46 Bible Verses About Happiness

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Happiness
  1. 4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 6 Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

    8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. 9 Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

  2. 8 Nimemweka Bwana mbele yangu daima.

    Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

    sitatikisika.

    9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;

    mwili wangu nao utapumzika salama,

    10 kwa maana hutaniacha kaburini,

    wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.

    11 Umenijulisha njia ya uzima;

    utanijaza na furaha mbele zako,

    pamoja na furaha za milele

    katika mkono wako wa kuume.

  3. 12 Wapenzi, msione ajabu kwa yale mateso yanayotukia miongoni mwenu, kana kwamba ni kitu kigeni kinachowapata. 13 Bali furahini kuwa mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili mpate kufurahi zaidi wakati utukufu wake utakapofunuliwa. 14 Kama mkitukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu yenu.

  4. 3 Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema;

    Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

    4 Jifurahishe katika Bwana

    naye atakupa haja za moyo wako.

  5. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.

  6. 13 Heri mtu yule aonaye hekima,

    mtu yule apataye ufahamu,

    14 kwa maana hekima ana faida kuliko fedha

    na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.

    15 Hekima ana thamani kuliko marijani;

    hakuna chochote unachokitamani

    kinachoweza kulinganishwa naye.

    16 Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;

    katika mkono wake wa kushoto

    kuna utajiri na heshima.

    17 Njia zake zinapendeza,

    mapito yake yote ni amani.

    18 Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;

    wale wamshikao watabarikiwa.

  7. 12 Kisha wana wetu wakati wa ujana wao

    watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,

    binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa

    kurembesha jumba la kifalme.

    13 Ghala zetu zitajazwa

    aina zote za mahitaji.

    Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,

    kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;

    14 maksai wetu watakokota

    mizigo mizito.

    Hakutakuwa na kubomoka kuta,

    hakuna kuchukuliwa mateka,

    wala kilio cha taabu

    katika barabara zetu.

    15 Heri watu ambao hili ni kweli;

    heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.

  8. 2 Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 3 kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4 Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.

  9. 9 Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua. 10 Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.

  10. 2 Hakika Mungu ni wokovu wangu;

    nitamtumaini wala sitaogopa.

    Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu;

    amekuwa wokovu wangu.”

    3 Kwa furaha mtachota maji

    kutoka visima vya wokovu.

    4 Katika siku hiyo mtasema:

    “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake;

    julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,

    tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

    5 Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu,

    hili na lijulikane duniani kote.

    6 Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,

    kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”

  11. 9 “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili.

  12. 22 Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,

    bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.

  13. 13 Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke,

    bali maumivu ya moyoni huponda roho.

  14. 13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

  15. 6 Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi. 7 Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa. 8 Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka. 9 Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

  16. Wimbo wa kwenda juu.

    1 Heri ni wale wote wamchao Bwana,

    waendao katika njia zake.

    2 Utakula matunda ya kazi yako;

    baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

  17. 16 Kisha akawaambia mfano huu: “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’

    18 “Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu za nafaka na kujenga nyingine kubwa zaidi na huko nitayahifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Nami nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, unywe, ufurahi.” ’

    20 “Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’

  18. 1 Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 2 ambaye kwa kupitia kwake tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo ndani yake sasa tunasimama, nasi twafurahia katika tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. 3 Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, 4 nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini, 5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

  19. 11 Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote. 12 Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa. 13 Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

  20. 5 Kama mtu ameoa karibuni, kamwe asipelekwe vitani au kupewa wajibu mwingine wowote. Kwa mwaka mmoja atakuwa huru kubaki nyumbani ili amfurahishe mke aliyemwoa.

  21. 17 “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi;

    kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.

  22. 20 Akawatazama wanafunzi wake, akasema:

    “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini,

    kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu.

    21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa,

    kwa sababu mtashibishwa.

    Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa,

    kwa sababu mtacheka.

    22 Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia,

    watakapowatenga na kuwatukana

    na kulikataa jina lenu kama neno ovu,

    kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

    23 “Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.

  23. 26 Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

  24. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

    1 Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako.

    Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake

    kwa ushindi unaompa!

    2 Umempa haja ya moyo wake

    na hukumzuilia maombi ya midomo yake.

    3 Ulimkaribisha kwa baraka tele

    na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

    4 Alikuomba maisha, nawe ukampa,

    wingi wa siku milele na milele.

    5 Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,

    umeweka juu yake fahari na utukufu.

    6 Hakika umempa baraka za milele,

    umemfanya awe na furaha

    kwa shangwe ya uwepo wako.

  25. 13 Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,

    nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.

  26. 1 Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana! Mimi kuwaandikia mambo yale yale hakuniudhi, kwa maana ni kinga kwa ajili yenu.

  27. 15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,

    wanaotembea katika mwanga

    wa uwepo wako, Ee Bwana.

    16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa,

    wanafurahi katika haki yako.

  28. 21 “Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’

  29. 52 Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu.

  30. 6 Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa. 7 Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu chochote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu. 8 Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo.

  31. 13 Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita Asheri.

  32. 9 Ndipo Bwana Mungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako. Bwana atakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako, 10 kama ukimtii Bwana Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.

  33. 4 Ndipo nitakwenda madhabahuni pa Mungu,

    kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu.

    Nitakusifu kwa kinubi,

    Ee Mungu, Mungu wangu.

    5 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?

    Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

    Weka tumaini lako kwa Mungu,

    kwa sababu bado nitamsifu

    Mwokozi wangu na Mungu wangu.

  34. 24 Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,

    tushangilie na kufurahi ndani yake.

  35. 2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,

    ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.

    Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,

    “Bwana amewatendea mambo makuu.”

  36. 10 Ninafurahia sana katika Bwana,

    nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

    Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

    na kunipamba kwa joho la haki,

    kama vile bwana arusi apambavyo

    kichwa chake kama kuhani,

    na kama bibi arusi ajipambavyo

    kwa vito vyake vya thamani.

  37. 10 Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 11 Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.

  38. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 29 Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza.

  39. 22 Je, wewe unayo imani? Ile imani uliyo nayo, uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya. 23 Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, amehukumiwa, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.

  40. 9 Je, tutawezaje kumshukuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu?

  41. 13 Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu.

  42. 8 Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako!

  43. 6 Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye

    kutuonyesha jema lolote?”

    Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.

    7 Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa

    kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.

  44. 5 Wapandao kwa machozi

    watavuna kwa nyimbo za shangwe.

  45. 1 Nikafikiri moyoni mwangu, “Haya basi, nitakujaribu kwa anasa nione ni lipi lililo jema.” Lakini hilo nalo likaonekana ni ubatili.

  46. 19 Kwa maana tumaini letu ni nini, au furaha yetu au taji yetu ya kujisifia mbele za Bwana Yesu Kristo wakati wa kuja kwake? Je, si ni ninyi? 20 Naam, ninyi ndio fahari yetu na furaha yetu.