Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 77

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Matendo Makuu Ya Mungu Yanakumbukwa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu.

1 Nilimlilia Mungu ili anisaidie,

nilimlilia Mungu ili anisikie.

2 Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana,

usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka

na nafsi yangu ilikataa kufarijika.

3 Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni;

nikatafakari, roho yangu ikadhoofika.

4 Ulizuia macho yangu kufumba;

nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema.

5 Nilitafakari juu ya siku zilizopita,

miaka mingi iliyopita,

6 nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku.

Moyo wangu ulitafakari

na roho yangu ikauliza:

7 “Je, Bwana atakataa milele?

Je, hatatenda mema tena?

8 Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele?

Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

9 Je, Mungu amesahau kuwa na huruma?

Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

10 Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu:

lakini nitakumbuka

miaka ya mkono wa kuume

wa Aliye Juu Sana.”

11 Nitayakumbuka matendo ya Bwana;

naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

12 Nitazitafakari kazi zako zote

na kuyawaza matendo yako makuu.

13 Ee Mungu, njia zako ni takatifu.

Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

14 Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza,

umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

15 Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako,

uzao wa Yakobo na Yosefu.

16 Maji yalikuona, Ee Mungu,

maji yalikuona yakakimbia,

vilindi vilitetemeka.

17 Mawingu yalimwaga maji,

mbingu zikatoa ngurumo kwa radi,

mishale yako ikametameta huku na huko.

18 Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli,

umeme wako wa radi ukaangaza dunia,

nchi ikatetemeka na kutikisika.

19 Njia yako ilipita baharini,

mapito yako kwenye maji makuu,

ingawa nyayo zako hazikuonekana.

20 Uliongoza watu wako kama kundi

kwa mkono wa Mose na Aroni.

Zaburi 77