15 Bible Verses About Creativity

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bible Verses About Creativity
  1. 30 Kisha Mose akawaambia Waisraeli, “Tazameni, Bwana amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 31 naye amemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, na uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 32 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 33 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi wa kupendeza. 34 Tena amempa yeye pamoja na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, uwezo wa kufundisha wengine. 35 Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zifanywazo na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari.

  2. 26 Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.”

    27 Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,

    kwa mfano wa Mungu alimuumba;

    mwanaume na mwanamke aliwaumba.

    28 Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”

    29 Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. 30 Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.

  3. 15 “Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,

    niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe,

    anayekula majani kama ngʼombe.

    16 Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,

    uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

    17 Mkia wake hutikisika kama mwerezi;

    mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.

    18 Mifupa yake ni bomba za shaba,

    maungo yake ni kama fito za chuma.

    19 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,

    lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.

    20 Vilima humletea yeye mazao yake,

    nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.

    21 Hulala chini ya mimea ya yungiyungi,

    katika maficho ya matete kwenye matope.

    22 Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;

    miti mirefu karibu na kijito humzunguka.

    23 Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;

    yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.

    24 Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,

    au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

  4. 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. 2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

    3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 4 Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

    6 Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” 7 Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.

  5. 13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

    uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

    14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

    kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

    kazi zako ni za ajabu,

    ninajua hayo kikamilifu.

    15 Umbile langu halikufichika kwako,

    nilipoumbwa mahali pa siri.

    Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

    16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

    Siku zangu zote ulizonipangia

    ziliandikwa katika kitabu chako

    kabla haijakuwepo hata moja.

    17 Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu!

    Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

    18 Kama ningezihesabu,

    zingekuwa nyingi kuliko mchanga.

    Niamkapo,

    bado niko pamoja nawe.

  6. 10 Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.

  7. 7 Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza,

    ninaleta mafanikio na kusababisha maafa.

    Mimi, Bwana, huyatenda haya yote.

    8 “Enyi mbingu juu, nyesheni haki,

    mawingu na yaidondoshe.

    Dunia na ifunguke sana,

    wokovu na uchipuke,

    haki na ikue pamoja nao.

    Mimi, Bwana, ndiye niliyeiumba.

    9 “Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,

    yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.

    Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,

    ‘Unatengeneza nini wewe?’

    Je, kazi yako husema,

    ‘Hana mikono’?

    10 Ole wake amwambiaye baba yake,

    ‘Umezaa nini?’

    Au kumwambia mama yake,

    ‘Umezaa kitu gani?’

    11 “Hili ndilo asemalo Bwana,

    yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake:

    Kuhusu mambo yatakayokuja,

    je, unaniuliza habari za watoto wangu,

    au kunipa amri kuhusu kazi za mikono yangu?

    12 Mimi ndiye niliyeumba dunia

    na kumuumba mwanadamu juu yake.

    Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu,

    nikayapanga majeshi yake yote ya angani.

  8. 29 Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake?

    Atahudumu mbele ya wafalme;

    hatahudumu mbele ya watu duni.

  9. 15 Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16 wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”

  10. 7 Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

  11. 1 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.

    3 Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa. 4 Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, 5 vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake. 6 Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani. 7 Kama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe, 8 kama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha.

  12. 14 Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono.

    15 Uwe na bidii katika mambo haya; ujitolee kwa ajili ya mambo haya kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea kwako.

  13. 19 Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,

    naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu

    na kuitengenezea mikufu ya fedha.

    20 Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii

    huuchagua mti usiooza.

    Humtafuta fundi stadi

    wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.

  14. 10 Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,

    ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote?

    11 Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,

    mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.

    Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,

    watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.

    12 Muhunzi huchukua kifaa

    na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto,

    hutengeneza sanamu kwa nyundo,

    huifanyiza kwa nguvu za mkono wake.

    Huona njaa na kupoteza nguvu zake,

    asipokunywa maji huzimia.

    13 Seremala hupima kwa kutumia kamba

    na huuchora mstari kwa kalamu;

    huchonga kwa patasi

    na kutia alama kwa bikari.

    Huifanyiza katika umbo la binadamu,

    la mwanadamu katika utukufu wake wote,

    ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.

  15. 20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.