77 Bible Verses About Singing

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Singing
  1. 18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

  2. 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. 17 Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.

  3. 1 Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha;

    tumfanyie kelele za shangwe

    Mwamba wa wokovu wetu.

    2 Tuje mbele zake kwa shukrani,

    tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

  4. 24 Kufuata maelekezo haya, yule mkuu wa gereza akawaweka katika chumba cha ndani sana mle gerezani, na akawafunga miguu yao kwa minyororo.

    25 Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26 Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka.

  5. 8 Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu. 9 Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema:

    “Wewe unastahili kukitwaa kitabu

    na kuzivunja lakiri zake,

    kwa sababu ulichinjwa

    na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu

    kutoka kila kabila, kila lugha,

    kila jamaa na kila taifa.

    10 Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani

    wa kumtumikia Mungu wetu,

    nao watatawala duniani.”

    11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. 12 Nao waliimba kwa sauti kuu, wakisema:

    “Anastahili Mwana-Kondoo, yeye aliyechinjwa,

    kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu

    na heshima na utukufu na sifa!”

    13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba:

    “Sifa na heshima na utukufu na uweza

    ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi

    na kwa Mwana-Kondoo,

    milele na milele!”

    14 Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.

  6. 1 Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki;

    kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.

    2 Msifuni Bwana kwa kinubi,

    mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.

    3 Mwimbieni wimbo mpya;

    pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.

    4 Maana neno la Bwana ni haki na kweli,

    ni mwaminifu kwa yote atendayo.

  7. 13 Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu.

  8. 1 Msifuni Bwana.

    Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

    sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

    2 Israeli na washangilie katika Muumba wao,

    watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

    3 Na walisifu jina lake kwa kucheza

    na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

  9. 1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya;

    mwimbieni Bwana dunia yote.

    2 Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake;

    tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

    3 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

    matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

  10. 2 Nikaona kile kilichoonekana kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Kando ya hiyo bahari, walikuwa wamesimama wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake pamoja na tarakimu ya jina lake. Mikononi mwao walikuwa wameshika vinubi walivyopewa na Mungu. 3 Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema:

    “Bwana Mungu Mwenyezi,

    matendo yako ni makuu na ya ajabu.

    Njia zako wewe ni za haki na za kweli,

    Mfalme wa nyakati zote!

    4 Ni nani ambaye hatakuogopa wewe Bwana

    na kulitukuza jina lako?

    Kwa kuwa wewe peke yako ndiwe mtakatifu.

    Mataifa yote yatakuja

    na kuabudu mbele zako,

    kwa kuwa matendo yako ya haki

    yamedhihirishwa.”

  11. 17 Bwana Mungu wako yu pamoja nawe,

    yeye ni mwenye nguvu kuokoa.

    Atakufurahia kwa furaha kubwa,

    atakutuliza kwa pendo lake,

    atakufurahia kwa kuimba.”

  12. 30 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

  13. 5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;

    moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

    6 Nitamwimbia Bwana,

    kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

  14. Zaburi.

    1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

    kwa maana ametenda mambo ya ajabu;

    kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu

    umemfanyia wokovu.

  15. 1 Msifuni Bwana.

    Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,

    jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!

  16. 16 Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.

  17. 33 Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote;

    nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.

    34 Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,

    ninapofurahi katika Bwana.

  18. 26 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

  19. 11 Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. 12 Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta. 13 Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema:

    “Yeye ni mwema;

    upendo wake unadumu milele.”

    Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu, 14 nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu la Mungu.

  20. 25 Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la Bwana wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na Bwana kupitia manabii wake. 26 Hivyo Walawi wakasimama tayari wakiwa na ala za uimbaji za Daudi na makuhani walikuwa na tarumbeta zao.

    27 Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia Bwana pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli. 28 Kusanyiko lote wakaabudu kwa kusujudu, wakati waimbaji wakiwa wanaimba na wenye tarumbeta wakipiga tarumbeta zao. Yote haya yaliendelea mpaka walipomaliza kutoa ile dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa.

    29 Kutoa sadaka kulipomalizika, mfalme na kila mtu aliyekuwepo pamoja naye wakapiga magoti na kuabudu. 30 Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu Bwana kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.

  21. 6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,

    mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.

    7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,

    mwimbieni zaburi za sifa.

  22. 22 Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi

    kwa ajili ya uaminifu wako;

    Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli,

    nitakuimbia sifa kwa zeze.

    23 Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha

    ninapokuimbia sifa,

    mimi, ambaye umenikomboa.

    24 Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki

    mchana kutwa,

    kwa maana wale waliotaka kunidhuru,

    wameaibishwa na kufadhaishwa.

  23. 27 Wakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa kule walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji wakitumia matoazi, vinubi na zeze. 28 Pia waimbaji walikusanywa pamoja kutoka maeneo yaliyozunguka Yerusalemu, kutoka vijiji vya Wanetofathi, 29 kutoka Beth-Gilgali, na kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu.

  24. 16 Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,

    asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;

    kwa maana wewe ndiwe ngome yangu

    na kimbilio langu wakati wa shida.

    17 Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.

    Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

    Mungu unipendaye.

  25. 4 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote,

    ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

    5 mwimbieni Bwana kwa kinubi,

    kwa kinubi na sauti za kuimba,

  26. Zaburi ya shukrani.

    1 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.

    2 Mwabuduni Bwana kwa furaha;

    njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

  27. 14 Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda. 15 Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, na pia nitaomba kwa akili yangu. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia.

  28. 6 Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. 7 Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288. 8 Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.

  29. 11 Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi,

    waimbe kwa shangwe daima.

    Ueneze ulinzi wako juu yao,

    ili wale wapendao jina lako

    wapate kukushangilia.

  30. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu.

    1 Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu;

    mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!

    2 Anzeni wimbo, pigeni matari,

    pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.

  31. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

    1 Nilimngoja Bwana kwa saburi,

    naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

    2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,

    kutoka matope na utelezi;

    akaiweka miguu yangu juu ya mwamba

    na kunipa mahali imara pa kusimama.

    3 Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,

    wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.

    Wengi wataona na kuogopa

    na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

  32. 1 Msifuni Bwana.

    Msifuni Mungu katika patakatifu pake,

    msifuni katika mbingu zake kuu.

    2 Msifuni kwa matendo yake makuu,

    msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

    3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,

    msifuni kwa kinubi na zeze,

    4 msifuni kwa matari na kucheza,

    msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

    5 msifuni kwa matoazi yaliayo,

    msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

  33. 1 Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao. 2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kwa kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao. 3 Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wanne wenye uhai na wale wazee. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. 4 Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni bikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.

  34. 31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

  35. 27 Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi. 28 Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Bwana kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.

  36. 2 Nitafurahi na kushangilia ndani yako.

    Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.

  37. 23 Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,

    kwa maana Bwana amefanya jambo hili.

    Ee vilindi vya dunia, piga kelele.

    Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,

    enyi misitu na miti yenu yote,

    kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo,

    ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.

  38. 13 Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu;

    furahi, ee dunia;

    pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima!

    Kwa maana Bwana anawafariji watu wake,

    naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.

  39. 12 Mtatoka nje kwa furaha

    na kuongozwa kwa amani;

    milima na vilima

    vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu,

    nayo miti yote ya shambani

    itapiga makofi.

  40. 1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:

    2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza,

    wakati watu wanapojitoa

    kwa hiari yao wenyewe:

    mhimidini Bwana!

    3 “Sikieni hili, enyi wafalme!

    Sikilizeni, enyi watawala!

    Nitamwimbia Bwana, nitaimba;

    kwa wimbo nitamhimidi Bwana,

    Mungu wa Israeli.

  41. 33 Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.

  42. 6 Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu Bwana, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko.

    7 Wakalisafirisha Sanduku la Mungu kwa gari jipya la kukokotwa na maksai kutoka nyumba ya Abinadabu, Uza na Ahio wakiliongoza gari hilo. 8 Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.

  43. 19 Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba; 20 Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya alamothi, 21 na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi. 22 Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.

  44. 4 Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake,

    mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu:

    jina lake ni Bwana,

    furahini mbele zake.

    5 Baba wa yatima, mtetezi wa wajane,

    ni Mungu katika makao yake matakatifu.

  45. 7 Mwimbieni Bwana kwa shukrani,

    mpigieni Mungu wetu kinubi.

