Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 54

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kutokana Na Adui

Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?”

1 Ee Mungu uniokoe kwa jina lako,

unifanyie hukumu kwa uwezo wako.

2 Ee Mungu, sikia maombi yangu,

usikilize maneno ya kinywa changu.

3 Wageni wananishambulia,

watu wakatili wanayatafuta maisha yangu,

watu wasiomjali Mungu.

4 Hakika Mungu ni msaada wangu,

Bwana ndiye anayenitegemeza.

5 Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia,

kwa uaminifu wako uwaangamize.

6 Nitakutolea dhabihu za hiari;

Ee Bwana, nitalisifu jina lako

kwa kuwa ni vyema.

7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote,

na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.

Zaburi 54