65 Bible Verses About Adultery

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Adultery
  1. 27 “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ 28 Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu. 30 Kama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu.

    31 “Pia ilinenwa kwamba, ‘Mtu yeyote amwachaye mkewe sharti ampe hati ya talaka.’ 32 Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.

  2. 14 Usizini.

    15 Usiibe.

    16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

    17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.”

    18 Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali 19 na wakamwambia Mose, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.”

  3. 23 Kwa maana amri hizi ni taa,

    mafundisho haya ni mwanga

    na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

    24 yakikulinda na mwanamke aliyepotoka,

    kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.

    25 Moyo wako usitamani uzuri wake

    wala macho yake yasikuteke,

    26 kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini,

    hata ukose kipande cha mkate,

    naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.

    27 Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake

    bila nguo zake kuungua?

    28 Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka

    bila miguu yake kuungua?

    29 Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;

    hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.

    30 Watu hawamdharau mwizi kama akiiba

    kukidhi njaa yake wakati ana njaa.

    31 Pamoja na hayo, kama akikamatwa,

    lazima alipe mara saba,

    ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.

    32 Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;

    yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.

    33 Mapigo na aibu ni fungu lake

    na aibu yake haitafutika kamwe;

    34 kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,

    naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.

    35 Hatakubali fidia yoyote;

    atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.

  4. 9 Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, 10 wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu. 11 Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.

  5. 4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.

  6. 6 Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko. 7 Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili. 8 Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa ajili ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi. 9 Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti. 10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema Bwana.

  7. 3 Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba

    hudondoza asali,

    na maneno ya kinywa chake

    ni laini kuliko mafuta;

    4 lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,

    mkali kama upanga ukatao kuwili.

    5 Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;

    hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.

    6 Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima;

    njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

    7 Sasa basi wanangu, nisikilizeni;

    msiache ninalowaambia.

    8 Njia zenu ziwe mbali naye,

    msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

    9 usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine

    na miaka yako kwa aliye mkatili,

    10 wageni wasije wakasherehekea utajiri wako

    na jitihada yako ikatajirisha

    nyumba ya mwanaume mwingine.

    11 Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,

    wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

    12 Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!

    Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

    13 Sikuwatii walimu wangu

    wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

    14 Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa

    katikati ya kusanyiko lote.”

    15 Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe,

    maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.

    16 Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji

    na vijito vyako vya maji viwanjani?

    17 Na viwe vyako mwenyewe,

    kamwe visishirikishwe wageni.

    18 Chemchemi yako na ibarikiwe

    na umfurahie mke wa ujana wako.

    19 Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri:

    matiti yake na yakutosheleze siku zote,

    nawe utekwe daima na upendo wake.

    20 Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba?

    Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?

    21 Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana,

    naye huyapima mapito yake yote.

    22 Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe;

    kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.

    23 Atakufa kwa kukosa nidhamu,

    akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.

  8. 10 “ ‘Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe.

    11 “ ‘Kama mtu atakutana kimwili na mke wa baba yake, hakumheshimu baba yake. Mwanaume huyo na mwanamke huyo wote wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

    12 “ ‘Ikiwa mtu atakutana kimwili na mke wa mwanawe, lazima wote wawili wauawe. Walichokifanya ni upotovu; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

  9. 8 Yesu akawajibu, “Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. 9 Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.”

  10. 20 “Hata hivyo, nina neno dhidi yako: Unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu ili wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kafara kwa sanamu. 21 Nimempa muda ili atubu kwa ajili ya uasherati wake, lakini hataki. 22 Kwa hiyo nitamtupa kwenye kitanda cha mateso, na nitawafanya hao wanaozini naye kupata mateso makali wasipotubia njia zake. 23 Nami nitawaua watoto wake. Nayo makanisa yote yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo yanayoitwa mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wowote juu yenu): 25 Lakini shikeni sana mlicho nacho, mpaka nitakapokuja.

  11. 10 “Watakula lakini hawatashiba;

    watajiingiza katika ukahaba

    lakini hawataongezeka,

    kwa sababu wamemwacha Bwana

    na kujiingiza wenyewe

    11 katika ukahaba,

    divai ya zamani na divai mpya,

    ambavyo huondoa ufahamu

    12 wa watu wangu.

    Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti

    nao hujibiwa na fimbo ya mti.

    Roho ya ukahaba imewapotosha,

    hawana uaminifu kwa Mungu wao.

    13 Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima

    na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima,

    chini ya mialoni, milibua na miela,

    ambako kuna vivuli vizuri.

    Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba

    na wake za wana wenu uzinzi.

    14 “Sitawaadhibu binti zenu wakati

    wanapogeukia ukahaba,

    wala wake za wana wenu

    wanapofanya uzinzi,

    kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya

    na kutambikia pamoja na makahaba

    wa mahali pa kuabudia miungu:

    watu wasiokuwa na ufahamu

    wataangamia!

  12. 11 Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. 12 Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.”

  13. 3 Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. 4 Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 5 Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” 6 Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki.

    Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. 7 Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.” 8 Akainama tena na kuandika ardhini.

    9 Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. 10 Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?”

    11 Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.”

    Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]

  14. 6 Basi mambo haya yalitokea kama mifano ili kutuzuia tusiweke mioyo yetu katika mambo maovu kama wao walivyofanya. 7 Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 8 Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 9 Wala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 Msinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu.

    11 Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. 12 Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 13 Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

    14 Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu.

  15. 14 Naye Mungu aliyemfufua Bwana kutoka kwa wafu atatufufua sisi pia kwa uweza wake. 15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Kristo mwenyewe? Je, nichukue viungo vya mwili wa Kristo na kuviunganisha na mwili wa kahaba? La hasha! 16 Hamjui kwamba aliyeungwa na kahaba anakuwa mwili mmoja naye? Kwa kuwa imenenwa, “Hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 17 Lakini mtu aliyeungwa na Bwana anakuwa roho moja naye.

    18 Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe. 19 Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, 20 kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

  16. 22 Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

    23 Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye, 24 utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

    25 Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

  17. 1 Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke. 2 Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. 3 Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe. 4 Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe. 5 Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.

  18. 4 Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu. 5 Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6 Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema:

    “Mungu huwapinga wenye kiburi,

    lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

    7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.

  19. 9 “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke,

    au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,

    10 basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine,

    nao wanaume wengine walale naye.

    11 Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu,

    naam, dhambi ya kuhukumiwa.

    12 Ni moto uwakao kwa Uharibifu;

    ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.

  20. 9 Kwa nini ulilidharau neno la Bwana kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni. 10 Basi kwa hiyo, upanga hautaondoka nyumbani mwako kamwe kwa sababu ulinidharau mimi na kumchukua mke wa Uria, Mhiti kuwa mkeo.’

    11 “Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Kutoka kwa nyumba yako mwenyewe nitaleta maafa juu yako. Mbele ya macho yako mwenyewe nitatwaa wake zako na kumpa yeye aliye wa karibu nawe, naye atakutana kimwili na wake zako mchana mwangavu. 12 Ulifanya kwa siri, lakini nitalifanya jambo hili wakati wa mchana mwangavu mbele ya Israeli yote.’ ”

    13 Ndipo Daudi akamjibu Nathani, “Nimefanya dhambi dhidi ya Bwana.”

    Nathani akamjibu, “Bwana amekuondolea dhambi yako. Hutakufa. 14 Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za Bwana kuonyesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa.”

  21. 17 Je, hamwelewi kwamba chochote kiingiacho kinywani huenda tumboni, na hatimaye hutolewa nje kikiwa uchafu? 18 Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. 19 Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. 20 Haya ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.”

  22. 1 Neno la Bwana lililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi, mfalme wa Israeli.

    2 Wakati Bwana alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, Bwana alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha Bwana.” 3 Kwa hiyo alimwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba na kumzalia Hosea mwana.

  23. 18 “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kumwoa mwanamke mwingine anazini, naye mwanaume amwoaye mwanamke aliyetalikiwa anazini.

  24. 2 Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka sheria ya ndoa. 3 Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi. Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.

  25. 19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.

  26. 3 Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, 4 ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, 5 si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. 6 Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali. 7 Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu.

  27. 18 Usizini.

  28. 37 kwa kuwa wamefanya uzinzi na damu imo mikononi mwao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, hata wamewatoa watoto wao walionizalia kuwa kafara, kuwa chakula kwao.

  29. 18 Mtawala mmoja akamuuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

    19 Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. 20 Unazijua amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

  30. 7 “Kwa nini niwasamehe?

    Watoto wenu wameniacha na kuapa kwa miungu ambayo si miungu.

