30 Bible Verses About Heartbreak

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Heartbreak
  1. 18 Bwana yu karibu na waliovunjika moyo,

    na huwaokoa waliopondeka roho.

    19 Mwenye haki ana mateso mengi,

    lakini Bwana humwokoa nayo yote,

    20 huhifadhi mifupa yake yote,

    hata mmoja hautavunjika.

  2. 2 Bwana hujenga Yerusalemu,

    huwakusanya Israeli walio uhamishoni.

    3 Anawaponya waliovunjika mioyo

    na kuvifunga vidonda vyao.

    4 Huzihesabu nyota

    na huipa kila moja jina lake.

    5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,

    ufahamu wake hauna kikomo.

    6 Bwana huwahifadhi wanyenyekevu

    lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.

  3. 3 Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”

  4. 27 Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

  5. 22 Mtwike Bwana fadhaa zako,

    naye atakutegemeza,

    hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

  6. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

    wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

    6 katika njia zako zote mkiri yeye,

    naye atayanyoosha mapito yako.

    7 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;

    mche Bwana ukajiepushe na uovu.

    8 Hii itakuletea afya mwilini mwako,

    na mafuta kwenye mifupa yako.

  7. 28 “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”

  8. 10 Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

    usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

    Nitakutia nguvu na kukusaidia;

    nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

  9. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

  10. 26 Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,

    bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu

    na fungu langu milele.

  11. 7 Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.

  12. 33 Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

  13. 20 Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu,

    utanihuisha tena,

    kutoka vilindi vya dunia

    utaniinua tena.

  14. 12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,

    bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.

    13 Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi,

    bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.

    14 Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,

    ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

    15 Ufahamu mzuri hupata upendeleo,

    bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.

    16 Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa,

    bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.

  15. 8 Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; 9 twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi. 10 Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Yesu ili kwamba uzima wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu.

  16. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.

    1 Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,

    wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

    2 Unirehemu Bwana,

    kwa maana nimedhoofika;

    Ee Bwana, uniponye,

    kwa maana mifupa yangu

    ina maumivu makali.

    3 Nafsi yangu ina uchungu mwingi.

    Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?

    4 Geuka Ee Bwana, unikomboe,

    uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

    5 Hakuna mtu anayekukumbuka

    akiwa amekufa.

    Ni nani awezaye kukusifu

    akiwa kuzimu?

    6 Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;

    usiku kucha nafurikisha

    kitanda changu kwa machozi;

    nimelowesha viti vyangu vya fahari

    kwa machozi.

    7 Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,

    yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.

  17. 1 Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,

    kwa sababu Bwana amenitia mafuta

    kuwahubiria maskini habari njema.

    Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

    kuwatangazia mateka uhuru wao,

    na hao waliofungwa

    habari za kufunguliwa kwao;

  18. 6 “Kwa hiyo lia kwa uchungu, mwanadamu! Lia kwa uchungu mbele yao kwa moyo uliopondeka na kwa huzuni nyingi.

  19. 10 waliokombolewa na Bwana watarudi.

    Wataingia Sayuni wakiimba;

    furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.

    Watapata furaha na shangwe;

    huzuni na majonzi vitakimbia.

  20. 21 Yesu akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

    22 Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana. Akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

  21. 33 Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana. 34 Akauliza, “Mmemweka wapi?”

    Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.”

    35 Yesu akalia machozi.

  22. 20 Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. 22 Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

  23. 18 Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu.

  24. 9 Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

  25. 5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

    bali upendo wake hudumu siku zote.

    Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

    lakini asubuhi kukawa na furaha.

  26. 18 “Msiyakumbuke mambo yaliyopita,

    wala msiyatafakari mambo ya zamani.

    19 Tazama, nitafanya jambo jipya!

    Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?

    Nitafanya njia jangwani

    na vijito vya maji katika nchi kame.

  27. 4 Heri wale wanaohuzunika,

    maana hao watafarijiwa.

  28. 18 “Roho wa Bwana yu juu yangu,

    kwa sababu amenitia mafuta

    kuwahubiria maskini habari njema.

    Amenituma kuwatangazia wafungwa

    kufunguliwa kwao,

    na vipofu kupata kuona tena,

    kuwaweka huru wanaoonewa,

  29. 4 Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. 5 Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

    8 Upendo haushindwi kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; zikiwepo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatapita.

  30. 6 Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana, 7 kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.