39 Bible Verses About Waiting

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Waiting
  1. Zaburi ya Daudi.

    1 Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu,

    wala usiwaonee wivu watendao mabaya,

    2 kwa maana kama majani watanyauka mara,

    kama mimea ya kijani watakufa mara.

    3 Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema;

    Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

    4 Jifurahishe katika Bwana

    naye atakupa haja za moyo wako.

    5 Mkabidhi Bwana njia yako,

    mtumaini yeye, naye atatenda hili:

    6 Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko,

    na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.

    7 Tulia mbele za Bwana

    na umngojee kwa uvumilivu;

    usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,

    wanapotekeleza mipango yao miovu.

    8 Epuka hasira na uache ghadhabu,

    usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.

    9 Kwa maana waovu watakatiliwa mbali,

    bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.

  2. 18 Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19 Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu. 20 Kwa kuwa viumbe vyote viliwekwa chini ya ubatili, si kwa chaguo lao, bali kwa mapenzi yake yeye aliyevitiisha katika tumaini, 21 ili kwamba viumbe vyote vipate kuwekwa huru kutoka kwa utumwa wa kuharibika na kupewa uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.

    22 Kwa maana twajua ya kuwa hata sasa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa maumivu kama utungu wa mwanamke wakati wa kuzaa. 23 Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu. 24 Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alicho nacho tayari? 25 Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatuna, basi twakingojea kwa saburi.

  3. 13 Nami bado nina tumaini hili:

    nitauona wema wa Bwana

    katika nchi ya walio hai.

    14 Mngojee Bwana,

    uwe hodari na mwenye moyo mkuu,

    nawe, umngojee Bwana.

  4. 5 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,

    katika neno lake naweka tumaini langu.

    6 Nafsi yangu inamngojea Bwana

    kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,

    naam, kuliko walinzi

    waingojeavyo asubuhi.

    7 Ee Israeli, mtumaini Bwana,

    maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,

    na kwake kuna ukombozi kamili.

    8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli

    kutoka dhambi zao zote.

  5. 22 Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,

    kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

    23 Ni mpya kila asubuhi,

    uaminifu wako ni mkuu.

    24 Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu,

    kwa hiyo nitamngojea.”

    25 Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,

    kwa yule ambaye humtafuta;

    26 ni vyema kungojea kwa utulivu

    kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

  6. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

    1 Nilimngoja Bwana kwa saburi,

    naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

  7. 5 Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,

    tumaini langu latoka kwake.

    6 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;

    ndiye ngome yangu, sitatikisika.

    7 Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,

    ndiye mwamba wangu wenye nguvu

    na kimbilio langu.

    8 Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote,

    miminieni mioyo yenu kwake,

    kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

  8. 35 “Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, 36 kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka kwenye karamu ya arusi, ili ajapo na kubisha mlango waweze kumfungulia mara. 37 Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia. 38 Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja mnamo usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. 39 Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angalijua saa mwizi atakuja, asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 40 Ninyi nanyi hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.”

  9. 27 Kwa nini unasema, ee Yakobo,

    nanyi ee Israeli, kulalamika,

    “Njia yangu imefichwa Bwana asiione,

    Mungu wangu hajali shauri langu?”

    28 Je wewe, hufahamu?

    Je wewe, hujasikia?

    Bwana ni Mungu wa milele,

    Muumba wa miisho ya dunia.

    Hatachoka wala kulegea,

    wala hakuna hata mmoja

    awezaye kuupima ufahamu wake.

    29 Huwapa nguvu waliolegea

    na huongeza nguvu za wadhaifu.

    30 Hata vijana huchoka na kulegea,

    nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

    31 bali wale wamtumainio Bwana

    atafanya upya nguvu zao.

    Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

    watapiga mbio wala hawatachoka,

    watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

  10. 18 “Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.

  11. 6 Wenye haki wataona na kuogopa,

    watamcheka, wakisema,

    7 “Huyu ni yule mtu ambaye

    hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,

    bali alitumainia wingi wa utajiri wake,

    na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

    8 Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni

    unaostawi katika nyumba ya Mungu,

    nautegemea upendo wa Mungu usiokoma

    milele na milele.

    9 Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,

    nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.

    Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.

  12. 22 Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!”

    Mngojee Bwana, naye atakuokoa.

  13. 5 niongoze katika kweli yako na kunifundisha,

    kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,

    nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

  14. 4 Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. 5 Yohana aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

  15. 1 Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.

    2 Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote. 3 Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 4 Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5 Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki. 6 Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

  16. 20 Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini,

    yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

  17. 7 Juu ya mlima huu ataharibu

    sitara ihifadhiyo mataifa yote,

    kile kifuniko kifunikacho mataifa yote,

    8 yeye atameza mauti milele.

    Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;

    ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.

    Bwana amesema hili.

