60 Bible Verses About Justice

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Justice
  1. 6 Nimjie Bwana na kitu gani na kusujudu

    mbele za Mungu aliyetukuka?

    Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa,

    nije na ndama za mwaka mmoja?

    7 Je, Bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu,

    au mito elfu kumi ya mafuta?

    Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu,

    mtoto wangu mwenyewe

    kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?

    8 Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu.

    Bwana anataka nini kwako?

    Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,

    na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

    9 Sikiliza! Bwana anauita mji:

    kulicha jina lako ni hekima:

    “Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru.

  2. 19 Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki. 20 Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa.

  3. 16 jiosheni na mkajitakase.

    Yaondoeni matendo yenu maovu

    mbele zangu!

    Acheni kutenda mabaya,

    17 jifunzeni kutenda mema!

    Tafuteni haki,

    watieni moyo walioonewa.

    Teteeni shauri la yatima,

    wateteeni wajane.

    18 “Njooni basi tuhojiane,”

    asema Bwana.

    “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu,

    zitakuwa nyeupe kama theluji;

    ingawa ni nyekundu sana kama damu,

    zitakuwa nyeupe kama sufu.

  4. 21 Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Sheria na Manabii wanaishuhudia. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti, 23 kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. 25 Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. 26 Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu, ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.

  5. 2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki

    na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

    3 Teteeni wanyonge na yatima,

    tunzeni haki za maskini na walioonewa.

    4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji,

    wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

  6. 8 “Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,

    kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.

    9 Sema na uamue kwa haki,

    tetea haki za maskini na wahitaji.”

  7. 8 “Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki,

    na ninachukia unyangʼanyi na uovu.

    Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao

    na kufanya agano la milele nao.

    9 Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,

    na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.

    Wale wote watakaowaona watatambua

    kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.”

  8. 9 “Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. 10 Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

  9. 6 “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. 7 Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia.

    8 “Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki.

    9 “Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri.

  10. 13 Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. 14 Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. 15 Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 16 Kwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu.

  11. 3 Nitalitangaza jina la Bwana.

    Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu!

    4 Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu,

    njia zake zote ni haki.

    Mungu mwaminifu ambaye hakosei,

    yeye ni mnyofu na mwenye haki.

  12. 11 Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki, 12 nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako.

  13. 3 Heri wale wanaodumisha haki,

    ambao daima wanafanya yaliyo mema.

    4 Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako,

    uwe msaada wangu unapowaokoa,

  14. 1 Hili ndilo asemalo Bwana:

    “Dumisheni haki

    na mkatende lile lililo sawa,

    kwa maana wokovu wangu u karibu

    na haki yangu itafunuliwa upesi.

  15. 4 Maana neno la Bwana ni haki na kweli,

    ni mwaminifu kwa yote atendayo.

    5 Bwana hupenda uadilifu na haki;

    dunia imejaa upendo wake usiokoma.

  16. 3 Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika

    zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.

  17. 13 “ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako.

    “ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

    14 “ ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

    15 “ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

  18. 27 Acha ubaya na utende wema,

    nawe utaishi katika nchi milele.

    28 Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki

    naye hatawaacha waaminifu wake.

    Watalindwa milele,

    lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.

    29 Wenye haki watairithi nchi,

    na kuishi humo milele.

  19. 15 Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki,

    bali kitisho kwa watenda mabaya.

  20. 1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

    2 “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu,

  21. 16 Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena. 17 Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa. 18 Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19 Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri.

  22. 23 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnatoa zaka ya mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu zaidi ya sheria, yaani haki, huruma na uaminifu. Iliwapasa kufanya haya makuu ya sheria bila kupuuza hayo matoleo.

  23. 35 “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. 36 Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

    37 “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Bwana.’ ”

  24. 6 Bwana hutenda haki,

    naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.

  25. 13 Mkono wako umejaa uwezo;

    mkono wako una nguvu,

    mkono wako wa kuume umetukuzwa.

    14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;

    upendo na uaminifu vinakutangulia.

  26. 16 Pia nikaona kitu kingine tena chini ya jua:

    Mahali pa kutolea hukumu,

    uovu ulikuwepo,

    mahali pa kupatia haki,

    uovu ulikuwepo.

    17 Nikafikiri moyoni mwangu,

    “Mungu atawaleta hukumuni

    wote wawili wenye haki na waovu,

    kwa maana kutakuwako na wakati kwa ajili ya kila jambo,

    wakati kwa ajili ya kila tendo.”

  27. 3 naye atafurahia kumcha Bwana.

    Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,

    wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

    4 bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,

    kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.

    Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,

    kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.

    5 Haki itakuwa mkanda wake

    na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.

  28. 1 “Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza,

    mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye;

    nitaweka Roho yangu juu yake,

    naye ataleta haki kwa mataifa.

    2 Hatapaza sauti wala kupiga kelele,

    wala hataiinua sauti yake barabarani.

    3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja,

    na utambi unaofuka moshi hatauzima.

    Kwa uaminifu ataleta haki,

    4 hatazimia roho wala kukata tamaa,

    mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia.

    Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.”

  29. 26 Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. 27 Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu. 28 Yeyote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu. 29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema? 30 Kwa kuwa tunamjua yeye aliyesema, “Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.” Tena asema, “Bwana atawahukumu watu wake.” 31 Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.

  30. 12 Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu.

    Usiwasahau wanyonge.

    13 Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?

    Kwa nini anajiambia mwenyewe,

    “Hataniita nitoe hesabu?”

    14 Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,

    umekubali kuyapokea mkononi mwako.

    Mhanga anajisalimisha kwako,

    wewe ni msaada wa yatima.

    15 Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,

    mwite atoe hesabu ya maovu yake

    ambayo yasingejulikana.

    16 Bwana ni Mfalme milele na milele,

    mataifa wataangamia watoke nchini mwake.

    17 Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,

    wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,

    18 ukiwatetea yatima na walioonewa,

    ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.

  31. 5 Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,

    au kumnyima haki asiye na hatia.

  32. 5 Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake. 6 Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi 7 na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 8 Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. 9 Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake, 10 siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.

  33. 1 Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,

    bali vipimo sahihi ni furaha yake.

  34. 23 Hii pia ni misemo ya wenye hekima:

    Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema:

    24 Yeyote amwambiaye mwenye hatia,

    “Wewe huna hatia,”

    Kabila zitamlaani

    na mataifa yatamkana.

    25 Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia,

    nazo baraka tele zitawajilia juu yao.

  35. 14 Tafuteni mema, wala si mabaya,

    ili mpate kuishi.

    Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi,

    kama msemavyo yupo nanyi.

    15 Yachukieni maovu, yapendeni mema;

    dumisheni haki mahakamani.

    Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote

    atawahurumia mabaki ya Yosefu.

  36. 23 Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, 24 kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia. 25 Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.

  37. 23 Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu? 24 Je, ikiwa watakuwepo watu wenye haki hamsini katika mji huo, hivi kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo ndani yake? 25 Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?”

    26 Bwana akasema, “Kama nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitausamehe huo mji wote kwa ajili yao.”

  38. 11 Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu,

    nao walioniona walinisifu,

    12 kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,

    naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.

    13 Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,

    nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.

    14 Niliivaa haki kama vazi langu;

    uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.

    15 Nilikuwa macho ya kipofu

    na miguu kwa kiwete.

    16 Nilikuwa baba kwa mhitaji;

    nilimtetea mgeni.

    17 Niliyavunja meno makali ya waovu,

    na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.

  39. 7 Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki,

    yeye hupenda haki.

    Wanyofu watauona uso wake.

  40. 5 Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,

    ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,

    6 Muumba wa mbingu na nchi,

    na bahari na vyote vilivyomo ndani yake:

    Bwana anayedumu kuwa mwaminifu

    milele na milele.

    7 Naye huwapatia haki walioonewa

    na kuwapa wenye njaa chakula.

    Bwana huwaweka wafungwa huru,

    8 Bwana huwafumbua vipofu macho,

    Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao,

    Bwana huwapenda wenye haki.

    9 Bwana huwalinda wageni

    na kuwategemeza yatima na wajane,

    lakini hupinga njia za waovu.

  41. 26 Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala,

    bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.

    27 Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu;

    waovu huwachukia sana wenye haki.

  42. 3 Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

  43. 1 Kila mtu na atii mamlaka inayotawala, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, nazo mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo yeye anayeasi dhidi ya mamlaka inayotawala anaasi dhidi ya kile kilichowekwa na Mungu, nao wale wafanyao hivyo watajiletea hukumu juu yao wenyewe. 3 Kwa kuwa watawala hawawatishi watu wale wanaotenda mema bali wale wanaotenda mabaya. Je, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Basi tenda lile lililo jema naye atakusifu. 4 Kwa maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Lakini kama ukitenda mabaya, basi ogopa, kwa kuwa hauinui upanga bila sababu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa kutekeleza adhabu juu ya watenda mabaya.

  44. 1 Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni.

  45. 17 Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni. 18 Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, 19 bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa. 20 Yeye alichaguliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 21 Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu.

  46. 5 Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema:

    “Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa,

    wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu,

    kwa sababu umehukumu hivyo;

    6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako

    na manabii wako,

    nawe umewapa damu wanywe

    kama walivyostahili.”

    7 Nikasikia madhabahu ikiitikia,

    “Naam, Bwana Mungu Mwenyezi,

    hukumu zako ni kweli na haki.”

  47. 11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita.

  48. Zaburi ya Daudi.

    1 Ee Bwana, sikia sala yangu,

    sikiliza kilio changu unihurumie;

    katika uaminifu na haki yako

    njoo unisaidie.

    2 Usimhukumu mtumishi wako,

    kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako.

  49. 5 Watu wabaya hawaelewi haki,

    bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

  50. 14 Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki,

    kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.

  51. 14 Hivyo uadilifu umerudishwa nyuma,

    nayo haki inasimama mbali,

    kweli imejikwaa njiani,

    uaminifu hauwezi kuingia.

    15 Kweli haipatikani popote,

    na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.

    Bwana alitazama naye akachukizwa

    kwamba hapakuwepo haki.

  52. 5 “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, na wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  53. 19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. 20 Badala yake:

    “Kama adui yako ana njaa, mlishe;

    kama ana kiu, mpe kinywaji.

    Kwa kufanya hivyo,

    unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”

  54. 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

  55. 27 Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.

  56. 7 Bwana anatawala milele,

    ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.

    8 Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki,

    atatawala mataifa kwa haki.

  57. 13 Mungu wa Abrahamu na Isaki na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Mwanawe Yesu, ambaye ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato, ingawa yeye alikuwa ameamua kumwachia aende zake. 14 Ninyi mlimkataa huyo Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 15 Hivyo mkamuua aliye chanzo cha uzima, lakini Mungu akamfufua kutoka kwa wafu. Sisi tu mashahidi wa mambo haya.

  58. 3 Hivyo wewe mwanadamu, utoapo hukumu juu yao na bado unafanya mambo yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? 4 Au waudharau wingi wa wema, ustahimili na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu wakuelekeza kwenye toba?

    5 Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa. 6 Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. 7 Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. 8 Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

  59. 2 Kwa kuwa kama ujumbe ulionenwa na malaika ulikuwa imara, na kila uasi na kutokutii kulipata adhabu ya haki, 3 je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana, ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia.

  60. 9 Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.