84 Bible Verses About Morning

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Morning
  1. 2 Sikiliza kilio changu ili unisaidie,

    Mfalme wangu na Mungu wangu,

    kwa maana kwako ninaomba.

    3 Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana;

    asubuhi naleta haja zangu mbele zako,

    na kusubiri kwa matumaini.

    4 Wewe si Mungu unayefurahia uovu,

    kwako mtu mwovu hataishi.

    5 Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,

    unawachukia wote watendao mabaya.

    6 Unawaangamiza wasemao uongo.

    Bwana huwachukia

    wamwagao damu na wadanganyifu.

    7 Lakini mimi, kwa rehema zako kuu,

    nitakuja katika nyumba yako,

    kwa unyenyekevu, nitasujudu

    kuelekea Hekalu lako takatifu.

    8 Niongoze katika haki yako, Ee Bwana,

    kwa sababu ya adui zangu,

    nyoosha njia yako mbele yangu.

  2. 21 Hata hivyo najikumbusha neno hili

    na kwa hiyo ninalo tumaini.

    22 Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,

    kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

    23 Ni mpya kila asubuhi,

    uaminifu wako ni mkuu.

    24 Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu,

    kwa hiyo nitamngojea.”

  3. Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.

    1 Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,

    kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,

    na hukuacha adui zangu

    washangilie juu yangu.

    2 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie

    na wewe umeniponya.

    3 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,

    umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

    4 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;

    lisifuni jina lake takatifu.

    5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

    bali upendo wake hudumu siku zote.

    Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

    lakini asubuhi kukawa na furaha.

  4. 8 Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,

    kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.

    Nionyeshe njia nitakayoiendea,

    kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu.

    9 Ee Bwana, uniokoe na adui zangu,

    kwa kuwa nimejificha kwako.

    10 Nifundishe kufanya mapenzi yako,

    kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu,

    Roho wako mwema na aniongoze

    katika nchi tambarare.

  5. 16 “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi ingʼaayo.”

  6. 35 Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Yesu akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta, 37 nao walipomwona, wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta!”

    38 Yesu akawajibu, “Twendeni mahali pengine kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia, kwa sababu hicho ndicho nilichokuja kukifanya.” 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya kote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu.

  7. 16 Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,

    asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;

    kwa maana wewe ndiwe ngome yangu

    na kimbilio langu wakati wa shida.

    17 Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.

    Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

    Mungu unipendaye.

  8. 12 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

    ili tujipatie moyo wa hekima.

    13 Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini?

    Wahurumie watumishi wako.

    14 Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma,

    ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.

    15 Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu,

    kulingana na miaka tuliyotaabika.

    16 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,

    utukufu wako kwa watoto wao.

    17 Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu;

    uzithibitishe kazi za mikono yetu:

    naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu.

  9. 76 “Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana;

    kwa kuwa utamtangulia Bwana

    na kuandaa njia kwa ajili yake,

    77 kuwajulisha watu wake juu ya wokovu

    utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

    78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu,

    nuru itokayo juu itatuzukia

    79 ili kuwaangazia wale waishio gizani

    na katika uvuli wa mauti,

    kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”

    80 Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli.

  10. 12 “Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,

    au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,

    13 yapate kushika miisho ya dunia,

    na kuwakungʼuta waovu waliomo?

  11. 26 “Atakayeshinda na kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa:

    27 “ ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma,

    atawavunja vipande vipande

    kama chombo cha udongo’:

    kama vile mimi nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu. 28 Nami nitampa pia ile nyota ya asubuhi.

  12. 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. 2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

    3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 4 Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

  13. 19 Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyongʼaa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu. 20 Zaidi ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe.

  14. 13 Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie;

    asubuhi maombi yangu huja mbele zako.

  15. 4 “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?

    Niambie, kama unafahamu.

    5 Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake?

    Hakika wewe unajua!

    Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

    6 Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini,

    au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,

    7 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,

    na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?

  16. 24 Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,

    tushangilie na kufurahi ndani yake.

  17. 4 Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa,

    ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka.

    Huniamsha asubuhi kwa asubuhi,

    huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.

    5 Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu,

    nami sikuwa mwasi,

    wala sikurudi nyuma.