  46. 9 Pazeni sauti ya nyimbo za furaha pamoja,

    enyi magofu ya Yerusalemu,

    kwa maana Bwana amewafariji watu wake,

    ameikomboa Yerusalemu.

  47. 4 Ninyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu,

    na kujinyoosha juu ya viti vya fahari.

    Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri

    na ndama walionenepeshwa.

    5 Ninyi mnapiga vinubi kama Daudi,

    huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali.

    6 Mnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa,

    na mnajipaka mafuta mazuri,

    lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yosefu.

    7 Kwa hiyo mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kwenda uhamishoni;

    karamu zenu na kustarehe kutakoma.

    8 Bwana Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema:

    “Nachukia kiburi cha Yakobo,

    nachukia ngome zake;

    nitautoa mji wao na kila kitu

    kilichomo ndani mwake.”

  48. 6 Watu walipokuwa wanarudi nyumbani baada ya Daudi kumuua yule Mfilisti, wanawake wakaja kutoka pande zote za miji ya Israeli kumlaki Mfalme Sauli kwa kuimba na kucheza, kwa nyimbo za furaha na kwa matari na zeze.

    7 Walipokuwa wanacheza, wakaimba:

    “Sauli amewaua elfu zake,

    naye Daudi makumi elfu yake.”

  49. 65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.

  50. Utenzi wa Ethani Mwezrahi.

    1 Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele;

    kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako

    ujulikane kwa vizazi vyote.

  51. Zaburi ya Daudi.

    1 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;

    kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.

  52. 1 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,

    wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

    2 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,

    waambieni matendo yake yote ya ajabu.

  53. 9 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,

    kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,

  54. 17 Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake,

    na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.

  55. 4 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;

    lisifuni jina lake takatifu.

  56. 2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,

    ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.

    Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,

    “Bwana amewatendea mambo makuu.”

  57. 5 Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima,

    kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.

  58. 10 waliokombolewa na Bwana watarudi.

    Wataingia Sayuni wakiimba;

    furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.

    Watapata furaha na shangwe;

    huzuni na majonzi vitakimbia.

  59. 10 Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

    sifa zake toka miisho ya dunia,

    ninyi mshukao chini baharini,

    na vyote vilivyomo ndani yake,

    enyi visiwa na wote wakaao ndani yake.

  60. 1 “Imba, ewe mwanamke tasa,

    wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto;

    paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha,

    wewe ambaye kamwe hukupata utungu;

    kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi

    kuliko wa mwanamke mwenye mume,”

    asema Bwana.

  61. 2 Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;

    amekuwa wokovu wangu.

    Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,

    Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.

  62. 4 likiwa na Sanduku la Mungu juu yake, naye Ahio alikuwa anatembea akiwa mbele yake. 5 Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.

  63. 12 Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa au kuonekana humo tangu siku ile.)

  64. 11 Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa Yuda tangu siku ile.)

  65. 21 Waisraeli waliokuwa Yerusalemu wakaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa muda wa siku saba, nao Walawi na makuhani walikuwa wakiimba kila siku, wakiwa na ala za uimbaji za kumsifu Bwana.

  66. 11 Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni,

    tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.

  67. 7 Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,

    utaniepusha na taabu

    na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

  68. 20 Kama vile avuaye mavazi siku ya baridi,

    au kama siki iliyomwagwa juu ya magadi,

    ndivyo alivyo yeye amuimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.

  69. 23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu!

    Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

  70. 19 “Sasa ujiandikie wimbo huu, uwafundishe Waisraeli na uwaamuru wauimbe, ili upate kuwa ushahidi wangu dhidi yao.

  71. 23 Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme, ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.

  72. 6 Bwana asifiwe,

    kwa maana amesikia kilio changu

    nikimwomba anihurumie.

    7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,

    moyo wangu umemtumaini yeye,

    nami nimesaidiwa.

    Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

    nami nitamshukuru kwa wimbo.

  73. 8 Amka, nafsi yangu!

    Amka, kinubi na zeze!

    Nitayaamsha mapambazuko.

    9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;

    nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

  74. 32 Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia,

    mwimbieni Bwana sifa,

  75. 30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,

    nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.

  76. 13 Nitakomesha kelele za nyimbo zako, na uimbaji wako wa kinubi kamwe hautasikika tena.

  77. 32 Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi.