25 Bible Verses About Abortion

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Abortion
  1. 13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

    uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

    14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

    kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

    kazi zako ni za ajabu,

    ninajua hayo kikamilifu.

    15 Umbile langu halikufichika kwako,

    nilipoumbwa mahali pa siri.

    Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

    16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

    Siku zangu zote ulizonipangia

    ziliandikwa katika kitabu chako

    kabla haijakuwepo hata moja.

  2. 22 “Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. 23 Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, 24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 25 kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko.

  3. 4 Neno la Bwana lilinijia, kusema,

    5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

    kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

    nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

  4. 21 Isaki akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Bwana akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. 22 Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Bwana.

    23 Bwana akamjibu,

    “Mataifa mawili yamo tumboni mwako,

    na mataifa hayo mawili

    kutoka ndani yako watatenganishwa.

    Mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine,

    na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”

    24 Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. 25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina lake Esau. 26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo. Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.

  5. 39 Wakati huo Maria akajiandaa, akaharakisha kwenda katika mji mmoja kwenye vilima vya Uyahudi. 40 Akaingia nyumbani kwa Zekaria na kumsalimu Elizabeti. 41 Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. 43 Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44 Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45 Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.”

  6. 13 Usiue.

  7. 27 Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,

    kwa mfano wa Mungu alimuumba;

    mwanaume na mwanamke aliwaumba.

  8. 3 Wana ni urithi utokao kwa Bwana,

    watoto ni zawadi kutoka kwake.

    4 Kama mishale mikononi mwa shujaa

    ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

    5 Heri mtu ambaye podo lake

    limejazwa nao.

    Hawataaibishwa wanaposhindana

    na adui zao langoni.

  9. 7 Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

  10. 3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.

    4 “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. 5 Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.

    6 “Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu,

    damu yake itamwagwa na mwanadamu,

    kwa kuwa katika mfano wa Mungu,

    Mungu alimuumba mwanadamu.

  11. 15 Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, 16 “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” 17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. 18 Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

    19 Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

    20 Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. 21 Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.

  12. 31 Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”

  13. 13 “Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu,

    walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,

    14 nitafanya nini Mungu atakaponikabili?

    Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?

    15 Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu,

    si ndiye aliwaumba?

    Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote

    ndani ya mama zetu?

  14. 3 “Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo,

    ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli,

    ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba,

    nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.

    4 Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

    Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

    Nimewahuluku, nami nitawabeba,

    nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.

  15. 1 Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili,

    ninyi mataifa mlio mbali:

    Kabla sijazaliwa, Bwana aliniita,

    tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu.

    2 Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa,

    katika uvuli wa mkono wake akanificha;

    akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa,

    na kunificha katika podo lake.

    3 Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu,

    Israeli, ambaye katika yeye

    nitaonyesha utukufu wangu.”

  16. 13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yohana. 14 Yeye atakuwa furaha na shangwe kwako, nao watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. 15 Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Bwana, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji chochote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake.

  17. 10 Bwana akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. 11 Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako.

  18. 3 Malaika wa Bwana akamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na huna mtoto, lakini utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanaume. 4 Lakini ujihadhari sana usinywe mvinyo wala kileo kingine chochote, wala usile kitu chochote kilicho najisi, 5 kwa kuwa utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanaume. Wembe usipite kichwani pake, kwa kuwa huyo mwana atakuwa Mnadhiri wa Mungu, aliyewekwa wakfu kwa ajili ya Mungu tangu tumboni mwa mama yake, naye ataanza kuwaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti.”

  19. 37 Wakawatoa wana wao

    na binti zao dhabihu kwa mashetani.

    38 Walimwaga damu isiyo na hatia,

    damu za wana wao na binti zao,

    ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani,

    nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.

    39 Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda;

    kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.

  20. 5 Sasa Bwana asema:

    yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake,

    kumrudisha tena Yakobo kwake

    na kumkusanyia Israeli,

    kwa maana nimepata heshima machoni pa Bwana,

    naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;

  21. 13 Hili ndilo asemalo Bwana:

    “Kwa dhambi tatu za Amoni,

    hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

    Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi

    ili kuongeza mipaka yake.

  22. 73 Mikono yako ilinifanya na kuniumba,

    nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

  23. 8 Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria. 9 Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 10 Upendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo upendo ndio utimilifu wa sheria.

  24. 11 ukanivika ngozi na nyama,

    na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?

    12 Umenipa uhai na kunitendea wema,

    katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.

  25. 1 “Lakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu,

    Israeli, niliyemchagua.

    2 Hili ndilo asemalo Bwana,

    yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,

    yeye atakayekusaidia:

    Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu,

    Yeshuruni, niliyekuchagua.