40 Bible Verses About Integrity
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)
-
3 Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
4 Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu,
bali haki huokoa kutoka mautini.
5 Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,
bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
6 Haki ya wanyofu huwaokoa,
bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
7 Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka;
yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
8 Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu,
naye mtu mwovu huingia humo badala yake.
9 Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu
humwangamiza jirani yake,
bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
10 Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;
mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
11 Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,
bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
-
Zaburi ya Daudi.
1 Ee Bwana, nithibitishe katika haki,
maana nimeishi maisha yasiyo na lawama;
nimemtumainia Bwana
bila kusitasita.
2 Ee Bwana, unijaribu, unipime,
uuchunguze moyo wangu
na mawazo yangu;
3 kwa maana upendo wako
uko mbele yangu daima,
nami natembea siku zote
katika kweli yako.
4 Siketi pamoja na watu wadanganyifu,
wala siandamani na wanafiki,
5 ninachukia kusanyiko la watenda mabaya
na ninakataa kuketi pamoja na waovu.
6 Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia,
naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana,
7 nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa,
huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.
8 Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi,
mahali ambapo utukufu wako hukaa.
9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi,
wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu,
10 ambao mikononi mwao kuna mipango miovu,
ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa.
11 Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama;
nikomboe na unihurumie.
12 Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare;
katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.
-
9 Mtu mwadilifu hutembea salama,
lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.
-
6 Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,
bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?
7 Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,
wamebarikiwa watoto wake baada yake.
-
1 Ilimpendeza Dario kuteua wakuu 120 kutawala katika ufalme wake wote, 2 pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara. 3 Basi Danieli alijidhihirisha, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote. 4 Walipofahamu hilo, wakuu na wasimamizi wakajaribu kutafuta sababu za kumshtaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu, wala hakupatikana na upotovu au uzembe. 5 Mwishoni watu hawa walisema, “Kamwe hatutapata msingi wa mashtaka dhidi ya huyu Danieli isipokuwa iwe inahusiana na sheria ya Mungu wake.”
-
19 Tazama adui zangu walivyo wengi,
pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!
20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe,
usiniache niaibike,
kwa maana nimekukimbilia wewe.
21 Uadilifu na uaminifu vinilinde,
kwa sababu tumaini langu ni kwako.
-
4 “Kukuhusu wewe, kama ukienenda kwa unyofu wa moyo na uadilifu, kama baba yako Daudi alivyofanya na kutenda yote ninayoyaagiza kwa kutunza maagizo yangu na sheria, 5 nitakiimarisha kiti chako cha enzi juu ya Israeli milele kama nilivyomwahidi Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe kuwa na mtu kwenye kiti cha enzi cha Israeli.’
-
3 Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”
-
11 Najua kwamba wapendezwa nami,
kwa kuwa adui yangu hanishindi.
12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza
na kuniweka kwenye uwepo wako milele.
13 Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele.
Amen na Amen.
-
6 Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama
kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.
-
1 Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,
kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.
-
9 Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”
10 Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”
Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.
-
5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.”
6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse.
-
8 Bwana na awahukumu kabila za watu.
Nihukumu Ee Bwana,
kwa kadiri ya haki yangu,
kwa kadiri ya uadilifu wangu,
Ewe Uliye Juu Sana.
-
Zaburi ya Daudi.
1 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;
kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.
2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:
utakuja kwangu lini?
Nitatembea nyumbani mwangu
kwa moyo usio na lawama.
-
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. 9 Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
-
22 Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana. 23 Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, 24 kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia.
-
1 Samweli akawaambia Israeli wote, “Nimesikiliza kila kitu mlichoniambia nami nimewawekea mfalme juu yenu. 2 Sasa mnaye mfalme kama kiongozi wenu. Lakini kwa habari yangu mimi ni mzee na nina mvi, nao wanangu wapo hapa pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu mpaka siku hii ya leo. 3 Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele za Bwana na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, mimi nitawarudishia.”
4 Wakajibu, “Hujatudanganya wala kutuonea. Hujapokea chochote kutoka kwenye mkono wa mtu awaye yote.”
5 Samweli akawaambia, “Bwana ni shahidi juu yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta chochote mkononi mwangu.”
Wakasema, “Yeye ni shahidi.”
-
70 Akamchagua Daudi mtumishi wake
na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.
71 Kutoka kuchunga kondoo alimleta
kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo,
wa Israeli urithi wake.
72 Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo,
kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.
-
7 Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu, 8 na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema juu yetu.
-
13 Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? 14 Lakini mmebarikiwa hata kama ikiwalazimu kuteseka kwa ajili ya haki. “Msiogope vitisho vyao, wala msiwe na wasiwasi.” 15 Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, 16 mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao.
17 Kwa maana ni afadhali kupata mateso kwa ajili ya kutenda mema, kama kuteseka huko ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu.
-
Hotuba Ya Mwisho Ya Ayubu
1 Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
2 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,
Mwenyezi ambaye amenifanya
nionje uchungu wa nafsi,
3 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,
nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,
4 midomo yangu haitanena uovu,
wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;
hadi nife, sitakana uadilifu wangu.
6 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha;
dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
-
22 Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,
bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
-
5 Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi. 7 Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali. 8 Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.
-
4 Je, yeye hazioni njia zangu
na kuihesabu kila hatua yangu?
5 “Kama nimeishi katika uongo
au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,
6 Mungu na anipime katika mizani za uaminifu,
naye atajua kwamba sina hatia:
7 kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia,
kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu,
au kama mikono yangu imetiwa unajisi,
8 basi wengine na wale nilichokipanda,
nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.
-
31 Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.
-
2 Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu.
-
8 Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi. 9 Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” 10 Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yosefu siku baada ya siku, Yosefu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye.
11 Siku moja Yosefu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwepo na mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. 12 Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia.
-
6 Kwa maana Bwana hutoa hekima,
na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7 Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,
yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,
8 kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki
na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.
-
3 Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika
zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.
-
25 Macho yako na yatazame mbele,
kaza macho yako moja kwa moja mbele yako.
26 Sawazisha mapito ya miguu yako
na njia zako zote ziwe zimethibitika.
27 Usigeuke kulia wala kushoto;
epusha mguu wako na ubaya.
-
6 Haki humlinda mtu mwadilifu,
bali uovu humwangusha mwenye dhambi.
-
3 Macho ya Bwana yako kila mahali,
yakiwaangalia waovu na wema.
-
18 Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama
hulindwa salama,
bali yeye ambaye njia zake ni potovu
ataanguka ghafula.
-
33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36 Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 ‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.
-
22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hilo ni giza kuu namna gani!
-
10 “Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu hata katika mambo makubwa, naye mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa.
-
16 Kwa hiyo ninajitahidi siku zote kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu.
-
1 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
-
2 Tupatieni nafasi mioyoni mwenu. Hatujamkosea mtu yeyote, hatujampotosha mtu yeyote, wala hatujamdhulumu mtu yeyote.
Shows Read in context, Share and Copy.