  18. 3 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia.

  19. 16 Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, “Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.” 17 Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni.”

    18 Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake. 19 Mahali pale akapaita Betheli, ingawa mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

  20. 8 Wale wanaoishi mbali sana

    wanaogopa maajabu yako,

    kule asubuhi ipambazukiapo

    na kule jioni inakofifilia

    umeziita nyimbo za furaha.

  21. 147 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;

    nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  22. 5 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,

    katika neno lake naweka tumaini langu.

    6 Nafsi yangu inamngojea Bwana

    kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,

    naam, kuliko walinzi

    waingojeavyo asubuhi.

    7 Ee Israeli, mtumaini Bwana,

    maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,

    na kwake kuna ukombozi kamili.

    8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli

    kutoka dhambi zao zote.

  23. 38 “Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. 39 Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. 40 Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.

  24. 6 Panda mbegu yako asubuhi,

    nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee,

    kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa,

    kwamba ni hii au ni ile,

    au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.

  25. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 29 Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza.

    31 Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu? 32 Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye?

  26. 8 Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

  27. 27 Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Abrahamu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za Bwana. 28 Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.

  28. 13 Siku iliyofuata, Mose akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. 14 Baba mkwe wake alipoona yote Mose anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi mpaka jioni?”

  29. 4 “Nifanye nini nawe, Efraimu?

    Nifanye nini nawe, Yuda?

    Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,

    kama umande wa alfajiri utowekao.

  30. 1 Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Yesu na kumjaribu kwa kumwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

    2 Yesu akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’ 3 Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati. 4 Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.

  31. 2 Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. 3 Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ngʼombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”

    4 Kwa hiyo Mose akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama Bwana alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake.

  32. 1 Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi:

    “Neno la Daudi mwana wa Yese,

    neno la mtu aliyeinuliwa na Aliye Juu Sana,

    mtu aliyepakwa mafuta na Mungu wa Yakobo,

    mwimbaji wa nyimbo wa Israeli:

    2 “Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu,

    neno lake lilikuwa ulimini mwangu.

    3 Mungu wa Israeli alinena,

    mwamba wa Israeli akaniambia:

    ‘Mtu anatawala watu kwa haki,

    wakati anapotawala

    akiwa na hofu ya Mungu,

    4 yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo

    asubuhi isiyo na mawingu,

    kama mwanga baada ya mvua

    uchipuzao majani kutoka ardhini.’

    5 “Je, si hivyo ilivyo nyumba yangu

    mbele za Mungu?

    Je, hajafanya Agano la milele nami,

    lililopangwa na kuimarishwa

    kila sehemu?

    Je, hatanifanya niufurahie wokovu wangu

    na kunijalia matakwa yangu yote?

    6 Lakini watu waovu wote

    watatupwa kando kama miiba,

    ambayo haikusanywi kwa mkono.

    7 Yeyote agusaye miiba

    hutumia chombo cha chuma

    au mpini wa mkuki,

    nayo huchomwa pale ilipo.”

  33. 12 Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,

    ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko!

    Umetupwa chini duniani,

    wewe uliyepata kuangusha mataifa!

  34. 12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo Bwana asemalo:

    “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi,

    mwokoeni mikononi mwa mdhalimu

    yeye aliyetekwa nyara,

    la sivyo ghadhabu yangu italipuka

    na kuwaka kama moto

    kwa sababu ya uovu mlioufanya:

    itawaka na hakuna wa kuizima.

  35. 1 “Kwa maana Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri ili kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu.

  36. 1 Sabato ilipomalizika, Maria Magdalene, Maria mama yake Yakobo, na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. 2 Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma, mara tu baada ya kuchomoza jua, walikwenda kaburini. 3 Njiani wakawa wanaulizana wao kwa wao, “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe kutoka kwenye ingilio la kaburi?”

    4 Lakini walipotazama, wakaona lile jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha kuvingirishwa kutoka pale penye ingilio la kaburi. 5 Walipokuwa wakiingia mle kaburini, wakamwona kijana mmoja aliyevaa joho jeupe akiwa ameketi upande wa kuume, nao wakastaajabu.

    6 Yule malaika akawaambia, “Msistaajabu. Mnamtafuta Yesu, Mnazareti, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza. 7 Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro, kwamba, ‘Anawatangulia kwenda Galilaya. Huko ndiko mtamwona, kama alivyowaambia.’ ”

    8 Hivyo wakatoka, wakakimbia kutoka mle kaburini wakiwa na hofu kuu na mshangao. Nao hawakumwambia mtu yeyote neno lolote, kwa sababu waliogopa.

  37. 26 Kwa hiyo wakamchukua yule fahali waliyepewa, nao wakamwandaa.

    Kisha wakaliitia jina la Baali kutoka asubuhi hadi adhuhuri, wakapiga kelele, “Ee Baali, utujibu!” Lakini hapakuwa na jibu; hakuna aliyejibu. Nao wakacheza kuizunguka madhabahu waliyoijenga.

  38. Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.

    1 Ni vyema kumshukuru Bwana

    na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

    2 kuutangaza upendo wako asubuhi,

    na uaminifu wako wakati wa usiku,

    3 kwa zeze yenye nyuzi kumi

    na kwa sauti ya kinubi.

  39. 2 Ee Bwana, uturehemu,

    tunakutamani.

    Uwe nguvu yetu kila asubuhi

    na wokovu wetu wakati wa taabu.

  40. 1 Yoshua na Waisraeli wote wakaondoka asubuhi na mapema kutoka Shitimu, wakaenda mpaka Mto Yordani, ambako walipiga kambi kabla ya kuvuka.

  41. 4 Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.

  42. 4 Nionyeshe njia zako, Ee Bwana,

    nifundishe mapito yako,

    5 niongoze katika kweli yako na kunifundisha,

    kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,

    nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

  43. 7 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;

    nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

    8 Amka, nafsi yangu!

    Amka, kinubi na zeze!

    Nitayaamsha mapambazuko.

    9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;

    nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

    10 Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni,

    uaminifu wako unazifikia anga.

  44. 2 Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.

  45. 8 Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana.

  46. 25 Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, sivyo? Kwa nini umenidanganya?”

  47. 55 Kesho yake asubuhi na mapema, Labani akawabusu wajukuu zake, binti zake na kuwabariki. Kisha akaondoka, akarudi nyumbani.

  48. 20 Kisha Bwana akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndilo Bwana asemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.

  49. 13 Kisha Bwana akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu,

  50. 13 “ ‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, utaitoa kila siku asubuhi. 14 Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa Bwana ni amri ya daima. 15 Kwa hiyo mwana-kondoo na sadaka ya nafaka na mafuta vitatolewa kila siku asubuhi kwa ajili ya sadaka ya daima ya kuteketezwa.

  51. 34 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.

  52. 1 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Yesu ili kumuua.

  53. 23 Baada ya kupanga siku ya kuonana naye, watu wengi wakaja kuanzia asubuhi hadi jioni akawaeleza na kutangaza kuhusu Ufalme wa Mungu akijaribu kuwahadithia juu ya Yesu kutoka Sheria ya Mose na kutoka Manabii. 24 Baadhi wakasadiki yale aliyosema, lakini wengine hawakuamini. 25 Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho Mtakatifu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:

    26 “ ‘Nenda kwa watu hawa na useme,

    “Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

    na pia mtatazama, lakini hamtaona.”

    27 Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

    hawasikii kwa masikio yao,

    na wamefumba macho yao.

    Wasije wakaona kwa macho yao,

    na wakasikiliza kwa masikio yao,

    wakaelewa kwa mioyo yao,

    na kugeuka nami nikawaponya.’

  54. 13 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu.

  55. 19 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne.

  56. 8 Asubuhi yake, alifadhaika akilini, hivyo akawaita waaguzi wote pamoja na watu wenye busara wa Misri. Walipokuja, Farao akawaeleza ndoto zake, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumfasiria.

  57. 15 Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka.

  58. 7 kisha asubuhi mtauona utukufu wa Bwana, kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani hata mtunungʼunikie?” 8 Pia Mose akasema, “Mtajua kuwa alikuwa Bwana wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnungʼuniki dhidi yetu, bali dhidi ya Bwana.”

  59. 21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za Bwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.

