41 Bible Verses About Bad Friends

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Bad Friends
  1. 33 Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.”

  2. 12 Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu. 16 Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi.

  3. 17 Rafiki hupenda wakati wote

    naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

  4. 24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka,

    usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,

    25 la sivyo utajifunza njia zake

    na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.

    26 Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani,

    au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.

    27 Kama ukikosa njia ya kulipa,

    kitanda chako

    kitachukuliwa ukiwa umekilalia.

  5. 19 Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi,

    bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.

    20 Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,

    bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.

    21 Balaa humwandama mtenda dhambi,

    bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.

  6. 5 Afadhali karipio la wazi

    kuliko upendo uliofichika.

    6 Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu,

    bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

  7. 24 Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,

    bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.

  8. 26 Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki,

    bali njia ya waovu huwapotosha.

  9. 28 Mtu mpotovu huchochea ugomvi,

    nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.

    29 Mtu mkali humvuta jirani yake

    na kumwongoza katika mapito yale mabaya.

  10. 9 Manukato na uvumba huleta furaha moyoni,

    nao uzuri wa rafiki huchipuka

    kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.

    10 Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,

    tena usiende nyumbani mwa ndugu yako

    wakati umepatwa na maafa.

    Bora jirani wa karibu

    kuliko ndugu aliye mbali.

  11. 17 Kama vile chuma kinoavyo chuma,

    ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.

  12. 9 Wawili ni afadhali kuliko mmoja,

    kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:

    10 Kama mmoja akianguka,

    mwenzake atamwinua.

    Lakini ni jambo la kuhuzunisha

    kwa mtu yule aangukaye

    naye hana wa kumwinua!

    11 Pia, kama wawili wakilala pamoja

    watapashana joto.

    Lakini ni vipi mtu aweza

    kujipasha joto mwenyewe?

    12 Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,

    watu wawili wanaweza

    kumkabili adui na kumshinda.

    Kamba ya nyuzi tatu

    haikatiki kwa urahisi.

  13. 9 Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,

    bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.

  14. 4 Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu.

  15. 12 Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia,

    kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu,

    ningejificha asinione.

    13 Kumbe ni wewe, mwenzangu,

    mshiriki na rafiki yangu wa karibu,

    14 ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,

    tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.

  16. 6 Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,

    bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.

    7 Kaa mbali na mtu mpumbavu,

    kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.

  17. 5 Adui zangu wanasema kwa hila,

    “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”

    6 Kila anapokuja mtu kunitazama,

    huzungumza uongo,

    huku moyo wake hukusanya masingizio;

    kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.

    7 Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu,

    hao huniwazia mabaya sana, wakisema,

    8 “Ugonjwa mbaya sana umempata,

    kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”

    9 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini,

    yule aliyekula chakula changu

    ameniinulia kisigino chake.

  18. 20 Mwenzangu hushambulia rafiki zake,

    naye huvunja agano lake.

    21 Mazungumzo yake ni laini kama siagi,

    hata hivyo vita vimo moyoni mwake.

    Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,

    hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.

  19. 16 Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.

  20. 5 Usimtumaini jirani;

    usiweke matumaini kwa rafiki.

    Hata kwa yule alalaye kifuani mwako

    uwe mwangalifu kwa maneno yako.

    6 Kwa kuwa mwana humdharau baba yake,

    naye binti huinuka dhidi ya mama yake,

    mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake:

    adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.

  21. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa kuwaambia kweli?

    17 Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku. 18 Ni vizuri wakati wote kuwa na shauku kwa ajili ya kusudi zuri, si wakati nikiwa pamoja nanyi tu. 19 Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara nyingine ninawaonea utungu, ninatamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20 Natamani kama ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha sauti yangu. Kwa maana nina wasiwasi kwa ajili yenu.

  22. 10 kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia.

  23. 16 Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu. 17 Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? 18 Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.

  24. 6 Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu, 7 miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine), 8 usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge. 9 Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumuua kisha mikono ya watu wengine wote. 10 Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwa Bwana Mungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. 11 Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.

  25. 11 Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji. 12 Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao. 13 Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

  26. 29 Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu. 30 Kama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu.

  27. 14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,

    hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.

    15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,

    ni kama vijito vya msimu,

    ni kama vijito ambavyo hufurika

    16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,

    ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,

    17 lakini hukauka majira ya ukame,

    na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.

  28. 19 Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa;

    wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.

  29. 8 Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,

    wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

    9 Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,

    na mkufu wa kuipamba shingo yako.

    10 Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,

    usikubaliane nao.

    11 Kama wakisema, “Twende tufuatane;

    tukamvizie mtu na kumwaga damu,

    njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

    12 tuwameze wakiwa hai kama kaburi,

    wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

    13 Tutapata aina zote za vitu vya thamani

    na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

    14 Njoo ushirikiane nasi,

    vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

  30. 1 Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji

    na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!

    Ningelia usiku na mchana

    kwa kuuawa kwa watu wangu.

    2 Laiti ningekuwa na nyumba

    ya kukaa wasafiri jangwani,

    ningewaacha watu wangu

    na kwenda mbali nao,

    kwa kuwa wote ni wazinzi,

    kundi la watu wadanganyifu.

    3 “Huweka tayari ndimi zao kama upinde,

    ili kurusha uongo;

    wamekuwa na nguvu katika nchi

    lakini si katika ukweli.

    Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,

    hawanitambui mimi,”

    asema Bwana.

    4 “Jihadhari na rafiki zako;

    usiwaamini ndugu zako.

    Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,

    na kila rafiki ni msingiziaji.

    5 Rafiki humdanganya rafiki,

    hakuna yeyote asemaye kweli.

    Wamefundisha ndimi zao kudanganya,

    wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.

  31. 14 Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani 15 na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16 Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu.

  32. 11 Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.

    12 Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kanisa? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani?

  33. 29 Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao. 30 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. 32 Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

  34. KITABU CHA KWANZA

    1 Heri mtu yule ambaye

    haendi katika shauri la watu waovu,

    wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,

    au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

    2 Bali huifurahia sheria ya Bwana,

    naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

    3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa

    kando ya vijito vya maji,

    ambao huzaa matunda kwa majira yake

    na majani yake hayanyauki.

    Lolote afanyalo hufanikiwa.

    4 Sivyo walivyo waovu!

    Wao ni kama makapi

    yapeperushwayo na upepo.

  35. 11 Rafiki na wenzangu wananikwepa

    kwa sababu ya majeraha yangu;

    majirani zangu wanakaa mbali nami.

  36. 6 Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi;

    tembeeni katika njia ya ufahamu.

  37. 4 Mali huleta marafiki wengi,

    bali rafiki wa mtu maskini humwacha.

  38. 16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa.

  39. 13 Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

  40. 7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.

  41. 6 Mtu yeyote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya wale wasiomtii.