.

  36. 3 Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 4 Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 5 Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake.

  37. 17 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru

    na kuliita jina la Bwana.

    18 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana

    mbele za watu wake wote,

  38. 18 Baada ya kukaa Korintho kwa muda, Paulo akaagana na wale ndugu walioamini, akasafiri kwa njia ya bahari kwenda Shamu akiwa amefuatana na Prisila na Akila. Walipofika Kenkrea, Paulo alinyoa nywele zake kwa kuwa alikuwa ameweka nadhiri.