  60. 21 Wakati mwingine wingu lilikuwepo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wowote wingu lilipoinuka, waliondoka.

  61. 10 Asubuhi na mapema siku iliyofuatia, Yoshua akawakutanisha watu wake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawa mbele ya watu kwenda Ai. 11 Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini mwa Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji. 12 Yoshua alikuwa amewachukua watu wapatao elfu tano, akawaweka katika uavizi kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa mji. 13 Wakawaweka askari katika maeneo yao: wale wote waliokuwa kambini wakawa kaskazini ya mji na wale waliokuwa wakivizia wakawa upande wa magharibi. Usiku huo Yoshua akaenda katika lile bonde.

    14 Mfalme wa Ai alipoona jambo hili, yeye pamoja na watu wote wa mji wakatoka kwa haraka asubuhi na mapema, ili kukutana na Israeli katika vita mahali fulani panapotazamana na Araba. Lakini hakujua kwamba kulikuwa kumewekwa waviziaji dhidi yake nyuma ya mji.

  62. 5 Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu.

  63. 9 Nyota zake za alfajiri na ziwe giza;

    nao ungojee mwanga bila mafanikio,

    wala usiuone mwonzi wa kwanza

    wa mapambazuko,

  64. 17 Jioni, asubuhi na adhuhuri

    ninalia kwa huzuni,

    naye husikia sauti yangu.

    18 Huniokoa nikawa salama katika vita

    vilivyopangwa dhidi yangu,

    ingawa watu wengi hunipinga.

  65. 8 Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko

    na uponyaji wako utatokea upesi;

    ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,

    na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.

  66. 16 Furahini siku zote; 17 ombeni bila kukoma; 18 shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

  67. 15 Kunako mapambazuko, malaika wakamhimiza Loti, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”

  68. 31 Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani.

  69. 21 Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka.

  70. 3 Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi.

  71. 12 Moto ulio juu ya madhabahu lazima uwe unaendelea kuwaka, kamwe usizimike. Kila asubuhi kuhani ataongeza kuni na kupanga sadaka ya kuteketezwa juu ya moto, na kuteketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake.

  72. 5 Kisha akamwambia Kora na wafuasi wake wote: “Asubuhi Bwana ataonyesha ni nani aliye wake na ni nani aliye mtakatifu, tena atamtaka mtu huyo aje kwake. Mtu yule ambaye atamchagua atamfanya kuja karibu naye.

  73. 21 Balaamu akaamka asubuhi, akatandika punda wake akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.

  74. 15 Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakauzunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba.

  75. 14 “ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaa Bwana litakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaoutwaa Bwana utakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakuja mbele mtu kwa mtu.

  76. 28 Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa na yule ngʼombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu yaliyojengwa upya!

  77. 20 Asubuhi na mapema Daudi akaondoka, akaliacha kundi la kondoo pamoja na mchungaji, akapakia vitu vile na kuondoka, kama vile Yese alivyokuwa amemwagiza. Akafika kambini wakati jeshi lilikuwa likitoka kwenda kwenye sehemu yake ya kupigania, huku wakipiga kelele za vita.

  78. 18 Akipiga chafya mwanga humetameta;

    macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.

  79. 10 Siku moja katika nyua zako ni bora

    kuliko siku elfu mahali pengine;

    afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu

    kuliko kukaa katika mahema ya waovu.

    11 Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao,

    Bwana hutoa wema na heshima;

    hakuna kitu chema anachowanyima

    wale ambao hawana hatia.

  80. 11 Ee Bwana, nifundishe njia yako,

    nami nitakwenda katika kweli yako;

    nipe moyo usiositasita,

    ili niweze kulicha jina lako.

    12 Ee Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote;

    nitaliadhimisha jina lako milele.

    13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;

    umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi.

  81. 5 Bwana aliye ndani yake ni mwenye haki,

    hafanyi kosa.

    Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake,

    kila kukipambazuka huitimiza,

    bali mtu dhalimu hana aibu.

  82. 18 Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale askari kuhusu yaliyomtukia Petro.

  83. 12 Usiku umeendelea sana, mapambazuko yamekaribia. Kwa hiyo tuyaweke kando matendo ya giza na tuvae silaha za nuru.

  84. 13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.