    Niliwapatia mahitaji yao yote,

    lakini bado wamefanya uzinzi na kusongana katika nyumba za makahaba.

    8 Wamelishwa vizuri, kama farasi waume wenye tamaa nyingi,

    kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine.

  31. 2 “Mkemeeni mama yenu, mkemeeni,

    kwa maana yeye si mke wangu,

    nami si mume wake.

    Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake

    na uzinzi kati ya matiti yake.

    3 Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchi

    na kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa.

    Nitamfanya kama jangwa,

    nitamgeuza awe nchi ya kiu,

    nami nitamuua kwa kiu.

    4 Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake,

    kwa sababu ni watoto wa uzinzi.

    5 Mama yao amekosa uaminifu

    na amewachukua mimba katika aibu.

    Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu,

    ambao hunipa chakula changu

    na maji yangu,

    sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu

    na kinywaji changu.’

    6 Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yake

    kwa vichaka vya miiba,

    nitamjengea ukuta ili kwamba

    asiweze kutoka.

    7 Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata;

    atawatafuta lakini hatawapata.

    Kisha atasema,

    ‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza,

    kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi

    kuliko sasa.’

  32. 20 Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21 Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, 22 tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”

  33. 38 Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamwambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”

    39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.

  34. 18 Yule mtu akamuuliza, “Amri zipi?”

    Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,

  35. 22 Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke

    kama fahali aendaye machinjoni,

    kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,

    23 mpaka mshale umchome ini lake,

    kama ndege anayenaswa kwenye mtego,

    bila kujua itamgharimu maisha yake.

    24 Sasa basi wanangu, nisikilizeni;

    sikilizeni kwa makini nisemalo.

    25 Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,

    wala usitangetange katika mapito yake.

    26 Aliowaangusha ni wengi;

    aliowachinja ni kundi kubwa.

    27 Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,

    ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

  36. 13 “Miongoni mwa manabii wa Samaria

    nililiona jambo la kuchukiza:

    Walitabiri kwa Baali

    na kuwapotosha Israeli watu wangu.

    14 Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu

    nimeona jambo baya sana:

    Wanafanya uzinzi

    na kuenenda katika uongo.

    Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,

    kwa ajili hiyo hakuna yeyote

    anayeachana na uovu wake.

    Wote wako kama Sodoma kwangu;

    watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”

  37. 19 Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

  38. 10 Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi ila ni Bwana): Mke asitengane na mumewe. 11 Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.

  39. 10 Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria.

  40. 13 Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki katika karamu zenu. 14 Wakiwa na macho yaliyojaa uzinzi, kamwe hawaachi kutenda dhambi. Huwashawishi wale wasio imara. Wao ni hodari kwa kutamani; ni wana wa laana! 15 Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa mshahara wa uovu.

  41. 20 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.

  42. 14 Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;

    yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana

    atatumbukia ndani yake.

  43. 22 Kwa ajili yao, watu wote wa uhamisho kutoka Yuda walioko Babeli watatumia laana hii: ‘Bwana na akutendee kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwachoma kwa moto.’ 23 Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya. Nami nayajua haya, na ni shahidi wa jambo hilo,” asema Bwana.

  44. 32 “ ‘Wewe mke mzinzi! Unapenda wageni, kuliko mume wako mwenyewe.

  45. 1 Sikieni neno la Bwana, enyi Waisraeli,

    kwa sababu Bwana analo shtaka

    dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi:

    “Hakuna uaminifu, hakuna upendo,

    hakuna kumjua Mungu katika nchi.

    2 Kuna kulaani tu, uongo na uuaji,

    wizi na uzinzi,

    bila kuwa na mipaka,

    nao umwagaji damu mmoja

    baada ya mwingine.

  46. 13 Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya Bwana kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. 14 Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababu Bwana ni shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa.

    15 Je, Bwana hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.

    16 “Ninachukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

    Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

  47. 22 Kisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

    23 Huyo mwanaume akasema,

    “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu

    na nyama ya nyama yangu,

    ataitwa ‘mwanamke,’

    kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

    24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

  48. 7 baada ya kitambo mke wa Potifa akamtamani Yosefu, akamwambia, “Njoo, ukutane nami kimwili!”

    8 Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi. 9 Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” 10 Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yosefu siku baada ya siku, Yosefu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye.

    11 Siku moja Yosefu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwepo na mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. 12 Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia.

  49. 1 Katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati wafalme watokapo kwenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu pamoja na watu wa mfalme na jeshi lote la Israeli. Wakawaangamiza Waamoni na kuuzunguka kwa jeshi mji wa Raba. Lakini Daudi akabaki Yerusalemu.

    2 Ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi aliinuka kitandani mwake na kutembeatembea juu ya paa la jumba lake la kifalme. Kutokea kule kwenye paa, akamwona mwanamke akioga. Mwanamke huyo alikuwa mzuri sana wa sura, 3 naye Daudi akatuma mtu mmoja kuuliza habari za huyo mwanamke. Huyo mtu akamwambia Daudi, “Je, huyu si Bathsheba binti Eliamu, naye ni mke wa Uria, Mhiti?” 4 Ndipo Daudi akatuma wajumbe kumleta. Huyo mwanamke akaja kwa Daudi, Daudi akakutana naye kimwili. (Huyo mwanamke ndipo tu alikuwa amejitakasa kutoka siku zake za hedhi.) Kisha akarudi nyumbani kwake. 5 Huyo mwanamke akapata mimba akampelekea Daudi ujumbe, kusema, “Mimi ni mjamzito.”

  50. 15 Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza,

    naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’

    naye huuficha uso wake.

    16 Katika giza, huvunja majumba,

    lakini wakati wa mchana hujifungia ndani;

    hawataki kufanya lolote nuruni.

    17 Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao;

    hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.

    18 “Lakini wao ni povu juu ya maji;

    sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa,

    hivyo hakuna hata mmoja

    aendaye kwenye shamba la mizabibu.

  51. 1 Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,

    kwa sababu Bwana amenitia mafuta

    kuwahubiria maskini habari njema.

    Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

    kuwatangazia mateka uhuru wao,

    na hao waliofungwa

    habari za kufunguliwa kwao;

    2 kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,

    na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

    kuwafariji wote waombolezao,

    3 na kuwapa mahitaji

    wale wanaohuzunika katika Sayuni,

    ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,

    mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

    vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

    Nao wataitwa mialoni ya haki,

    pando la Bwana,

    ili kuonyesha utukufu wake.

  52. 9 “ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo, na kufukiza uvumba kwa Baali, na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, 10 kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza?

  53. 27 uzinzi wako na kulia kwako kama farasi kulikojaa tamaa,

    ukahaba wako usio na aibu!

    Nimeyaona matendo yako ya machukizo

    juu ya vilima na mashambani.

    Ole wako, ee Yerusalemu!

    Utaendelea kuwa najisi mpaka lini?”

  54. 3 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?”

    4 Akawajibu, “Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, 5 naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? 6 Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”

  55. 15 Lakini kama yule asiyeamini akijitenga, basi afanye hivyo. Katika hali kama hiyo mwanamke au mwanaume aaminiye hafungwi, kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani.

  56. 17 Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 18 Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili.

  57. 18 “Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana,

    naam, vinne nisivyovielewa:

    19 Ni mwendo wa tai katika anga,

    mwendo wa nyoka juu ya mwamba,

    mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari,

    nao mwendo wa mtu pamoja na msichana.

    20 “Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi,

    hula akapangusa kinywa chake na kusema,

    ‘Sikufanya chochote kibaya.’

  58. 1 kila mara nilipotaka kumponya Israeli,

    dhambi za Efraimu zinafichuliwa

    na maovu ya Samaria yanafunuliwa.

    Wanafanya udanganyifu,

    wevi huvunja nyumba,

    maharamia hunyangʼanya barabarani,

    2 lakini hawafahamu kwamba

    ninakumbuka matendo yao yote mabaya.

    Dhambi zao zimewameza,

    ziko mbele zangu siku zote.

    3 “Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,

    wakuu wao kwa uongo wao.

    4 Wote ni wazinzi,

    wanawaka kama tanuru

    ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea

    kuanzia kukanda unga

    hadi umekwisha kuumuka.

  59. 5 “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, na wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  60. 22 Wewe usemaye mtu asizini, wewe mwenyewe wazini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, wafanya jambo la kumchukiza katika mahekalu?

  61. 9 Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

  62. 16 Wewe mke, unajuaje kama utamwokoa mumeo? Au wewe mume unajuaje kama utamwokoa mkeo?

  63. 17 Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

    20 Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo.

  64. 15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. 16 Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 17 Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

  65. 8 Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”