56 Bible Verses About Thankfulness

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Thankfulness
  1. 16 Furahini siku zote; 17 ombeni bila kukoma; 18 shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

  2. 15 Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. 17 Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.

  3. 18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

    21 Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.

  4. Zaburi ya shukrani.

    1 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.

    2 Mwabuduni Bwana kwa furaha;

    njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

    3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.

    Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;

    sisi tu watu wake,

    kondoo wa malisho yake.

    4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

    na katika nyua zake kwa kusifu,

    mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

    5 Kwa maana Bwana ni mwema

    na upendo wake wadumu milele;

    uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

  5. 4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 6 Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

    8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

  6. 1 Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha;

    tumfanyie kelele za shangwe

    Mwamba wa wokovu wetu.

    2 Tuje mbele zake kwa shukrani,

    tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

    3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,

    mfalme mkuu juu ya miungu yote.

  7. 10 Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. 11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

    12 Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu. 13 Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote. 14 Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu. 15 Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

  8. 53 Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa. 54 Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

    55 “Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako?

    Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

    56 Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

  9. 2 Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. 3 Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.

  10. 34 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

    upendo wake wadumu milele.

    35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.

    Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa,

    ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,

    na kushangilia katika sifa zako.”

  11. Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.

    1 Ni vyema kumshukuru Bwana

    na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

    2 kuutangaza upendo wako asubuhi,

    na uaminifu wako wakati wa usiku,

    3 kwa zeze yenye nyuzi kumi

    na kwa sauti ya kinubi.

  12. 6 Hivyo basi, kama vile mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kukaa ndani yake, 7 mkiwa na mizizi, na mmejengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.

  13. 1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.

    Fadhili zake zadumu milele.

    2 Mshukuruni Mungu wa miungu.

    Fadhili zake zadumu milele.

    3 Mshukuruni Bwana wa mabwana:

    Fadhili zake zadumu milele.

  14. 30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,

    nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.

    31 Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume,

    zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.

  15. 1 Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 2 kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 3 Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, 4 anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli.

  16. 1 Msifuni Bwana.

    Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

    upendo wake wadumu milele.

    2 Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana

    au kutangaza kikamilifu sifa zake?

  17. Zaburi ya Daudi.

    1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

    Vyote vilivyomo ndani yangu

    vilihimidi jina lake takatifu.

    2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,

    wala usisahau wema wake wote,

    3 akusamehe dhambi zako zote,

    akuponya magonjwa yako yote,

    4 aukomboa uhai wako na kaburi,

    akuvika taji ya upendo na huruma,

    5 atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,

    ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.

  18. 10 Basi Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alikwenda nyumbani kwenye chumba chake cha ghorofani ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Akapiga magoti na kuomba mara tatu kwa siku, akimshukuru Mungu wake kama alivyokuwa akifanya mwanzoni.

  19. 2 Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima. 3 Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Yesu Kristo.

  20. 18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,

    nitakusifu katikati ya watu wengi.

  21. 8 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

    na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,

    9 kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu,

    na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.

  22. 3 Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi, 4 kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote: 5 imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili 6 iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote. 7 Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu, 8 ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.

    9 Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu. 10 Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu, 11 mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha 12 mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. 13 Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa, 14 ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.

  23. 7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,

    moyo wangu umemtumaini yeye,

    nami nimesaidiwa.

    Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

    nami nitamshukuru kwa wimbo.

  24. Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.

    1 Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,

    kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,

    na hukuacha adui zangu

    washangilie juu yangu.

    2 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie

    na wewe umeniponya.

    3 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,

    umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

    4 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;

    lisifuni jina lake takatifu.

    5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

    bali upendo wake hudumu siku zote.

    Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

    lakini asubuhi kukawa na furaha.

  25. 21 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

    na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

    22 Na watoe dhabihu za kushukuru,

    na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.

  26. 8 Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote.

  27. 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16 Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

    17 Yesu akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?” 19 Yesu akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.”

  28. 16 Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, 17 wakisema:

    “Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi,

    uliyeko na uliyekuwako,

    kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu

    na ukaanza kutawala.

    18 Mataifa walikasirika nao

    wakati wa ghadhabu yako umewadia.

    Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa

    na kuwapa thawabu watumishi wako manabii

    na watakatifu wako pamoja na wale wote

    wanaoliheshimu Jina lako,

    wakubwa kwa wadogo:

    na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”

  29. 11 Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,

    na utukufu na enzi na uzuri,

    kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

    ni chako wewe.

    Ee Bwana, ufalme ni wako;

    umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

    12 Utajiri na heshima vyatoka kwako;

    wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.

    Mikononi mwako kuna nguvu na uweza

    ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

    13 Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru

    na kulisifu Jina lako tukufu.

  30. 11 Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.

  31. 15 Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.

    16 Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

  32. 3 Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka. 4 Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.

  33. 12 Namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona mwaminifu, akaniteua kwa kazi yake. 13 Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu. 14 Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.

  34. 10 Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la Bwana, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumtukuza Bwana, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli. 11 Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa Bwana hivi:

    “Yeye ni mwema;

    upendo wake kwa Israeli

    wadumu milele.”

    Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana ulikuwa umewekwa.

  35. 11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,

    ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

    12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.

    Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

  36. 1 Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao, 2 mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.

    3 Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. 4 Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.

  37. 17 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru

    na kuliita jina la Bwana.

  38. 62 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru

    kwa sababu ya sheria zako za haki.

  39. 19 Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu,

    ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.

    20 Mungu wetu ni Mungu aokoaye,

    Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo.

  40. 1 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,

    wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

    2 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,

    waambieni matendo yake yote ya ajabu.

  41. 1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

    upendo wake wadumu milele.

  42. 25 Wakati huo Yesu alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. 26 Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

  43. 11 Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, 12 wakisema:

    “Amen!

    Sifa na utukufu

    na hekima na shukrani na heshima

    na uweza na nguvu

    viwe kwa Mungu wetu milele na milele.

    Amen!”

  44. 20 Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. 21 Miriamu akawaimbia:

    “Mwimbieni Bwana,

    kwa maana ametukuka sana.

    Farasi na mpanda farasi

    amewatosa baharini.”

    22 Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji.

  45. 26 Mshukuruni Mungu wa mbinguni,

    Fadhili zake zadumu milele.

  46. 9 Yesu akatoa mfano huu kwa wale waliojiamini kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine: 10 “Watu wawili walikwenda Hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 Yule Farisayo, akasimama, akasali hivi na kuomba kwake mwenyewe: ‘Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine ambao ni wanyangʼanyi, wadhalimu, na wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma, na natoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’

    13 “Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipigapiga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

    14 “Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana yeyote ajikwezaye atashushwa, na yeyote ajishushaye atakwezwa.”

  47. 1 Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. 2 Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, 3 wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, 4 wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu: 5 wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.

  48. 11 Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. 12 Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta. 13 Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema:

    “Yeye ni mwema;

    upendo wake unadumu milele.”

    Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu,

  49. 20 Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu 21 na kusema:

    “Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,

    nami nitaondoka uchi,

    Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa,

    jina la Bwana litukuzwe.”

    22 Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.

  50. 8 Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu,

    sauti ya sifa yake isikike,

    9 ameyahifadhi maisha yetu

    na kuizuia miguu yetu kuteleza.

  51. 13 Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako,

    tutakusifu milele;

    toka kizazi hadi kizazi

    tutasimulia sifa zako.

  52. 4 Katika siku hiyo mtasema:

    “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake;

    julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,

    tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

    5 Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu,

    hili na lijulikane duniani kote.

    6 Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,

    kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”

  53. 17 Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa. 18 Nanyi, mkiisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mmekuwa watumwa wa haki.

  54. 24 Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

    25 Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.

  55. 13 Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.

  56. 8 Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema:

    “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,

    ni Bwana Mungu Mwenyezi,

    aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”

    9 Kila mara viumbe hao wanne wenye uhai wanapomtukuza, kumheshimu na kumshukuru yeye aketiye kwenye kile kiti cha enzi, tena aishiye milele na milele, 10 wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake aketiye kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi, wakisema:

    11 “Bwana wetu na Mungu wetu,

    wewe unastahili kupokea utukufu

    na heshima na uweza,

    kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote,

    na kwa mapenzi yako viliumbwa

    na vimekuwako.”