Search Help

Search the whole Bible in your chosen Translation.

1. Find Verses Using Words

Examples:

Notes:

2. Find Verses Using Advanced Matching

Finds baptism, baptize, baptized, baptizing

Finds love, loved, loving

3. Find a passage

Opens John chapter 3.

Opens John 3, verses 16–17. A book name on its own, such as "John", searches for that word.

Zaburi 87

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Sifa Za Yerusalemu

Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni

kuliko makao yote ya Yakobo.

3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,

ee mji wa Mungu:

4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabua na Babeli

miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:

Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,b

nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,

“Huyu na yule walizaliwa humo,

naye Aliye Juu Sana mwenyewe

atamwimarisha.”

6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:

“Huyu alizaliwa Sayuni.”

7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,

“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Translator’s notes

  1. 87:4 (a): Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.
  2. 87:4 (b): Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.

Zaburi 87