Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 29

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba

Zaburi ya Daudi.

1 Mpeni Bwana, enyi mashujaa,

mpeni Bwana utukufu na nguvu.

2 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;

mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.

3 Sauti ya Bwana iko juu ya maji;

Mungu wa utukufu hupiga radi,

Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.

4 Sauti ya Bwana ina nguvu;

sauti ya Bwana ni tukufu.

5 Sauti ya Bwana huvunja mierezi;

Bwana huvunja vipande vipande

mierezi ya Lebanoni.

6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,

Sirionia urukaruke kama mwana nyati.

7 Sauti ya Bwana hupiga kwa miali

ya umeme wa radi.

8 Sauti ya Bwana hutikisa jangwa;

Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.

9 Sauti ya Bwana huzalisha ayala,

na huuacha msitu wazi.

Hekaluni mwake wote wasema,

“Utukufu!”

10 Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;

Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.

11 Bwana huwapa watu wake nguvu;

Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.

Translator’s notes

  1. 29:6 (a): Yaani Mlima Hermoni.

Zaburi 29