    9 Katika siku ile watasema,

    “Hakika huyu ndiye Mungu wetu;

    tulimtumaini, naye akatuokoa.

    Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini;

    sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”

  18. 18 Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema,

    anainuka ili kuwaonyesha huruma.

    Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki.

    Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

  19. 6 Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;

    dumisha upendo na haki,

    nawe umngojee Mungu wako siku zote.

  20. 18 Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho. 19 Baada ya kufanywa hai, alikwenda na kuzihubiria roho zilizokuwa kifungoni: 20 roho hizo ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Noa, wakati wa kujenga safina, ambamo watu wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa ili wasiangamie kwa gharika.

  21. 2 Ee Bwana, uturehemu,

    tunakutamani.

    Uwe nguvu yetu kila asubuhi

    na wokovu wetu wakati wa taabu.

  22. 16 Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia juu ya shauri hilo baya, alikwenda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.

    17 Ndipo Paulo akamwita mmoja wa viongozi wa askari, akamwambia, “Mpeleke huyu kijana kwa jemadari, analo jambo la kumweleza.” 18 Hivyo yule kiongozi wa askari akampeleka yule kijana kwa jemadari, akamwambia, “Paulo yule mfungwa aliniita na kuniomba nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukueleza.”

    19 Yule jemadari akamshika yule kijana mkono, akampeleka kando na kumuuliza, “Unataka kuniambia nini?”

    20 Yule kijana akasema, “Wayahudi wamekubaliana wakuombe umpeleke Paulo kwenye baraza lao kesho kwa kisingizio kwamba wanataka kufanya uchunguzi wa kina wa shauri lake. 21 Lakini usishawishiwe nao kwa maana zaidi ya watu arobaini wanamvizia. Wamejifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wawe wamemuua Paulo. Sasa wako tayari, wanangoja idhini yako kwa ajili ya ombi lao.”

  23. 3 Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea

    atakayeaibishwa,

    bali wataaibishwa

    wafanyao hila bila sababu.

  24. 7 “Lakini sasa Bwana, nitafute nini?

    Tumaini langu ni kwako.

    8 Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote,

    usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.

  25. 14 Bwana huwategemeza wote waangukao,

    na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.

    15 Macho yao wote yanakutazama wewe,

    nawe huwapa chakula chao wakati wake.

    16 Waufumbua mkono wako,

    watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

  26. 7 Mapito ya wenye haki yamenyooka.

    Ewe uliye Mwenye Haki,

    waisawazisha njia ya mtu mnyofu.

    8 Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako,

    twakungojea wewe,

    jina lako na sifa zako

    ndizo shauku za mioyo yetu.

    9 Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku,

    wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku.

    Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia,

    watu wa ulimwengu hujifunza haki.

  27. 4 Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia,

    hakuna sikio lililotambua,

    hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe,

    anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao.

  28. 33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane. 34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa.

    Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.

  29. 34 Mngojee Bwana,

    na uishike njia yake.

    Naye atakutukuza uirithi nchi,

    waovu watakapokatiliwa mbali,

    utaliona hilo.

  30. 13 Lakini mara walisahau aliyowatendea,

    wala hawakungojea shauri lake.

    14 Jangwani walitawaliwa na tamaa zao,

    walimjaribu Mungu nyikani.

    15 Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba,

    lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.

  31. 23 Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea,

    na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea.

    Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi;

    wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako.

    Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana;

    wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”

  32. 3 Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika;

    unazungumzia mambo ya mwisho,

    na kamwe hautakosea.

    Iwapo utakawia, wewe usubiri;

    kwa hakika utakuja na hautachelewa.

  33. 8 Bwana anasema,

    “Kwa hiyo ningojee mimi,

    siku nitakayosimama kuteka nyara.

    Nimeamua kukusanya mataifa,

    kukusanya falme

    na kumimina ghadhabu yangu juu yao,

    hasira yangu kali yote.

    Dunia yote itateketezwa

    kwa moto wa wivu wa hasira yangu.

  34. 16 Paulo alipokuwa akiwasubiri huko Athene, alisumbuka sana moyoni mwake kuona vile mji huo ulivyojaa sanamu. 17 Hivyo akahojiana kwenye sinagogi na Wayahudi pamoja na Wayunani waliomcha Mungu, na pia sokoni kila siku na watu aliopatana nao huko.

  35. 7 Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. 8 Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.

  36. 3 Nimechoka kwa kuomba msaada,

    koo langu limekauka.

    Macho yangu yanafifia,

    nikimtafuta Mungu wangu.

  37. 7 Lakini mimi, namtazama Bwana kwa matumaini,

    namngoja Mungu Mwokozi wangu;

    Mungu wangu atanisikia mimi.

  38. 20 Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Yesu Kristo, 21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote chini yake.

  39. 27 Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu, 28 vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.