Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 63

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Shauku Kwa Ajili Ya Uwepo Wa Mungu

Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda.

1 Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,

nakutafuta kwa moyo wote;

nafsi yangu inakuonea kiu,

mwili wangu unakuonea wewe shauku,

katika nchi kame na iliyochoka

mahali ambapo hapana maji.

2 Nimekuona katika mahali patakatifu

na kuuona uwezo wako na utukufu wako.

3 Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,

midomo yangu itakuadhimisha.

4 Nitakusifu siku zote za maisha yangu,

na kwa jina lako nitainua mikono yangu.

5 Nafsi yangu itatoshelezwa

kama kwa wingi wa vyakula;

kwa midomo iimbayo

kinywa changu kitakusifu wewe.

6 Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe,

ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.

7 Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,

chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.

8 Nafsi yangu inaambatana nawe,

mkono wako wa kuume hunishika.

9 Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa,

watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.

10 Watatolewa wafe kwa upanga,

nao watakuwa chakula cha mbweha.

11 Bali mfalme atafurahi katika Mungu,

wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,

bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.

Zaburi 63