Maandalizi ya Huduma ya Hekalu

1015 KK

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

1 Nyakati 23:2–24:31

2 Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 3 Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. 4 Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, 5 na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

6 Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

7 Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:

Ladani na Shimei.

8 Wana wa Ladani walikuwa watatu:

Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.

9 Wana wa Shimei walikuwa watatu:

Shelomothi, Hazieli na Harani.

Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.

10 Nao wana wa Shimei walikuwa wanne:

Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.

11 Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

13 Wana wa Amramu walikuwa:

Aroni na Mose.

Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele. 14 Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.

15 Wana wa Mose walikuwa:

Gershomu na Eliezeri.

16 Wazao wa Gershomu:

Shebueli alikuwa wa kwanza.

17 Wazao wa Eliezeri:

Rehabia alikuwa wa kwanza.

Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

18 Wana wa Ishari:

Shelomithi alikuwa wa kwanza.

19 Wana wa Hebroni walikuwa:

Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.

20 Wana wa Uzieli walikuwa:

Mika wa kwanza na Ishia wa pili.

21 Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Wana wa Mahli walikuwa:

Eleazari na Kishi.

22 Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

23 Wana wa Mushi:

Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.

24 Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana. 25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, 26 Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.” 27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

28 Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu. 29 Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa. 30 Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni 31 na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

32 Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana.

24:1 Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. 3 Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. 4 Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. 5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

6 Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

7 Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,

ya pili Yedaya,

8 ya tatu Harimu,

ya nne Seorimu,

9 ya tano Malkiya,

ya sita Miyamini,

10 ya saba Hakosi,

ya nane Abiya,

11 ya tisa Yeshua,

ya kumi Shekania,

12 ya kumi na moja Eliashibu,

ya kumi na mbili Yakimu,

13 ya kumi na tatu Hupa,

ya kumi na nne Yeshebeabu,

14 ya kumi na tano Bilga,

ya kumi na sita Imeri,

15 ya kumi na saba Heziri,

ya kumi na nane Hapisesi,

16 ya kumi na tisa Pethahia,

ya ishirini Yehezkeli,

17 ya ishirini na moja Yakini,

ya ishirini na mbili Gamuli,

18 ya ishirini na tatu Delaya,

ya ishirini na nne Maazia.

19 Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

20 Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:

Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;

kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.

21 Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:

Ishia alikuwa wa kwanza.

22 Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,

kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.

23 Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

24 Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;

kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.

25 Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;

na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.

26 Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.

Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.

27 Wana wa Merari:

kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.

28 Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.

29 Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:

alikuwa Yerameeli.

30 Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.

Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. 31 Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.