19 Bible Verses About Time Management

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Time Management
  1. 14 kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana:

    “Amka, wewe uliyelala,

    ufufuke kutoka kwa wafu,

    naye Kristo atakuangazia.”

    15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16 mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana.

  2. 13 Basi sikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.” 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, “Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.” 16 Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni uovu. 17 Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.

  3. 12 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

    ili tujipatie moyo wa hekima.

  4. 4 “Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu

    na hesabu ya siku zangu;

    nijalie kujua jinsi maisha yangu

    yanavyopita upesi.

    5 Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;

    muda wangu wa kuishi ni kama

    hauna thamani kwako.

    Maisha ya kila mwanadamu

    ni kama pumzi.

    6 Hakika kila binadamu ni kama njozi

    aendapo huku na huko:

    hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili;

    anakusanya mali nyingi,

    wala hajui ni nani atakayeifaidi.

  5. 33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.

  6. KITABU CHA NNE

    Maombi ya Mose, mtu wa Mungu.

    1 Bwana, wewe umekuwa makao yetu

    katika vizazi vyote.

    2 Kabla ya kuzaliwa milima

    au hujaumba dunia na ulimwengu,

    wewe ni Mungu tangu milele hata milele.

    3 Huwarudisha watu mavumbini,

    ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”

    4 Kwa maana kwako miaka elfu

    ni kama siku moja iliyokwisha pita,

    au kama kesha la usiku.

    5 Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo,

    nao ni kama majani machanga ya asubuhi:

    6 ingawa asubuhi yanachipua,

    ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka.

  7. 14 Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana;

    nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”

    15 Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,

    uniokoe mikononi mwa adui zangu

    na wale wanifuatiao.

  8. 11 Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho.

  9. 8 Lakini wapenzi, msisahau neno hili: kwamba kwa Bwana, siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.

  10. 6 Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana;

    mwiteni maadamu yu karibu.

  11. 11 Nanyi fanyeni hivi, mkiutambua wakati tulio nao. Saa ya kuamka kutoka usingizini imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu umekaribia zaidi kuliko hapo kwanza tulipoamini. 12 Usiku umeendelea sana, mapambazuko yamekaribia. Kwa hiyo tuyaweke kando matendo ya giza na tuvae silaha za nuru. 13 Basi na tuenende kwa adabu kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa kufanya karamu za ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi.

  12. 5 Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.

  13. 1 Usijisifu kwa ajili ya kesho,

    kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.

  14. 2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamriwa, sikukuu zilizoamriwa za Bwana, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu.

    3 “ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwa Bwana.

    4 “ ‘Hizi ni sikukuu za Bwana zilizoamriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamriwa:

  15. 10 Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,

    au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,

    lakini yote ni ya shida na taabu,

    nazo zapita haraka, nasi twatoweka.

  16. 6 Ewe mvivu, mwendee mchwa;

    zitafakari njia zake ukapate hekima!

    7 Kwa maana yeye hana msimamizi,

    wala mwangalizi, au mtawala,

    8 lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi

    na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

    9 Ewe mvivu, utalala hata lini?

    Utaamka lini kutoka usingizi wako?

    10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

    bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

    11 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

    na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

  17. 36 “Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.

  18. 16 Kisha akawaambia mfano huu: “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’

    18 “Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu za nafaka na kujenga nyingine kubwa zaidi na huko nitayahifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Nami nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, unywe, ufurahi.” ’

    20 “Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’

    21 “Hivyo ndivyo ilivyo kwa wale wanaojiwekea mali lakini hawajitajirishi kwa Mungu.”

  19. 1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. 2 Kwa maana asema:

    “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia,

    siku ya wokovu nilikusaidia.”

    Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa.