36 Bible Verses About Bitterness

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Bitterness
  1. 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao hakuna mtu atakayemwona Bwana. 15 Angalieni sana mtu yeyote asiikose neema ya Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. 16 Angalieni miongoni mwenu asiwepo mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja aliuza haki ya uzaliwa wake wa kwanza. 17 Baadaye kama mnavyofahamu, alipotaka kurithi ile baraka, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.

  2. 30 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. 32 Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

  3. 14 Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia. 15 Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

  4. 25 Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni mkiwa na neno na mtu, ili naye Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. [

  5. 20 Ole wao wanaoita ubaya ni wema,

    na wema ni ubaya,

    wawekao giza badala ya nuru,

    na nuru badala ya giza,

    wawekao uchungu badala ya utamu,

    na utamu badala ya uchungu.

  6. 26 Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, 27 wala msimpe ibilisi nafasi.

  7. 22 Kwa hiyo tubu kwa uovu huu wako na umwombe Bwana. Yamkini aweza kukusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako. 23 Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi.”

  8. 13 Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima. 14 Lakini ikiwa mna wivu na ni wenye chuki na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu kwa ajili ya hayo wala msiikatae kweli. 15 Hekima ya namna hiyo haishuki kutoka mbinguni, bali ni ya kidunia, isiyo ya kiroho, na ya kishetani. 16 Kwa maana panapokuwa na wivu na ubinafsi, ndipo penye machafuko na uovu wa kila namna.

    17 Lakini hekima itokayo mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki. 18 Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

  9. 19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.

  10. 22 Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. 23 Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara) 24 Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?”

    25 Ndipo Mose akamlilia Bwana, naye Bwana akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu.

    Huko Bwana akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. 26 Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”

    27 Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji.

  11. 14 “Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”

  12. 18 Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele za Bwana, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana. 19 Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.

  13. 1 “Nayachukia sana haya maisha yangu;

    kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia,

    nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.

  14. 10 Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe,

    wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake.

  15. 25 Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi,

    akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri.

  16. 25 Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake

    na uchungu kwa yeye aliyemzaa.

  17. 17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. 20 Badala yake:

    “Kama adui yako ana njaa, mlishe;

    kama ana kiu, mpe kinywaji.

    Kwa kufanya hivyo,

    unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”

    21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

  18. 19 Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika. 20 Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.

  19. 14 Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.

  20. 23 “ ‘Kuhani ataandika laana hizi kwenye kitabu, kisha atazioshea laana hizo kwenye yale maji machungu. 24 Kuhani atamnywesha yule mwanamke yale maji machungu yaletayo laana, nayo maji haya yatamwingia na kumsababishia maumivu makali.

  21. 11 Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Watamla mwana-kondoo, pamoja na mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu.

  22. 11 “Kwa hiyo sitanyamaza;

    nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu,

    nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.

  23. 13 Alinichoma moyo wangu kwa mishale

    iliyotoka kwenye podo lake.

    14 Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote,

    wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.

    15 Amenijaza kwa majani machungu

    na kunishibisha kwa nyongo.

  24. 12 Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. 14 Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.

  25. 34 Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”

  26. 8 Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu.

  27. 3 Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba

    hudondoza asali,

    na maneno ya kinywa chake

    ni laini kuliko mafuta;

    4 lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,

    mkali kama upanga ukatao kuwili.

  28. 11 Je, chemchemi yaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi?

  29. 11 Nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.

  30. Hotuba Ya Nane Ya Ayubu

    1 Ndipo Ayubu akajibu:

    2 “Hata leo malalamiko yangu ni chungu;

    mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.

    3 Laiti ningefahamu mahali pa kumwona;

    laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!

    4 Ningeliweka shauri langu mbele zake,

    na kukijaza kinywa changu na hoja.

  31. 19 Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,

    uchungu na nyongo.

    20 Ninayakumbuka vyema,

    nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.

  32. 10 Nitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo,

    na kuimba kwenu kote kuwe kilio.

    Nitawafanya ninyi nyote mvae nguo ya gunia

    na kunyoa nywele zenu.

    Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee,

    na mwisho wake kama siku ya uchungu.

  33. 1 Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu.

  34. 12 Chuki huchochea faraka,

    lakini upendo husitiri mabaya yote.

  35. 7 Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali,

    bali kwa mwenye njaa

    hata kile kilicho kichungu

    kwake ni kitamu.

  36. 26 Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti,

    mwanamke ambaye ni mtego,

    ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea

    na mikono yake ni minyororo.

    Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa,

    bali mwenye dhambi atanaswa naye.