Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 47

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Mtawala Mwenye Enzi Yote

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

1 Pigeni makofi, enyi mataifa yote,

mpigieni Mungu kelele za shangwe!

2 Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana,

Mfalme mkuu juu ya dunia yote!

3 Ametiisha mataifa chini yetu

watu wengi chini ya miguu yetu.

4 Alituchagulia urithi wetu,

fahari ya Yakobo, aliyempenda.

5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

Bwana kwa sauti za tarumbeta.

6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,

mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.

7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,

mwimbieni zaburi za sifa.

8 Mungu anatawala juu ya mataifa,

Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.

9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika

kama watu wa Mungu wa Abrahamu,

kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;

yeye ametukuka sana.

Zaburi 47