Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 111

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu

1 aMsifuni Bwana.

Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote,

katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

2 Kazi za Bwana ni kuu,

wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.

3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu,

haki yake hudumu daima.

4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe,

Bwana ni mwenye neema na huruma.

5 Huwapa chakula wale wanaomcha,

hulikumbuka agano lake milele.

6 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,

akiwapa nchi za mataifa mengine.

7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,

mausia yake yote ni ya kuaminika.

8 Zinadumu milele na milele,

zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.

9 Aliwapa watu wake ukombozi,

aliamuru agano lake milele:

jina lake ni takatifu na la kuogopwa.

10 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

wote wanaozifuata amri zake wana busara.

Sifa zake zadumu milele.

Translator’s notes

  1. 111 (a): Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

Zaburi 111