40 Bible Verses About Procrastination

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Procrastination
  1. 6 Ewe mvivu, mwendee mchwa;

    zitafakari njia zake ukapate hekima!

    7 Kwa maana yeye hana msimamizi,

    wala mwangalizi, au mtawala,

    8 lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi

    na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

    9 Ewe mvivu, utalala hata lini?

    Utaamka lini kutoka usingizi wako?

    10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

    bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

    11 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

    na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

  2. 13 Mvivu husema, “Yuko simba barabarani,

    simba mkali anazunguka mitaa!”

    14 Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake,

    ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.

    15 Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,

    naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.

    16 Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe,

    kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

  3. 4 Mvivu halimi kwa majira;

    kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama

    lakini hapati chochote.

  4. 4 Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini

    lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.

    5 Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi

    ni mwana mwenye hekima,

    lakini yeye alalaye wakati wa mavuno

    ni mwana mwenye kuaibisha.

  5. 24 Mikono yenye bidii itatawala,

    bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.

  6. 4 Mvivu hutamani sana na hapati kitu,

    bali nafsi ya mwenye bidii

    hutoshelezwa kikamilifu.

  7. 59 Yesu akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.”

    Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

    60 Yesu akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.”

    61 Mtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikawaage jamaa yangu.”

    62 Yesu akamwambia, “Mtu yeyote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”

  8. 30 Nilipita karibu na shamba la mvivu,

    karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,

    31 miiba ilikuwa imeota kila mahali,

    ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na

    ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.

    32 Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona,

    nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:

    33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

    bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

    34 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

    na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

  9. 15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16 mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana.

  10. 9 Mtu aliye mlegevu katika kazi yake

    ni ndugu na yule anayeharibu.

  11. 13 Mvivu husema, “Yuko simba nje!”

    au, “Nitauawa katika mitaa!”

  12. 19 Njia ya mvivu imezibwa na miiba,

    bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.

  13. 13 Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,

    uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.

  14. 25 Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake,

    kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.

    26 Mchana kutwa hutamani zaidi,

    lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.

  15. 13 Basi sikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.” 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, “Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.” 16 Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni uovu.

  16. 27 Mtu mvivu haoki mawindo yake,

    bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.

  17. 13 Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

  18. 7 Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, 8 wala hatukula chakula cha mtu yeyote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote miongoni mwenu. 9 Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe kielelezo. 10 Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.”

    11 Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. 12 Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Yesu Kristo, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe.

  19. 15 Uvivu huleta usingizi mzito,

    naye mtu mzembe huona njaa.

  20. 18 Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama,

    kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.

  21. 60 Nitafanya haraka bila kuchelewa

    kuzitii amri zako.

  22. 33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia. 34 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.

  23. 1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. 2 Kwa maana asema:

    “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia,

    siku ya wokovu nilikusaidia.”

    Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa.

  24. 23 Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, 24 kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia.

  25. 9 Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu. 10 Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia. 11 Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, 12 ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi.

  26. 26 Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho,

    ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.

  27. 24 Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,

    lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!

  28. 4 Wakati unapomwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza. Yeye hafurahii wapumbavu; timiza nadhiri yako. 5 Ni afadhali usiweke nadhiri kuliko kuiweka na usiitimize.

  29. 4 Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.

  30. 14 Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote.

  31. 17 Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.

  32. 9 Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.

  33. 21 Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

  34. 19 Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,

    bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.

  35. 10 Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.

  36. 6 Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana;

    mwiteni maadamu yu karibu.

  37. 16 Mpeni utukufu Bwana Mungu wenu,

    kabla hajaleta giza,

    kabla miguu yenu haijajikwaa

    juu ya vilima vitakavyotiwa giza.

    Mlitarajia nuru,

    lakini ataifanya kuwa giza nene

    na kuibadili kuwa huzuni kubwa.

  38. 16 Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Bwana alikuwa na huruma kwao.

  39. 11 Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,

    bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

  40. 23 “Kwa hiyo, kama unatoa sadaka yako madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako ana kitu dhidi yako, 24 iache sadaka yako hapo mbele ya madhabahu. Enda kwanza ukapatane na ndugu yako; kisha urudi na ukatoe sadaka yako.

    25 “Patana na mshtaki wako upesi wakati uwapo njiani pamoja naye kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani.