23 Bible Verses About Summer

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Summer
  1. 22 “Kwa muda dunia idumupo,

    wakati wa kupanda na wa kuvuna,

    wakati wa baridi na wa joto,

    wakati wa kiangazi na wa masika,

    usiku na mchana

    kamwe havitakoma.”

  2. 5 Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi

    ni mwana mwenye hekima,

    lakini yeye alalaye wakati wa mavuno

    ni mwana mwenye kuaibisha.

  3. 12 Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani,

    unaleta wokovu duniani.

    13 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;

    ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

    14 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani

    nawe ukamtoa kama chakula

    kwa viumbe vya jangwani.

    15 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito,

    ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.

    16 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,

    uliziweka jua na mwezi.

    17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,

    ulifanya kiangazi na masika.

  4. 6 Ewe mvivu, mwendee mchwa;

    zitafakari njia zake ukapate hekima!

    7 Kwa maana yeye hana msimamizi,

    wala mwangalizi, au mtawala,

    8 lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi

    na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

  5. 32 “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 33 Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni.

  6. 18 Ee Mfariji wangu katika huzuni,

    moyo wangu umezimia ndani yangu.

    19 Sikia kilio cha watu wangu

    kutoka nchi ya mbali:

    “Je, Bwana hayuko Sayuni?

    Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”

    “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,

    kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

    20 “Mavuno yamepita,

    kiangazi kimekwisha,

    nasi hatujaokolewa.”

    21 Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia;

    ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika.

    22 Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi?

    Je, hakuna tabibu huko?

    Kwa nini basi hakuna uponyaji

    wa majeraha ya watu wangu?

  7. 25 Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo,

    hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.

  8. 29 Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. 30 Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. 31 Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.

  9. 1 Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: kikapu cha matunda yaliyoiva. 2 Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?”

    Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.”

    Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”

    3 Bwana Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!”

    4 Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji,

    na kuwaonea maskini wa nchi,

    5 mkisema,

    “Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita

    ili tupate kuuza nafaka,

    na Sabato itakwisha lini

    ili tuweze kuuza ngano?”

    Mkipunguza vipimo,

    na kuongeza bei,

    na kudanganya kwa mizani zisizo sawa,

    6 mkiwanunua maskini kwa fedha,

    na wahitaji kwa jozi ya viatu,

    na mkiuza hata takataka za ngano

    pamoja na ngano.

  10. 1 Taabu gani hii niliyo nayo!

    Nimefanana na yule akusanyaye

    matunda ya kiangazi,

    aokotaye masazo baada ya kuvunwa

    shamba la mizabibu;

    hakuna kishada chenye matunda ya kula,

    hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.

  11. 1 Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno,

    ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.

  12. 15 Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,

    pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;

    nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu

    na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”

    asema Bwana.

  13. 28 “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29 Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni.

  14. 35 Ndipo ile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja, na vikawa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote.

  15. 4 Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

    uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,

    litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:

    mara mtu aionapo, huichuma na kuila.

  16. 8 Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji

    uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.

    Hauogopi wakati wa joto ujapo;

    majani yake ni mabichi daima.

    Hauna hofu katika mwaka wa ukame

    na hautaacha kuzaa matunda.”

  17. 6 Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani

    na wanyama pori,

    ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,

    nao wanyama pori wakati wote wa masika.

  18. 14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,

    hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.

    15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,

    ni kama vijito vya msimu,

    ni kama vijito ambavyo hufurika

    16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,

    ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,

    17 lakini hukauka majira ya ukame,

    na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.

  19. 4 Usiku na mchana

    mkono wako ulinilemea,

    nguvu zangu zilinyonywa

    kama vile katika joto la kiangazi.

  20. 4 Hili ndilo Bwana aliloniambia:

    “Nitatulia kimya na kutazama

    kutoka maskani yangu,

    kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,

    kama wingu la umande

    katika joto la wakati wa mavuno.”

  21. 17 Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.

  22. 10 Mimi mwenyewe nitakaa Mispa ili kuwawakilisha mbele ya Wakaldayo wanaotujia, lakini ninyi mtavuna divai, matunda ya kiangazi na mafuta, nanyi mtaweka katika vyombo vyenu vya kuhifadhia, na kuishi katika miji mliyojitwalia.”

    11 Wayahudi wote waliokuwa Moabu, Amoni, Edomu na nchi nyingine zote waliposikia kwamba mfalme wa Babeli ameacha mabaki ya watu katika Yuda na amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kuwa mtawala wao, 12 wakarudi wote katika nchi ya Yuda kwa Gedalia huko Mispa, kutoka nchi zote ambazo walikuwa wametawanywa. Nao wakavuna divai na matunda tele wakati wa kiangazi.

  23. 8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki, na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi wakati wa kiangazi na wakati wa masika.