26 Bible Verses About Laughter
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)
-
1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,
na kabila za watu kula njama bure?
2 Wafalme wa dunia wanajipanga
na watawala wanajikusanya pamoja
dhidi ya Bwana
na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao
na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
4 Yeye atawalaye mbinguni hucheka,
Bwana huwadharau.
5 Kisha huwakemea katika hasira yake
na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
6 “Nimemtawaza Mfalme wangu
juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
7 Nitatangaza amri ya Bwana:
Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu,
leo mimi nimekuzaa.
8 Niombe, nami nitayafanya mataifa
kuwa urithi wako,
miisho ya dunia kuwa milki yako.
-
12 Waovu hula njama dhidi ya wenye haki
na kuwasagia meno,
13 bali Bwana huwacheka waovu,
kwa sababu anajua siku yao inakuja.
-
1 Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 3 Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 4 Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 5 Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.
6 Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” 7 Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.”
-
22 Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,
bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
-
10 Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.”
Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake. 11 Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12 Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?”
13 Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ 14 Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.”
15 Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.”
Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”
-
2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,
ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.
Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,
“Bwana amewatendea mambo makuu.”
3 Bwana ametutendea mambo makuu,
nasi tumejaa furaha.
-
20 “Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia,
wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.
21 Bado atakijaza kinywa chako na kicheko,
na midomo yako na kelele za shangwe.
-
1 Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo,
nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:
2 wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,
wakati wa kupanda na wakati wa kungʼoa yaliyopandwa,
3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya,
wakati wa kubomoa,
na wakati wa kujenga,
4 wakati wa kulia na wakati wa kucheka,
wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza,
-
24 Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita
na hakuna yeyote aliyekubali
niliponyoosha mkono wangu,
25 kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
na hamkukubali karipio langu,
26 mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
nitawadhihaki wakati janga litawapata:
27 wakati janga litawapata kama tufani,
wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,
wakati dhiki na taabu zitawalemea.
28 “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
watanitafuta lakini hawatanipata.
-
21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa,
kwa sababu mtashibishwa.
Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa,
kwa sababu mtacheka.
-
13 Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,
nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
-
13 Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke,
bali maumivu ya moyoni huponda roho.
14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa,
bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.
15 Siku zote za wanaoonewa ni za taabu,
bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.
16 Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana,
kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.
17 Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo
kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.
-
25 Amevikwa nguvu na heshima,
anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.
-
7 Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao,
hutema upanga kutoka midomo yao,
nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”
8 Lakini wewe, Bwana, uwacheke;
unayadharau mataifa hayo yote.
-
6 Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria,
ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.
Hili nalo pia ni ubatili.
-
25 Ole wenu ninyi mlioshiba sasa,
maana mtaona njaa.
Ole wenu ninyi mnaocheka sasa,
maana mtaomboleza na kulia.
-
2 Nikasema, “Kicheko nacho ni upumbavu. Nayo matokeo ya anasa ni nini?”
-
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.
-
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko,
kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo.
-
10 Wanawabeza wafalme,
na kuwadhihaki watawala.
Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma;
wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.
-
22 Utayacheka maangamizo na njaa,
wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa
wanyama wakali wa mwituni.
-
4 “Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu,
ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu:
mimi ni mtu wa kuchekwa tu,
ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!
-
23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele, 24 akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka.
-
25 Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa wakasema, “Mleteni Samsoni aje acheze ili tufurahi.” Basi wakamleta Samsoni kutoka mle gerezani naye akacheza mbele yao.
Wakamweka kati ya nguzo mbili.
-
27 Wakati wa adhuhuri, Eliya akaanza kuwadhihaki, akisema, “Pigeni kelele zaidi! Hakika yeye ni mungu! Labda amezama katika mawazo mazito, au ana shughuli nyingi, au amesafiri. Labda amelala usingizi mzito, naye ni lazima aamshwe.”
-
7 Ee Bwana, umenidanganya,
nami nikadanganyika;
wewe una nguvu kuniliko,
nawe umenishinda.
Ninadharauliwa mchana kutwa,
kila mmoja ananidhihaki.
Shows Read in context, Share and Copy.