Ahazi Anaungana na Tiglath-Pileseri (continued)

Ahazi anafanya muungano na Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru.

740 KK

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

Hosea 6

1 “Njooni, tumrudie Bwana.

Ameturarua vipande vipande

lakini atatuponya;

ametujeruhi lakini

atatufunga majeraha yetu.

2 Baada ya siku mbili atatufufua;

katika siku ya tatu atatuinua,

ili tuweze kuishi mbele zake.

3 Tumkubali Bwana,

tukaze kumkubali yeye.

Kutokea kwake ni hakika kama vile

kuchomoza kwa jua;

atatujia kama mvua za masika,

kama vile mvua za vuli

ziinyweshavyo nchi.”

4 “Nifanye nini nawe, Efraimu?

Nifanye nini nawe, Yuda?

Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,

kama umande wa alfajiri utowekao.

5 Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande

kwa kutumia manabii wangu;

nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,

hukumu zangu zinawaka

kama umeme juu yenu.

6 Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,

kumkubali Mungu zaidi

kuliko sadaka za kuteketezwa.

7 Wamevunja Agano kama Adamu:

huko hawakuwa waaminifu kwangu.

8 Gileadi ni mji wenye watu waovu,

umetiwa madoa kwa nyayo za damu.

9 Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu,

ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;

wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,

wakifanya uhalifu wa aibu.

10 Nimeona jambo la kutisha

katika nyumba ya Israeli.

Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba

na Israeli amenajisika.

11 “Pia kwa ajili yako, Yuda,

mavuno yameamriwa.

“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,

Ahazi Anakufa; Nguvu za Hezekia Zinatabiriwa 726 KK

Kifo cha Ahazi, na utabiri wa nguvu za Hezekia.

2 Nyakati 28:26–27

26 Matukio mengine ya utawala wake na njia zake nyingine zote, tangu mwanzo hadi mwisho, zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 27 Ahazi akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Isaya 14:28–32

28 Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki:

29 Msifurahi, enyi Wafilisti wote,

kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika;

kutoka mzizi wa huyo nyoka

atachipuka nyoka mwenye sumu kali,

uzao wake utakuwa joka lirukalo,

lenye sumu kali.

30 Maskini kuliko maskini wote watapata malisho,

nao wahitaji watalala salama.

Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa,

nayo njaa itawaua walionusurika.

31 Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji!

Yeyukeni, enyi Wafilisti wote!

Wingu la moshi linakuja toka kaskazini,

wala hakuna atakayechelewa katika safu zake.

32 Ni jibu gani litakalotolewa

kwa wajumbe wa taifa hilo?

“Bwana ameifanya imara Sayuni,

nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

2 Nyakati 28:1–3

1 Ahazi alikuwa na miaka ishirini alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Bwana. 2 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na pia akasubu sanamu kwa ajili ya kuabudu Mabaali. 3 Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Ben-Hinomu, na kuwatoa wanawe kafara kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa Bwana aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli.

2 Wafalme 16:19–20

19 Matukio mengine ya utawala wa Ahazi na yale aliyoyafanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 20 Ahazi akalala na baba zake, naye akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Ufalme wa Israeli 739 KK

Tawala za Peka na Hoshea

2 Wafalme 15:30–31

30 Kisha Hoshea mwana wa Ela akafanya shauri baya dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akamshambulia na kumuua, kisha akaingia mahali pake kuwa mfalme katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.

31 Matukio mengine ya utawala wa Peka na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

2 Wafalme 17:1–2

1 Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Ahazi mfalme wa Yuda, Hoshea mwana wa Ela akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, akatawala kwa miaka tisa. 2 Akafanya maovu machoni pa Bwana, lakini si kama wafalme wengine wa Israeli waliomtangulia.