Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 110

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Bwana Na Mfalme Wake Mteule

Zaburi ya Daudi.

1 Bwana amwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

mpaka nitakapowafanya adui zako

kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”

2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;

utatawala katikati ya adui zako.

3 Askari wako watajitolea kwa hiari

katika siku yako ya vita.

Ukiwa umevikwa fahari takatifu,

kutoka tumbo la mapambazuko

utapokea umande wa ujana wako.a

4 Bwana ameapa,

naye hatabadilisha mawazo yake:

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,

atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga

na kuwaponda watawala wa dunia nzima.

7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,b

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Translator’s notes

  1. 110:3 (a): Au: vijana wako watakujia kama umande.
  2. 110:7 (b): Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.

Zaburi 110