Nasaba Tofauti, Mifuatano Tofauti ya Urithi, na Matukio Tofauti (continued)

Nasaba tofauti, mifuatano tofauti ya urithi, na matukio tofauti, ambayo yaelekea yaliingizwa wakati kanoni ilipokamilika.

karibu 300 KK

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (OKCV)

1 Nyakati 3–4

1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:

Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli;

wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;

2 wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;

wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;

3 wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali;

wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.

4 Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.

Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu, 5 nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:

mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Solomoni. 6 Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti, 7 Noga, Nefegi, Yafia, 8 Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa. 9 Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.

10 Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu,

mwanawe huyo alikuwa Abiya,

mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati,

mwanawe huyo alikuwa Asa,

11 mwanawe huyo alikuwa Yehoramu,

mwanawe huyo alikuwa Ahazia,

mwanawe huyo alikuwa Yoashi,

12 mwanawe huyo alikuwa Amazia,

mwanawe huyo alikuwa Azaria,

mwanawe huyo alikuwa Yothamu,

13 mwanawe huyo alikuwa Ahazi,

mwanawe huyo alikuwa Hezekia,

mwanawe huyo alikuwa Manase,

14 mwanawe huyo alikuwa Amoni

na mwanawe huyo alikuwa Yosia.

15 Wana wa Yosia walikuwa:

Yohanani mzaliwa wake wa kwanza,

Yehoyakimu mwanawe wa pili,

wa tatu Sedekia,

wa nne Shalumu.

16 Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:

Yekonia mwanawe,

na Sedekia.

17 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:

Shealtieli mwanawe, 18 Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.

19 Wana wa Pedaya walikuwa:

Zerubabeli na Shimei.

Wana wa Zerubabeli walikuwa:

Meshulamu na Hanania.

Shelomithi alikuwa dada yao.

20 Pia walikuwepo wengine watano:

Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.

21 Wazao wa Hanania walikuwa:

Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.

22 Wazao wa Shekania:

Shemaya na wanawe:

Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.

23 Wana wa Nearia walikuwa:

Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.

24 Wana wa Elioenai walikuwa:

Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.

4:1 Wana wa Yuda walikuwa:

Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.

2 Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi.

3 Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu:

Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. 4 Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha.

Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.

5 Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

6 Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.

7 Wana wa Hela walikuwa:

Serethi, Sohari, Ethnani, 8 na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.

9 Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” 10 Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

11 Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni. 12 Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka.

13 Wana wa Kenazi walikuwa:

Othnieli na Seraya.

Wana wa Othnieli walikuwa:

Hathathi na Meonathai. 14 Meonathai akamzaa Ofra.

Seraya akamzaa Yoabu,

baba wa Ge-Harashimu. Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi.

15 Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu:

Iru, Ela na Naamu.

Naye mwana wa Ela alikuwa:

Kenazi.

16 Wana wa Yahaleleli walikuwa:

Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.

17 Wana wa Ezra walikuwa:

Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa. 18 Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.

19 Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa:

baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.

20 Wana wa Shimoni walikuwa:

Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni.

Wazao wa Ishi walikuwa:

Zohethi na Ben-Zohethi.

21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa:

Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea, 22 Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.) 23 Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme.

24 Wazao wa Simeoni walikuwa:

Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.

25 Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.

26 Wazao wa Mishma walikuwa:

Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.

27 Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda. 28 Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali, 29 Bilha, Esemu, Toladi, 30 Bethueli, Horma, Siklagi, 31 Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi. 32 Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani; jumla miji mitano: 33 pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baali. Haya yalikuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao.

34 Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia, 35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli. 36 Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya, 37 Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.

38 Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana, 39 wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. 40 Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.

41 Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao. 42 Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri. 43 Wakawaua Waamaleki waliobaki, waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo.